Ndoa ilivunjika kabla ya kuanza

Masaibu:' Usiku wa honeymoon,niligundua ana sehemu mbili za siri’

‘Niko sawa ,lakini tunafaa tuzungumze.Kuna jambo ambalo unafaa ujue’ Bernice alijibu .

Muhtasari
  • Ben  alipatwa na mshutuko  na pale pale kumbukumbu zote za jinsi hawajawahi kuoga pamoja kama wapenzi na  hata hajawahi kumwona Bernice uchi zilimjia .
  • Akakumbuka  jinsi mkewe alivyokuwa akikwepa  Ben asimuone akiwa uchi .hapo ndipo alipojua kweli sababu ya  mkewe kukataa sionekane naye uchi .

Ushawahi  kusikia kuhusu ndoa iliyodumu muda mfupi zaidi ? kama hujawahi kufikiria kuhusu  ufupi wa ndoa basi  masaibu yaliomkumba Ben na mpenzi wake Bernice yatakushangaza na kukuacha kinywa wazi .

Baada ya Uchumba uliodumu miezi sita ,wawili hao waliamua kwamba itakuwa dhambi kushiriki mapenzi bila kwanza kufunga ndoa . Ben na Bernice walikutana kanisani na  uhusiano wao ulianza kama urafiki kabla ya kuboreka na kuwa  wapenzi . Hakuna aliyeweza kuwatenganisha wawili hao na wenzao kanisani waliwatazama kama  kielelezo cha jinsi wapendanao wanavyofaa kuishi .  Harusi kubwa ilipangwa na   wapenzi hawakuwa na shaka kwamba ndoa yao itakuwa bora na itadumu lakini   mipango ya binadamu ,Mola keshaijua .Siku ya siku ilipofika  walifunga pingu za maisha . Kila kitu kilionekana kwenda kwa njia safi na hata mipango ya jinsi watakavyoishi  baada ya fungate  au honeymoon ilikuwa ishafanywa . Urembo wa Bernice uliwavutia wengi  na Ben alijiona kama mtu mwenye  bahati kubwa sana kuweza kupendwa na  kipusa huyo ambaye kulikuwa  na stori nyingi za jinsi alivyowakataa wanaume wengi waliotaka kumuuoa . Bernice  alikuwa mtu wa kipekee ,hakuwa na rafiki  hata mmoja wa kike na Ben alijiambia kwamba hilo sio jambo la kumpa wasi wasi kwa sababu huenda ni maumbile yake kutaka kujifanyia mambo yake kivyake .

Kwa sababu ya msaada mkubwa waliopewa na kanisa katika kufanikisha ndoa yao,Ben na Bernice waliambiwa na viongozi wa kanisa lao kwamba hawatatoa hata shilingi moja kwa harusi yao ila watayarishe tu hela za kwenda honeymoon ! wapenzi walifurahi na hata wakaamua  eneo ambako watasafiri kwenda fungate yao .Ikaamuliwa kwamba baada ya harusi basi wangesafiri kwenda  Singapore kwa muda wa wiki tatu kabla ya kurejea na kuanza maisha rasmi kama mke na mume . Ben alijawa furaha akijua kwamba wakati wa honeymoon ndipo atapokuwa akifanya tendo la ndoa na mke wake kwa mara ya kwanza ,na pia Bernice alikuwa amemweleza kwamba yeye alikuwa bikra . Bahati iliyoje kwa mwanamke wa umri kama wa Bernice kuwa bikra ,kweli nimebahatika mimi! alijiambia kimoyomoyo .

Walipofika  Singapore katika  hoteli ambayo wangeiita makao yao  kwa wiki tatu Ben na Bernice walifahamu kwamba kuna jambo ambalo lazima lingeziteka ndimi zao –kushiriki mapenzi ila  Ben aligundua kwamba mke wake hakuwa  na kasi ya kuzungumzia suala hilo wala hata kuonyesha  daalili kwamba wangeshiri  mapenzi .  Kwa muda mfupi waliokuwa katika chumba cha hoteli yao alijihisi ni kana kwamba yupo mle ndani na dadake! Usiku ulipowadia , Ben keshajivua  nguo zote huku damu ikimpa msukumo  na kuufanya moyo wake kupiga kwa kasi .Kungoja kwake kwa zaidi ya miezi saba sasa kulikuwa kumefika tamati! Hatimaye anaifanya ndoa yake kuwa rasmi kwa kumpa penzi moto moto mkewe! Dunia ina ukatili,na hakuna anayekutayarish a kwa ukatili huo . Bernice alipoingia kitandani ,alionekana kutetemeka na kuzongwa na wasiwasi .

‘Kuna tatizo? Mbona unaonekana kuwa na wasi wasi ?’ Ben alimuuliza .

‘Niko sawa ,lakini tunafaa tuzungumze.Kuna jambo ambalo unafaa ujue’ Bernice alijibu .

Ben alipomuangalia mkewe kwa karibu na kumuona akitokwa machozi alijua hapa kuna habari mbaya .Lakini alishangaa mbona habari hiyo mbaya ilikuwa ilkija wakati huu na sio  muda wote ambao walikuwa na  Bernice .

‘  Ben , kwanza nataka ujue kwamba  nakupenda sana na wewe ndiye mwanamme wa kwanza ambaye nimekubali kumfungulia moyo wangu’. Bernice Alianza

‘ Najua  usiku wa leo ni wetu wa kwanza kushiriki tendo la ndoa .Na umeingoja sana siku hii .Ila ningependa ujue kwamba  mimi ni huntha.Nina sehemu mbili za siri ,ya  mwanamke na ya mwanamme’. Bernice alifichua . Ben  alipatwa na mshutuko  na pale pale kumbukumbu zote za jinsi hawajawahi kuoga pamoja kama wapenzi na  hata hajawahi kumwona Bernice uchi zilimjia . Akakumbuka  jinsi mkewe alivyokuwa akikwepa  Ben asimuone akiwa uchi .hapo ndipo alipojua kweli sababu ya  mkewe kukataa sionekane naye uchi .Alikuwa na haya ya kusema kwamba  ana sehemu mbili tofauti za siri !

‘Bernice,Lakini mbona unaniambia hayo  sasa .baada ya kufunga ndoa na kufika honeymoon?’ Hilo ndilo swali pekee ambalo Ben aliweza kujikakamua kumuuliza mkewe. Uchungu mkali ulimpitia mwili mzima asikose kujua mbona  Bernice alingoja hadi wakati huu ili kumfichulia jambo kubwa kama hilo . Ben alichukulia kisa hicho kizima kama usaliti mkubwa wa penzi .Alionekana kana kwamba alitumiwa vibaya lakini hakuwa tayari  kukubali kwamba mke wake ni  huntha. Juhudi za Bernice kujaribu kumweleza kwamba aliogopa angemuacha iwapo angesema ukweli mapema ziliambulia patupu .Ben alifunga virago vyake na kumuambia Bernice anarejea nyumbani Kenya . Ndoa yao ilikuwa imekwisha!