Sababu unapaswa kuzingatia msamaha wakati mpenzi wako amekudanganya

Muhtasari
  • Sababu unapaswa kuzingatia msamaha wakati mpenzi wako amekudanganya
cheating
cheating

Asilimia kubwa ya wanandoa na wapenzi huachana baada ya mmoja wao kudanganya na kuenda nje ya uhusiano wao.

Lakini kuna wale baadaye huomba msamaha baada ya kugundua makosa yao, sio wote ambao husamehewa na kisha kutemana kwa ajili ya kosa hilo.

Je unaweza msamehe mpenzi wako baada ya kuenda nje ya uhusiano wenu? kama jibu lako  ni la, hizi hapa sababu unapaswa kuzingatia msamaha baada ya mpenzi wako kukudanganya.

1.Ni jambo la wakati mmoja

Kuna sababu ambayo mpenzi wako alitoka nje ya uhusiano wenu, sababu hiyo inaweza kuwa wewe au jambo lingine, lakini endapo ni jambo ambalo ametenda mara moja na amegundua makosa yake na kukuomba msamaha, haya basi kwanini usimsamhe/

2.Je anafaa kusamehewa

KUna baadhi ya watu ambao wamezoea kuchanganya damu kila mara endapo wamo katika uhusiano wa kimapenzi na kutotosheka na mwanamke au mwanamume mmoja lakini sababu ya kutenda hayo ni ipi?

Ni jambo ambalo amejizoesha kufanya, lakini endapo amekubali makosa yake na kuomba msamha je unaweza okoa uhusiano wenu na kumsamehe labda ata badilika kwa ajili ya msamaha wako.

3.Majuto ya kweli

Labda baada ya kutekelza kitendo hicho mwenzi wako ana majuto ya kweli kwa hivyo unapaswa kuzngatia msamaha wake.