Ishara kwamba uko tayari kuwa kwenye uhusiano baada ya kuwa 'single' kwa muda mrefu

Muhtasari
  • Kuna baadhi ya watu ambao huchukua likizo baada ya kutoka uhusiano mmoja hadi mwingine
  • Kuna wale uamua kukaa bila mpenzi kwa miaka, na kuazoe maisha ya kukaa 'single'

Kuna baadhi ya watu ambao huchukua likizo baada ya kutoka uhusiano mmoja hadi mwingine.

Kuna wale uamua kukaa bila mpenzi kwa miaka, na kuazoe maisha ya kukaa 'single'.

Lakini wafahamu huwezi kaa bila mpenzi miaka yote? kuna ishara ambazo huonyesha kwamba yuko tayari kuwa katika uhusiano baada ya kukaa 'single' kwa muda mrefu.

Kuna wale huwa wanaamua kukaa single baada ya kuumizwa moyo, na wengi hutaka nafasi yaoya maisha.

Ishara hizo ni zipi, ishara hizo ni kama vile zifuatavyo;

1.Umeendelea na maisha na uko tayari

Baada ya kuumizwa moyo kuna wale uamua kuendelea na maisha na wale uamua kwamba hawawezi kuishi bila mpenzi wao.

Kama uliamua kukaa 'single' kwa ajili umeumizwa roho haya basi kama umeendelea na maisha yako na kumsahau mpenzi wako wa awali fahamu ya kwamba upo tayari kuingia katika uhusiano mwingine.

2.Unajijua na kujifahamu vyema

Kuna baadhi ya watu ambao huingia katika uusiano wa kimapenzi bila ya kujijua na kufahamu haswa wanataka nini katika uhusiano huo.

Lakini endapo umekaa 'single' kwa muda mrefu na unajifahamu na unajua kile wataka maishani mwako haya basi jua uko tayari kuwa katika uhusiano wa kimapenzi.

3.Ukipatana na mtu ambaye anaonekana kama mpango halisi

uan wale watakuongelesha tu kwa maana wamehisi wanataka kukuongelesha,lakini kuna wale watakuongelesha na uhisi kweli huo ni upendo wa kweli na mapenzi yananoga kweli kweli.