Masaibu ya Valentin'es

Jinsi siku ya wapendanao ilivyogeuka kuwa ya ‘Wachukianao’-Nilimpata kwa mpenzi wa pembeni

Aliamua kujilegeza na akasema -‘Pole wrong house…’.

Muhtasari
  • Aliamua wakati wa chakula cha mchana kupiga safari yaharaka kwenda katika nyumba ya mpenziwe Brenda ili kuhakikisha kweli iwapo alikuwa amekwenda kazini .
  • Macho yake  hayakumpa fursa ya kuamini alichoona na akashindwa kati ya kubisha mlango na kuingia au kwenda zake .

 

Siku ya Valentine  huwa ya wapendanao kudhihirisha penzi lao kwa kila mmoja lakini kwa Alex ,siku hiyo wiki iliyopita ilikuwa mabaya sana katika maisha na uhusiano wake na mpenzi wake wa miaka mitatu Brenda . Bila kujua Brenda alikuwa na uhusiano wa pembeni na mwanamme mwingine ,Alex alikuwa amepanga kumshtukiza mwenzake wa zawadi kem kem na pia kumpeleka   katika mkahawa mzuri wa kifahari ili waweze kusherehekea penzi lao lakini ole wake! Siku hiyo ,ijumaa tarehe 14 ,ilianza kama siku nyingine …alienda kazini na hata walizungumza kuhusu mipango yao baadaye usiku huo . Lakini Alex anasema walipokuwa wanazungumza kwenye simu , alipata hisia Fulani isio ya kawaida kwamba huenda Brenda hakuwa kazini na alionekana kana kwamba alikuwa yungali katika nyumba yake mtaa tofauti na alikoishi Alex .

Licha ya kuagana naye kwenye simu   kwamba baadaye watakutana katikati mwa jiji kwa mipango yao ya valentine ,Alex hakutulia na hata akamwambia mwenzake kazini kwamba anahisi ni kwamba Brenda hajamwambia ukweli kwamba yuko kazini . Kuna watu ambao wana bahati kwa njia ya kuweza kupata daalili au ishara kwamba  mambo hayapo shwari na Alex nafikiri ana  bahati ya kuwa na uwezo kama huo unaompa ishara wakati kuna tatizo .

Aliamua wakati wa chakula cha mchana kupiga safari yaharaka kwenda katika nyumba ya mpenziwe Brenda ili kuhakikisha kweli iwapo alikuwa amekwenda kazini . Maskini jamaa alipofika katikamtaa wa Buruburu anakoishi Brenda alipata mlango wake upo wazi na pazia zimeinuliwa kuonyesha kwamba kuna mtu alikuwa chumbani . Alisogea karibu ili kuchunguza aliyekuwa ndani na  bila kutarajia  alichungulia dirishani na hakuamini macho yake kwa sababu mpenzi wake Brnda alikuwa chumbani ,sebuleni na alikuwa amemkalaia  mwanamme mwingine akimlisha pizza . Kando yao kwneye kiti kulikuwa    shada kubwa la maua yaliyotundukwa kwenye kifaa maalum ha kubebea maua .  Juu kwenye dari kulikuwa na mapambo a baluni zilizopulizwa hewa na kuwekwa ukutani jambo linaloashiriwa kwamba palikuwa na kitu kama sheehe au karamu . Macho yake  hayakumpa fursa ya kuamini alichoona na akashindwa kati ya kubisha mlango na kuingia au kwenda zake .

Alex alijawa na hamaki asijue iwapo amehadaiwa kimapenzi au kuna jambo ambalo hakulielewa lakini  uchu wake wa kutaka kujua ukweli ukamzidi fikra na akajipata amebisha mlango . Aliyefungua  ni yule mtu dume ,  jamaa bonge mwenye miraba mine ambaye alionekana kuwa mtu mzima aliyekomaa na hata kwa kumuangalia tu ungejua ni mume wa mtu na familia yake .Lakini anafanya nini kifua wazi katika nyumba ya Brenda? Maswali haya yalimjia katika sekunde chache kabla ya mazungumzo kuanza kati ya Alex na   mwizi wa mapenzi aliyekuwa amesimama mlangoni ,akimtenganisha yeye na mpenzi wake Brenda.  Jamaa alikuwa  amejiamini sana hadi hakungoja Alex amsalimie bali ndiye aliyefoka swali kwa Alex-  ‘Sema kijana ,unataka nini?’ Alex alishangaa kuulizwa hivi katika nyumba  ambayo  amewahi kuja mara nyingi na hata kulala huko ? kwa  sekunde kadhaa  hata alijipata na woga kwani alijimbia kwamba anavyojiamini jamaa huyu labda ndiye mabaye amekuwa akimlipia kodi Brenda!

Aliamua kujilegeza na akasema -‘Pole wrong house…’. Aliendelea kutembea ni kana kwamba alikuwa akiitafuta nyumba nyingine . Alex  hakuamini alichoona na wakati akiendelea kuondoka ,akamsikia Brenda akicheka kwa sauti . Alihakikisha kwamba aliyekuwa mle ndani ni  mpenzi wake na kwa hamaki aliifuta nambari yake ya simu na akaapa kamwe kutozungumza naye .Usaliti huo umemshtusha Alex  na haamini hadi sasa kwamba Siku iliyofaa kuwa yake kudhihirisha penzi kwa Brenda  ilitumbukia kuwa siku aliogundua yote kumhusu msichana aliyefiriki angekuwa mke wake na mama ya watoto wake.