Orodha ya filamu ambazo zimevuma kwenye runinga za wakenya

Muhtasari
  • Orodha ya filamu ambazo zimevuma kwenye runinga za wakenya
  • Bali na kuwa na filamu na vipindi nyingi kwenye runinga zetu, kuna zile ambazo zimependwa zaidi kuliko vingine

Vipindi vimekuja na kupendwa na wenye kupenda kutazama filamu mbalimbali, sio filamu zote ambazo hupeperushwa katika runinga na kupendwa na watazamaji.

Bali na kuwa na filamu na vipindi nyingi kwenye runinga zetu, kuna zile ambazo zimependwa zaidi kuliko vingine.

Kila kipindi kina masaa na wakati wake, wakati huo utawapata watazamaji wakiwa makini sana kwenye runinga zao.

 

Kuna baadhi ya filamu ambazo zimevvuma sana kwenye runinga za wakenya na zimependwa sana.

Hii hapa orodha ya baadhi ya filamu hizo;

1.Pete

Ni kipindi ambacho hupeperushwa katika uninga ya Maisha Magic East, ni kipindi ambacho huzungumzia uongozi kati na ndugu wawili, ambao wanapigania pete ya uongozi iliyoachwa na baba yao baada ya kuaga dunia.

2.Maria

Ni kipindi ambacho hupeperushwa katika runinga ya Citizen, huwa kinazungumzia maisha ya utajiri na maisha ya Ghetto, na jinsi ya kunyakua utajiri.

3.Selina

 

Selina kimependwa sana na watazamaji wa runinga ya Maisha magic East, huwa kinazungumzia wapenzi wawili ambao wanapigana na changamoto zote zinazowakumba ili waweze kunawiri mapenzi yao.

4.Anda Kava

Kipindi hiki kimekuwa kikipeperushwa na Maisha Magic East, waigizaji wakuu ni Abel Mutua na mchekeshai Njugush.

Huwa wanaigiza kama wapelelezi wa uhalifu.

Kati ya vipindi hivi unapenda kipi zaidi?