Mume wangu aliniacha baada ya kugundua nina virusi vya ukimwi-Mwanamke alia

Muhtasari
  • Sio matamanio ya mtu yeyote kuwa mgonjwa au kutaka kupitia changamoto ngumu maishani mwake
  • Kuna baadhi ya wale hupambana na changamoto hizo na hata kuwa washind
  • Mwanamke mmoja alimsimulia mtangazaji Massawe jinsi aliambukizwa virusi vya ukimwi na aliyekuwa mumewe
sad woman
sad woman

Sio matamanio ya mtu yeyote kuwa mgonjwa au kutaka kupitia changamoto ngumu maishani mwake.

Kuna baadhi ya wale hupambana na changamoto hizo na hata kuwa washindi.

Lakini kuambukizwa virusi ambavyo utaishi navyo maishani mwako ni jambo la uchungu na la kuhuzunisha.

Mwanamke mmoja alimsimulia mtangazaji Massawe jinsi aliambukizwa virusi vya ukimwi na aliyekuwa mumewe.

"Nilikuwa kwenye ndoa ambapo nilitoka, sababu ya kutoka ni kuwa aliyekuwa mume wangu aliniambukiza ukimwi bila yangu ya kujua

Baada ya kutoka kwenye ndoa niliolewa tena, lakini baada ya mwanamume huyo kujua nina virusi vya ukimwi alinitoroka

Nimekuwa nikiishi na virusi hivyo kutoka mwaka wa 2009, katika ndoa yangu ya kwanza nilikuwa nimebarikiwa na watoto wawili, na ndio baba yao anawashughulikia vizuri siwezi nika lalamika

Katika ndoa ya pili, nilibarikiwa na mtoto mmoja, na baada ya mume wangu kunitoroka hajakuwa akimsaida mtoto wake,nikimpigia simu amekuwa akiwapea wanawake waniongeleshe," Alisimulia mwanamke huyo.

Kwa kweli wagonjwa kama hao wanapaswa kupokea upendo kutoka kwa jamaa zao, lakini asilimia kubwa hupokea kejeli nyingi na kukatalia na jamaa wao.