BILIONEA CHRIS KIRUBI

Orodha ya kampuni kubwa alizomiliki na kuongoza bilionea Chris Kirubi

Mwaka wa 2017, Kampuni ya Centum iliweza kuzindua jengo kubwa la maduka la Two Rivers kando na barabara ya Limuru baada ya kununua shamba la ekari 100 maeneo hayo.

Muhtasari

•Kirubi aliwashangaza wengi baada ya kujitangaza kuwa mmoja wa wacheza santuri katika stesheni  yake ya redio ya Capital FM na kujipa jina la usanii ‘DJ CK’

•Kirubi alimilikI zaidi ya kampuni 10 kubwa.

Chris-Kirubi
Chris-Kirubi

Kifo cha mwanabiashara mashuhuri nchini, Chris Kirubi, kilitangazwa na familia yake siku ya Jumatatu. 

Marehemu alikuwa anaugua maradhi ya saratani tangu mwaka wa 2017. Aliaga akiwa na umri wa miaka 80.

Kirubi alitambulikana kama mwanabiashara shupavu, kiongozi, mshauri na  mfano wa kuigwa na wengi. Alikuwa kati ya watu tajiri zaidi nchini Kenya na barani Afrika kwa ujumla.

Tunaangazia baadhi ya kampuni kubwa za kibiashara ambazo marehemu alimiliki na kuongoza kabla ya kifo chake. 

1. Centum

Kirubi ndiye alikuwa mwenye hisa nyingi katika kampuni ya uwekezaji ya CENTUM.

Kampuni ya Centum inadaiwa kuwa miongoni mwa kampuni zilizo na hisa nyingi zaidi kwenye soko la hisa la Nairobi Securities Exchange.

Mwaka wa 2017, Kampuni hiyo iliweza kuzindua jengo kubwa la maduka la Two Rivers kando na barabara ya Limuru baada ya kununua shamba la ekari 100 maeneo hayo.

Centum pia imekita mizizi yake nchini Uganda.

2. International House Limited

Kirubi alikuwa mkurugenzi mtendaji katika kampuni ya usimamizi wa mali ya International House Limited.

Kampuni hiyo ilianzishwa mwakani 1985 baada ya kununua jumba la International House kutoka kwa kampuni ya Canada.

 

3. Bayer East Africa LTD

Kirubi alikuwa naibu mwenyekiti katika kampuni ya Bayer East Africa Ltd.

Kampuni ya Bayer East Africa LTD inahusiana na utafiti na ubunifu wa Kisayansi kwenye nyanja za ukulima na afya.

Ina mizizi yake nchini Ujerumani.

Bayer East Africa ambayo ina makao yake makuu jijini Nairobi imeweza kupanuka hadi nchini Ethiopia, Tanzania, Uganda na Rwanda.

4. HACO Tiger Brands (EA) LTD

Kirubi ndiye mmiliki wa kampuni ya Haco Tiger Brands ambayo inahusiana na manguo, viatu, kalamu, vipondozi, vifaa vya stima, bidhaa za plastiki, kemikali na biashara zingine.

Bidhaa za kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mwaka wa 1974 zinauzwa hadi nje ya mipaka ya Kenya.

5. DHL Worldwide Express Ltd

Kirubi alimiliki kampuni ya usafirisha ya DHL Worldwide Ltd.

Kampuni hiyo inahusika na kusafirisha vitu kwa zaidi ya mataifa 220 ulimwenguni.

6. Capital Media Group

Kirubi alinunua kampuni ya Capital Media Group ambayo inamiliki stesheni ya Capital FM mwaka wa 2014.

Aliwashangaza wengi baada ya kujitangaza kuwa mmoja wa wacheza santuri katika stesheni hiyo na kujipa jina la usanii ‘DJ CK’

Bilionea huyo aliwahi kukiri kuwa alinunua stesheni ya Capital kwa sababu kampuni yake ilikuwa inatumia pesa mingi kufanya matangazo pale.

Kwenye mahjiano katika kipindi cha Churchill Show mwezi September mwaka uliopita, Kirubi alisema kuwa mapenzi yake kwa muziki wa ujana yalimfanya kununua stesheni hiyo.

7. Nairobi Bottlers

Kampuni ya Nairobi Bottlers ambayo ilimilikiwa na Kirubi inahusiana na utengenezaji na usambazaji wa vinywaji ikiwemo bidhaa za kampuni ya Cocacola.

Maji ya Keringet, juisi ya minute maid na kahawa ya Fuze ni baadhi ya bidhaa za kampuni hiyo.

8. Smart Applications International Ltd

Kirubi pia alimiliki kampuni ya kiteknolojia ya Smart Applications.