Baada ya kula tunda wanakwepa

Hit&Run: Wanaume hunitumia na kukwepa

Mwanamke ,yadaiwa anafaa kuwa na uwezo wa kujua daalili za mwanamme ambaye lengo lake ni dona dona za hapa na pale na kisha kutoroka

Muhtasari
  • Sio mara moja bali kwa sasa ameachwa na wanaume 7 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita .
  • Inawezekana ukawana mtu mzuri lakini kwa bahati mbaya watu wanaokuja katika maisha yako sio watu wanaokufaa .

 

 

Kila   mwanzo wa uhusiano hubeba matumaini  kwamba uhusiao huo utadumu kwa muda mrefu na hata ikiwezekana kuishia katika ndoa . Angalau hivyo ndivyo alivyoamini na kutarajia Jessica Kinja wakati alipoanza kupendana na mpenzi wake wa kwanza Samuel miaka kadhaa iliyopita .

 Lakini kwake  ,safari ya mapenzi imekuwa ya kuvunja moyo na kuwaacha hoi kwani wanaume wote ambao huja katika maisha yake ,hawadumu kwani baada ya mazoea ya muda na daalili za kuaminiana ,wao hukwepa na kumuacha pweke .Sio mara moja bali kwa sasa ameachwa na wanaume 7 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita .

 Jessica ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32 anasema yalikuwa matamanio yake sana kuwa katika ndoa baada ya kumaliza masomo na kupata kazi lakini haelewi mbona imekuwa vigumu kwake kukaa katika uhusiano wa kudumu au muda mrefu na mwanamme yeyote anayekuja katika maisha yake . Amesema hakuna kibaya ama cha kutisha  ambacho kinafaa kutajwa kama sababu ya kuachwa . Rafiki zake wengi wameshaolewa na hata wengi wao hushangaa kinachomfanyikia .

Jessica  anasema  anashuku kwamba tabia yake ya kupenda Zaidi na moyo wote ndio hufanya wanaume  kumtenda . Kingine anachojutia ni kwamba wanapoanza kupanga kuhusu siku za usoni na maisha ya ndoa ,wanaume wengi huanza kupunguza kasi ya uhusiano wao . Hajaweza kuelewa mbona hatima hii ndio humpata na ametfuta msaada wa  mshauri .

 Mshauri na hata  baadhi ya rafiki zake wamemuambia Jessica kwamba huenda yeye huwapenda wanaume wasiofaa . Inawezekana ukawana mtu mzuri lakini kwa bahati mbaya watu wanaokuja katika maisha yako sio watu wanaokufaa .

 Jessica anasema mtu aliyemvunja moyo sana na kumkosesha usingizi hadi sasa ni  mwanamme mmoja aliyekuw  mwalimu kama yeye ambaye baada ya uhusiano wa miaka miwili na nusu walitarajiwa kufunga ndoa ,lakini kwa ghafla bila sababu za kutosha ,jamaa aliamua kutafuta uhamisho kwenda shule nyingine na kukatiza uhusiano wao . Hajaweza kuelewa kilichofanyika kwani tangia hapo amekuwa akiingia katika uhusiano mmoja hadi mwingine bila kuishia katika lolote la kudumu ama lenye matumaini ya kumalizikia katika ndoa .

 Mwanamke ,yadaiwa anafaa kuwa na  uwezo wa kujua daalili za mwanamme ambaye lengo lake ni dona dona za hapa na pale na kisha kutoroka .Mshauri wa uhusiano Geoff Kimore anasema ni bora kwa mwanamke yeyote kuwa na ujasiri wa kumuuluiza mwanamme anayetaka uhusiano naye kuhusu  nia yake  katika uhusiano ili  kuweza kujua watu wanaolenga kumpotezea muda .