Orodha ya watu waliotoweka na kupatikana wakiwa wameuawa tangu Januari 2021

Muhtasari
  • Orodha ya watu waliotoweka, na kupatikana wakiwa wameuawa
  • Lakini matumaini yao yalizimwa kila kuchao, kwani kuna wale waliwapoteza wapendwa wao kwa njia moja au nyingine
Marehemu Jennifer Wambua
Marehemu Jennifer Wambua
Image: HISANI

KItendawili huwa kinazidi kuwa kigumu sana wakati, familia inapompoteza mmoja wa wapendwa wao bila ya kuwapata.

Watu wengi walitarajia mwaka wa 2021 utakuwa mwaka mwema, baada ya watu wengi kupoteza maisha yao kutokana na janga la corona mwaka wa 2020.

Lakini matumaini yao yalizimwa kila kuchao, kwani kuna wale waliwapoteza wapendwa wao kwa njia moja au nyingine.

Visa vya watu kutokewa nchini vimezidi kuongeza kila kuchao, bila ya kujua waendako, wote ambao wametoweka wamepatikana au walipatikana wakiwa wameauwa, bila ya wengi kujua sababu ya vifo vyao.

Wengi wameachwa wakiomboleza na kutafuta haki kwa wapendwa wao, lakini je watapata ukweli na haki ya wapendwa wao?

Hii hapa orodha ya watu waliotoweka na kupatikana wakiwa wameaga dunia tangu Januari mwaka wa 2021;

1.Mohammed Bashir Mohamoud

Mwili wa mwanabiashara huyo ulipatikana katika mtto Nyamindi mei 16 baada ya kuripotiwa kutoweka siku tatu.

Gari lake lilichomwa, huku mabaki ya gari hilo yakitoweka katika eneo la tukio, huku maswali chungu nzima yakibaki akilini mwa jamaa na marafiki zake, je nani alimtaka Bashir afe?

2.Jennifer Wambua

Mwili wa afsa huyo wa NLC ulipataikana Machi 15 baada ya kutoweka kwa siku chache.

Jenipher Wambua ambaye alikuwa naibu mkurugenzi wa mawasiliano wa tume ya ardhi alikuwa hajaonekana tangu siku ya Ijumaa, na ripoti ya mtu aliyepotea tayari ilikuwa imewasilishwa na bwanake katika kituo cha polisi cha Capitol Hill, Nairobi.

Pia kitendawili cha mauaji yake kilisalia kuwa kigumu zaidi, je nani alitaka Jennifer afe?

3.Elijah Oboung (35), Benjamin Imbai (30), Brian Oduar(36) na Jack Anyango Otieno(39) 

Wanne hao walitoweka Aprili 19 wakiwa katika klabu moja mtaa wa Kitengela, miili ya wanne hao ilipatikana katika maeneo tofauti, huku maswali, ya jamaa zao yakikosa kujibiwa.

Je fumbo la mauaji hayo litatatuliwa, au jamaa za watu hao watazidi kutafuta majibu ya maswali yao.

Na je nani aliwataka wauawe, na kwanini wakatendewa unyama huo? ina maana watu wameacha kuwa na roho za ubinadamu