Soma jinsi wanafunzi wanapaswa kutumia pesa zao za HELB ili kujiepusha na msoto

Muhtasari
  • Mkopo wa HELB ni moja wapo ya mikopo ambayo wanafunzi wa chuo kikuu hupokea kila muhula ili waweze kujikimu endapo wamo shuleni
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Moi waandamana siku ya Jumatano wakitaka mikopo kutoka HELB
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Moi waandamana siku ya Jumatano wakitaka mikopo kutoka HELB
Image: MATHEWS NDANYI

Mkopo wa HELB ni moja wapo ya mikopo ambayo wanafunzi wa chuo kikuu hupokea kila muhula ili waweze kujikimu endapo wamo shuleni.

Kwa muda sasa wanafunzi wamechukulia mikopo hiyo kwa urahisi mwingi huku asilimia kubwa ikitumia pesa hizo kwa njia isiyo faha.

Huku kama umepokea pesa za HELB ni lazima kila mwanafunzi aregeshe pesa hizo  baada ya kuhitimu masomo yake awe na kazi au asiwe na kazi.

 

Tatizo liko pale ambapo wanafunzi wakipokea pesa hizo wanajivinjari,kununua nguo au vitu vya bei ya juu huku wengine wakiwfurahisha wanawake na pesa hizo, bila ya ujua kwamba baada ya kutoka katika chuo kikuu atalipia pesa hizo akiwa pekeyake.

Wiki chache zilizopita tulishuhudia wanafunzi wakiwa wanaandamana kwa ajili ya pesa za HELB huku wakilalamikia maisha duni.

Lakini swali ambalo wengi hawakujiuliza ingekuwa wanafunzi hao wameshikana na kuunda kikundi na kufungua biashara wangeharibu wakati wao wakiwa wanaandamana, na kutosoma?

Lakini kama hutaki kujuta baadaye hizi hapa njia ambazo unapaswa kutumia pesa za HELB ili kujiepusha na msoto.

1.Fungua Biashara

Sio lazima uwe na milioni ya pesa ili ufungue biashara, nina hakika wanafunzi wa chuo kikuu hutumia zaidi ya elfu kumi kujivinjari, chukua elfu tano anza biashara ata kama ni ya kuuza mitumba.

Biashara yako itanawiri kila siku kuenda nyingine ukiwa makini nayo.

 

2.Mwanablogu

Kama una talanata ya kuandika unaeza anzisha kazi na mwanablogu kisha utapata pesa na hautategemea pesa za helb sana.

3.Bajeti

Kama wataka kufanikiwa maishani ishi maisha ya chini, huku ukiwekeza pesa zako kwa maana huwezi jua ya kesho yatakuwa vipi.

4.Marafiki

Jiepushe na marafiki ambao hawana mwelekeo au wanakutambua wakati umepokea pesa zako za HELB,hao sio marafiki ambao wanakutakia mazuri bali wanataka kuanguka kwako.

5.Wekeza

Ukiwekeza kwa miaka nne, utapata pesa nzuri za kuanzisha biashara au kufanya jambo ambalo litakuletea pesa kila mwisho wa mwezi.

Natumai umepata jambo moja au nyingine kutoka kwa makala haya na jinsi unapaswa kutumia pesa za HELB.

Wanafunzi wanapswa kukumbuka kwamba kuna maisha ya kesho, bali wengi hutilia maanani maisha tu ya leo.