Njia bora za kukabiliana na wimbi la tatu la virusi vya corona

Muhtasari
  • Njia bora za kukabiliana na wimbi la tatu la virusi vya corona
  • 'Uzoefu' huu wa janga hufanya iwe rahisi kukabiliana na mabadiliko, kama kufungwa tena kwa shule na biashara. Kwa hivyo, labda unayo mpango tayari

Habari za wimbi la tatu la corona ni jambo ambalo wakenya wengi hawangetaka kusikia wala kutarajia,Hasa baada ya mwaka mzima wa vizuizi na masharti , na kanuni za wizara ya afya ili kuthibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Tishio la anuwai ya kuambukiza ya corona tayari imechangia kuongezeka kwa visa katika kaunti nyingi.

Wakati wa habari za janga la corona wengi wa wananchi walipatwa na mshangao tunajua vizuri zaidi nini cha kutarajia kufikia sasa.

'Uzoefu' huu wa janga hufanya iwe rahisi kukabiliana na mabadiliko, kama kufungwa tena kwa shule na biashara. Kwa hivyo, labda unayo mpango tayari.

Kuna baadhi ya njia mwafaka ambazo kila mmoja anapaswa kufuata na kuzingatia ili kukabiliana na janga jili.

Njia hizo ni kama vile zifuatavyo;

1.Kujikinga

Kama wataka kutoboa katika wimbi la tatu la msambao wa maambukizi ya corona lazima ufuate kanuni za wizara ya afya ili kujikinga na tusisahau kuvallia baroka na kunawa mikono.

2.Bajeti

Kama bajeti yako ilikuwa ya gharama ya juu zaidi unapaswa kupunguza bajeti yako na uwekeze pesa zako, kumbuka kampuni ambayo umeandikwa sio ya amam au baba yako, lakini wengi usahau hayo na kucheza na kazi yao.

3.Panga kula chakula ambacho kina afya

Ndio wakati huu wananchi wengi wanakabiliana na wakati mgumu katika maisha yao, lakini wanapaswa  kutafuta chakula ambacho kinaongeza afya mwilini ili uwe na nguvu, ya kukabiliana na janga la corona.

4.Tafuta mashauri

Endapo umepatwa na msongo wa mawazo ni heri umkimbilie daktari ili akushauri usije kufanya jambo au mambo ambayo utajuta baadaye au familia yako itajuta