Zawadi unaweza kumnunulia mpenzi wako wa kiume siku ya wapendanao

Muhtasari
  • Zawadi unaweza mnunulia mpenzi wako wa kiume siku ya wapendanao

Huku wengi wakijitayarisha kwa ajili ya siku ya wapendanao ambayo husheherekewa kila tarehe 14 Februari kila mwaka wengi wanatarajia zawadi utoka kwa wapenzi wao.

Wanaume wengi huwanunulia wapenzi wao zawadi tofauti kama vile maua,saa, na zawadi zinginee nyingi.

Lakini wanawake kwanini mwaka huu usimnunulie mume wako zawadi badal ya yake kukununulia?

 

Haya basi kama umeamua kumnunulia mume wako au mpenzi wako wa kiume zawadi si ya wapendanao hizi hapa baadi ya zawadi ambao unapswa kumnunulia.

1.Saa

Nenda kwenye duka la kuuza saa chagua saa nzuri na yenye kupendeza mpe mumeo au mpenzi wako siku ya wapendanao.

2.Kifaa cha kunyoa

Usimuache mpenzi wako akae na nywele, kama mwizi au mtu hajielewi kama hana kifaa cha kunyoa ndevu basi jukumu ni lako umnunulie na kumpelekea siku ya valentines.

3.Nguo 

Kama kwa kweli unampenda mpenzi wako nenda kwenye duka la kuuza nguo mnunulie nguo kutoka juu hadi chini na hata viatu, kwa hakika atazidi kukupenda kwa maana umemuonyesha kuwa unamjali.

 

4.Mpeleke akajivinjari

Ndio unaweza kuwa huna pesa za nguo wala zawadi nyingine lakini una za kuenda kutembea, mtembeze basi na aweze kujivinjari siku hiyo.

5.Miwani

Miwani si mbaya ukimununulia mume wako au mpenzi wako ya maridadi tu.