Soma kwa nini wenye shahada nchini kenya wanaishi katika maisha duni

Muhtasari
  • Sababu 7 kwanini wenye shahada wanaishi maisha duni licha ya wao kuwa na fursa maishani mwao
  • Kuna wale wanategemea shahada yao bila ya kutambua talanta na vipaji vyao
Graduation
Graduation

Tumewaona wakiwa mitaani wakitafuta kazi na hata kwenye mitandao wakisema kwamba wana shahda ya chuo kikuu lakini hawajafanikiwa kupata kazi.

Ni swali ambalo wengi ujiuliza kwanini wenye shahada ya chuo kikuu wanaishi maisha duni licha ya wao kuhitimu na kuwa na elimu.

Hizi hapa sababu kwanini wanaishi katika maisha duni pamoja na familia zao;

1.Hawafikirii zaidi ya vyeti vyao

Wengi hutegemea kilicho kwenye vyeti vyao vya shahada yao, hawajui kufikiria kama wanaweza kufanya biashara ili kujikimu maisha.

Wanajua tu cheti chao kitawatete kila mahali.

2.Huwa wanapea vyeti vya kipaumbele kuliko talanta zao

Ndio utampata ana shahada lakini haimsaidii ilhali anakipaji ambacho anaweza kupata riziki ya kila siku lakini hana haja na talanta yake anataka tu kupata kazi ambayo alisomea kwenye chuo kikuu.

3. Vyeti vyao huwatayarisha katika ulimwengi haupo

Kwa sasa wenye shahada wamo nje wakitafuta kazi ilhali hamna kazi kama vile wengi wanadai, ulimwengu wa kazi yao ulikwisha kitambo ilhali hawafahamu hayo na kufikiria vingiine.

4.Hawajijui ilhali wanajua mambo mengi

Kwanza unapaswa kujijua wewe ni nani na unaweza kufanya nini na shahada yako au mbali na shahada yako utapata riziki aje.

Lakini kwa mara nyingi wenye shahada hawajifahamu katika ulimwengu wao lakini wanajua mengi kuhusu elimu yao.

Ukijafahamu wewe ni nani na unataka nini maishani utafaulu.

5.Vyeti vyao huwatayarisha kutafuta ulinzi kuliko kuchukua tendo la ujasiri

Kama wataka kufaulu maishaini chukua tendo la ujasiri anza biashara wacha kukaa ungoje uitwe ofisini ambapo ulienda kutafuta kazi.

6.Digrii na vyeti vinaweza kuua mipango

Vinaweza kuua mipango aje najua wajiuliza hivyo, endapo umeanza biashara na mara ya kwanza ikose kutoa faida ambayo ulikuwa umepanga haya basi utafikira una digrii ambayo unapaswa kutafuta kazi na kuacha biashara ambayo ingenawiri kwa siku chache zijazo.

7.Gigrii na vyetu ukutayarisha kutafuta kazi na wala sio fursa

Ukweli ni kwamba wengi utafuta kazi na wala sio fursa ambayo unahitaji maishani mwako na unaishi katika maisha duni mika na mikaka.