Ujuzi kila mtoto anapaswa kujifunza ili kuwa mtu mzima anayewajibika

Muhtasari
  • Watu wanapokuwa watu wazima, wengi wao hutambua kuna ujuzi fulani ambao wanakosa na wanatamani wazazi wao wangewafundisha wakati walikuwa wadogo.
  • Kwa wengine, ni mambo kama uhuru na kujiamini. Wengine hutamani kujua zaidi juu ya kupanga na kujenga kazi yao
WhatsAppImage2017-05-15at10.13.35
WhatsAppImage2017-05-15at10.13.35

Watu wanapokuwa watu wazima, wengi wao hutambua kuna ujuzi fulani ambao wanakosa na wanatamani wazazi wao wangewafundisha wakati walikuwa wadogo.

Kwa wengine, ni mambo kama uhuru na kujiamini. Wengine hutamani kujua zaidi juu ya kupanga na kujenga kazi yao.

Na kuna mambo mengine ambayo yangesaidia watoto kujua ambayo yangewaandaa kwa siku zijazo.

 

Pia ni matamanio ya kila mzazi kuona watoto wake wanawajibika katika maisha yao, lakini ni ujuzi upi wanapaswa kutumia wakiwa watoto?

Hii hapa ya orodha kila mtoto anapaswa kijifunza;

1.Jinsi ya kujitetea

Sio watu wazima tu wanahitaji kujitetea pia watoto wanahitaji kujitetea endapo wamekosana na marafiki zao.

Na kujilinda haifai hata kuwa kwa mwili. Watoto wanaweza kutumia maneno kuzidisha mzozo, kwa hivyo sio lazima wapigane

Ni muhimu kumfundisha mtoto wako kuwa mwenye uthubutu wa maneno, na asimpe mnyanyasaji majibu ya kihemko waliyokuwa wakitarajia, au aondoke tu

2.Jinsi ya kupika

 

Karne hii ya sasa watoto wengi wanajua tu starehe za kutazama televisheni na kutumia tu simu na wala hawajui kupika ata chai.

Wanapaswa kujua jinsi ya kupika ili wakiwa wakubwa wawajibike.

3.Jinsi ya kutumia muda wao

Wazazi wanapaswa kuwafunza watoto wao jinsi muda ni muhimu katika maisha yao kwani wakiwa wazima watahitaji muda wao na kama hawajui kuutumia vyema hawatajibika maishani mwao.

4.Jinsi ya kutumia pesa

Watoto wanapaswa kujifunza jinsi ya kutumia pesa kwa maana wakiwa wakubwwa pia wanahitahi pesa katika maisha yao na wanapaswa kufahamu jinsi ya kuzitumia.

5.JInsi ya kufanya maamuzi

Ukijua kufanya uamuzi maishani mwako kwa hakika mtoto akiwa mtu mzima pia atajua kuamua uamuzi wake na wala sio kufuata kile wenzake wanamuambia na kumpotosha.

6,Jinsi ya kukaa na wenzake

KUna baadhi ya watoto hawapendwi na wenzao kwa sababu ya kuzua vurugu kila waendapo, mfunze mtoto wako jinsi ya kuishi na wenzake na akikua mtu mzima hutajuta kwa maana atajua kuwajibika.

Zaidi ya yote wazazi wanapaswa kuwafunza watoto kuwa na nidhamu na heshima katika maisha yao, kwani biblia inasema kwamba funza mtoto njia atakayo fuata na akiwa mzee hataishahau.