Hizi hapa sababu kwa nini unahitaji kuweka uhusiano wako faragha

Muhtasari
  • Hizi hapa sababu kwanini unahitaji kuweka uhusiano wako faragha
  • Baadhi ya watu mashuhuri wameeka ndoa, na uhusiano wao wa kimapenzi kwenye umma ilhali kuna wale uhusiano wao wameuweka  faragha

Je unapenda uhusiano wako wa kimapenzi ukiwa kwenye faragha au ukiwa kwenye umma, kile chote mnafanya marafiki zako wanafahamu.

Baadhi ya watu mashuhuri wameeka ndoa, na uhusiano wao wa kimapenzi kwenye umma ilhali kuna wale uhusiano wao wameuweka  faragha.

Kuna sababu chache ambazo unahitaji kufahamu kwanini unapswa kuweka uhusiano wako faragha

Sababu hizo ni kama vile zifuatavyo;

1.Inaweka kando ushauri mbaya

Kama uhusiano wako uko kwenye faragha haya basi hutapata ushauri mbaya kutoka kwamarafiki na wanamitandao.

2. Shinikizo kutoka pande zote

Hutapata shinikizo nyingi kutoka kwa marafiki, jamaa zako au mitandaoni kwani unafahamu na kujua kile unaendelea katika uhusiano wako.

Hapo hamtakosana na mpenzi wako sana wa ajili ya shinikizo kutoka kila mahali.

3.Inaimarisha kifungo katika uhusiano wako

Ukiweka uhusiano wako kwa faragha mapenzi kati yenu yanaendelea kunoga kila kuchao, kwa maana hamna anayejua wala kuingilia mapenzi yenu.

Ndio najua wengi wanauliza kwanini waweke uhusiano wao  faragha, kwani hamna mtu ambaye anapenda kufichwa kama ARV's, lakini mwishowe utafahamu kwamba ni vyema uhusiano wako wa kimapenzi uwe kwa faragha.