Ishara zinazoonyesha mwanamke hayuko tayari kukupoteza katika uhusiano

Muhtasari

Ishara zinazoonyesha mwanamke hayuko tayari kukupoteza katika uhusiano

Pia kuna wale ambao hupenda watu wasiofaha na mwishowe kuumizwa mioyo yao.

Upendo ni mzuri wakati umempenda mtu ambaye anafaa na anakuheshimu na kukuthamini, pia kila mtu hutamani kupendwa licha ya changamoto ambazo wamepitia.

Pia kuna wale ambao hupenda watu wasiofaha na mwishowe kuumizwa mioyo yao.

Kuna baadhi ya ishara ambazo wanawake huonyesha na kuthibitisha kwaba hayuko tayari kukuachwa, hata changamoto ziwe nyingi aje.

 

Kuna wale watakupenda ukia na pesa ukiishiwa haya basi anajiondoa mbio mbio bila ya kutambua jinsi utasikia wa utahisi.

Hizi hapa baadhi ya ishara zinazoonyesha na kuthibitisha kwamba mwanamke hayuko tayari kukupoteza au kukuacha.

1.Hatachoka kukutumikia

Kukutumikia yaani yuko tayari kufanya chochote au lolote ili uwe na furaha, hatachoka kufkufanyia kazi katika nyumba yako.

2.Huwa amekukasirikia kila wakati

Kwanini kama mwanamke anakupenda ukweli hatafurahi kukuona ukiwa na wanawake wengine, kinacho mjia kwenye akili yake ni kwamba unataka kumtema.

Pia hatafurahi kwamba unatangamana na wao anataka tu kuwa nawe kila wakati.

 

3.Yuko tayari kuwa nawe wakati wowote

Maisha yana milima na mabonde kama mwanamke anakupenda atatumia wakati wake kuwa nawe wakati wowote kama unapitia changamoto au kama una furaha.

4.Anataka kukutambulisha kwa marafiki zake kila wakati

Hii ni ishara kwamba hakuchezi na mwanaume mwingine yeyote bali amekutambua tu wewe pekee.