Kwa sababu ya kutaka kupendwa

Mnafanyiwa vitu vya kiajabu-chupi ndani ya chai ?

aribio lake la kujaribu kujitetea halikusikizwa kwa sababu sam alitoka nje na kuimwaga ile chai na kwenda kazini

Muhtasari
  • Hapo ndipo Irene alishawishika kujaribu kufanya hivo na siku yake ya 40 ikawadia .
  • Mengi pia hufanyika na uchunguzi katika makundi haya  ya akina dada pia yatakupa taswira ya kuogofya kuhusu wanayofanya baadhi ya wanawake ili kupendwa zaidi na wanaume .

Kuna vitu vya ajabu ambavyo watu hufanya ili kuwateka wenzao kimapenzi lakini hakuna kilichovunja uhusiano wa Irene kwa ghafla baada ya kupatikana  na mpenzi wake akiiweka  chupi yake katika  chai yake .

Yote yalianza katika ukumbi mmoja wa whatsapp ambapo Irene na wanawake wenzake walikuwa wakijadili njia nyingi ambazo wao hutumia ili  kuwanata wanaume wao. Zaidi ya wawili walisema kwamba kuweka chupi yako katika chai yake ni jambo litaloshughulikia  tatizo hilo kwani atakupenda hata bila yeye mwenyewe kujua. Kama inavyofanyika kuhusu masuala ya mapenzi, wanawake hawaogopi kujaribu hata vitu vya kutisha ili mradi tu wawe na uhakika kwamba watazidi kupendwa na mmoja  waliye naye katika uhusiano. Hapo ndipo Irene alishawishika kujaribu kufanya hivo na siku yake ya 40 ikawadia .

Mzaha wa kukalia mtu chapati umekuwepo kwa muda mrefu lakini wasichojua wengi ni kwamba ni kweli kuna wanawake ambao huvua nguo na kuikalia chapati wanapopika, yote kwa minajili ya kuwateka waume zao kimapenzi na sio mzaha tena. Mengi pia hufanyika na uchunguzi katika makundi haya  ya akina dada pia yatakupa taswira ya kuogofya kuhusu wanayofanya baadhi ya wanawake ili kupendwa zaidi na wanaume .

Irene aliendelea kuzichukua chupi zake akizikamulia ndani ya chai ya Sam, na kamwe mwenzake hakujua ila sasa yake masaibu yalianza  siku  ambayo  alisahau kuiotoa chupi yake katika birika iliyokuwa na chai aliomwekea Sam pale mezani. Sam alipojaribu kujitilia kwenye kikombe, basi pakawa  na tatizo kwa sababu chupi ile iliziba  tundu la kutoa chai kwenye birika na ndiposa akaamua kuifungua na kisha …Kaboom! Sam alishanga kuona kama nguo ya ndani ya Irene katika birika la chai. Mwanzo hata alifikiri ni kichungi kimeharibikia ndani na alipoitoa, ilikuwa bayana kwamba ile ilikuwa chupi na hakuna jinsi mpenzi wake angejitetea  kwa sababu jikoni na chumba  viko mbali sana .

Irene alifika kwa wakati  ufaao kwa sababu pindi tu  Sam alipoinua ile chupi akiitoa kwenye birika, yeye  alikuwa akitoka dukani kuleta mkate na  mshtuko wake ulimsaliti kwani alionekana kuduwaa kwa sekunde kadhaa kabla ya kusema lolote. Jaribio lake la kujaribu kujitetea halikusikizwa kwa sababu sam alitoka nje na kuimwaga ile chai na kwenda kazini .

Ujumbe wa  kumtaka aondoke kwake aliutuma Sam akiwa kazini na maskini Irene hakuwa na budi ila kusalimu amri kwamba  juhudi zake za kutaka kupendwa zaidi kwa kutumia njia za mkato zilikuwa zimegonga mwamba .   Kando na masaibu ya Irene pia kuna mengine makubwa haya ya kuweka vitu vya ajabu ajabu katika chakula cha wanaume , kidudu mtu kanidokezea  siku fulani kwamba kuna wanawake wanaoweka damu ya hedhi yao katika vyakula vya wanaume kwa imani kwamba hatua hiyo itawafanya wapendwe zaidi .

Ni vitu  vipi vingine umewahi kusikia vinavyofanywa na watu kwa lengo la kutaka kupendwa zaidi?