Mejja ajibu madai ya kuiba kibao kutoka kwa msanii chipukizi

Muhtasari
  • Mejja ajibu madai ya kuiba kibao kutoka kwa msanii chipukizi
Mejja
Image: Hisani

Msanii Mejja amejibu na kukana madai ya kushikamana na mzalishaji wake na kuiba kibao kutoka kwa msanii chipukizi wa humu nchini.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Mejja alionekana kusikitishwa na madai hayo huku akisema kwamba amekuwa akiwasaidia wasanii iweje aibe kibao.

"NiLiKuwa Mimea Zangu NaKuTaNa Na Hii UFala, YaaNi chuki ambacho ni cha kiwango kingine,mimi ni mtu yule yule ambaye anawasaidia wasanii chipukizi  Sasa Leo NiMeKuwa NaChuKuwa Doba Inaitwa DuNia, kama hii ni jinsi na njia  Yaku Ni weka chini Siwachi KUTOA NGOMA amini hayo  HADI NIFE Mungu juu ya yote," Alisema Mejja.

Revina, msanii chipukizi alisema madai hayo ili apokee msaada kutoka kwa mwanablogu Robert Alai.

Msanii huyo alisema kwamba Mejja aliiba kibao cha 'Tabia za watu wa Nairobi' ambacho Mejja alikitoa wiki iliyopita.