Hizi hapa sababu kwa nini baadhi ya wanawake hukula 'fare' ya wanaume

Muhtasari
  • Hizi hapa sababu kwanini baadhi ya wanawake hukula 'fare' ya wanaume
  • Kwa hivyo swali linabaki kuwa ni nani anayeweza kuwa sababu ya tabia kama hizo, ni mwanamume au mwanamke

Wanaume wengine wamekuwa kwenye mtego na  kuwa wahasiriwa wa kuwatumia wanawake nauli ili waende kuwatembelea au kumpeleka 'outing'.

Baada ya mwanamume huyo kutuma nauli anapewa Block kwenye mitandao ya kijamii, kisha mwanamke huyo anakosa kuenda vile walivyokuwa wamekubaliana.

Kwa hivyo swali linabaki kuwa ni nani anayeweza kuwa sababu ya tabia kama hizo, ni mwanamume au mwanamke

Hizi hapa baadhi ya sababu kwanini wanawake wengi hukula nauli ya wanaume na kutotimiza vile walikuwa wamekubaliana.

1.Kulipiza kisasi

Labda mwanamume huyo alimkosea mwanamke huyo, na kwa maana anataka kulipiza kisasi kwa yale alimtendea mwaamke huyo anaamua kula pesa zake kwa ujanja.

2.Hakupendi

Sio kila mwanamke anakuambia anakupenda unaamini, kuna yule anataka kula pesa zako na anakutoka kwa ujanja,na kwa sababu hataki kukuambia anakufanyia kitendo kama ya kula 'fare' ili umuache,

3.Kukufunza somo

Hata baada ya kuwatumia wanawake kadhaa nauli na kisha wanakula,unakuwa hujajifunza somo hata moja, kuna yule mwanamke utapatana naye akupe somo moja ambalo hutawahi sahau maishani.

4. Labda amesota

Vile walisema hii ni kanairo, na kama huna ujanja,utasota sio kila mwanamke ana kazi hii Nairobi kuna wale wataistisha mwanamume nauli, wakiahidi kuenda kuwatembelea lakini wakipokea pesa hizo  wanatimiza mahitaji yao.

Lakini wewe Olisikia wapi, mwanamke akitumiwa pesa akiwa na shida anakosa kuhitimiza atatimiza shida yake lakini hatakuja kukuona.

5.Anayetuma nauli hiyo anaweza kuwa hatari

Wakati mwingine baadhi ya wanaume wanaweza kuwa na wasiwasi sana wakati wamempenda mwanamke

 wanasisitiza katika kukutana nao.Kwa mwanamke anajua wewe ni hatari tu, atachukua faida ya hilo na kula 'fare'.

Je umekula 'fare ya mwanamume yeyote, au umewahi mtumia mwanake yeyote 'fare' na akakula?