Wanachotakiwa kufanya wamiliki wa shahada ili kupigana na ndoto mbaya za ajira

Muhtasari
  • Wanachotakiwa kufanya wamiliki wa shahada ili kupigana na ndoto mbaya za ajira
Graduation
Graduation

Tumewaona wengi wakizunguka hap na pale wakitafuta kazi licha yao kuwa na shahda kwenye mfuko.

Kauli iliingia nchini kuwa kenya hamna kazi, kwa hivyo kila mtu anapaswa kuishi awezavyo.

Baadhi ya watu ambao wamemiliki shahada walianzisha bishara ili kupigana na ndoto mbaya ya ajira.

 

Kuna pia wale wanategemea tu shahada yao iweze kuwapa kazi, kwa maana hawana namna nyingine yeyote.

Siku chache muigizaji Omosh alijitokeza na kueleza shida ambazo amekuwa akipitia licha ya yake kuwa na shahada ya uhasibu.

Lakini swali kuu ni je wanapaswa kufanya nini ili kupigana na ndoto hii?

Hizi hapa baadhi ya mambo ambayo wanapaswa kufanya;

1.Wakuje pamoja na kuanzisha kampuni

Licha ya wao kuwa na shahda kuna wale wamebarikiwa na kipaji cha kuanzisha  biashara au kampuni na kisha inafaulu na wanajiariri.

2.Wajifunze ujuzi tofauti

 

Hapaswi kutegemea tu shahda zao kwa maana sisi sote hatuwezi toshea mahali pamoja, ndio unaweza kuwa na shahada lakini ujifunze kuuza matunda na hata kutengeneza sabuni na kadhalika.

3.Watilie maanani kazi ambazo zinahitaji watu wengi

Lazima upate riziki yako ya kila siku, na kuendeleza maisha yako, kama kazi ambayo inahitaji watu ni ya kufagia katika kampuni haya basi jiunge na uanze.

Weka shahda yako kando na uchape kazi mwishowe utafaulu maishani mwako.

4.Watafute kazi kwenye mitando ya kijamii

Ndio kuna wale watasema kuwa kazi hizo si nzuri na nizawalaghai lakini kwa hakika kama utapata moja anza kutengeneza maisha yako na kazi hiyo.