WANAJESHI WA AFRIKA

Yafahamu mataifa 10 barani Afrika yenye uwezo mkubwa wa kijeshi 2021

Uwezo wa kijeshi ni muhimu katika taifa lolote endelevu linalotaka kulinda mipaka yake mbali na maslahi yake kwa jumla .

Muhtasari

•Hakujakuwa na amani wala uthabiti katika eneo la Afrika Kaskazini tangu kung'olewa madarakani kwa Muammar Gaddafi.

•Kwa jumla Misri ndilo taifa linaloongoza kijeshi barani Afrika kutokana na ukubwa wa jeshi lake. Taifa hilo limewekwa katika nambari ya 12 kote duniani kutokana na uwezo wake.

Mwanajeshi wa DRC
Mwanajeshi wa DRC
Image: Hisani

Uwezo wa kijeshi ni muhimu katika taifa lolote endelevu linalotaka kulinda mipaka yake mbali na maslahi yake kwa jumla .

Mtandao wa Global Firepower kupitia utafiti wake umeorodhesha uwezo wa kila jeshi barani Afrika kulingana na idadi ya wanajeshi, uwezo wake wa angani, ardhini, fedha zinazotengwa kugharamia majeshi hayo, vifaa vya kijeshi, mali asli, uwezo wa majini na kadhalika.

1. Misri

Kwa jumla Misri ndilo taifa linaloongoza kijeshi barani Afrika kutokana na ukubwa wa jeshi lake. Taifa hilo limewekwa katika nambari ya 12 kote duniani kutokana na uwezo wake.

Jeshi hilo la Misri linamiliki: Jeshi la majini, Jeshi la angani.

Takriban wanajeshi 500,000 wanahudumu katika jeshi hilo, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya taifa lolote barani Afrika.

Mbali na idadi kubwa ya wanajeshi wake, taifa hilo pia lina magari 10,000 ya kijeshi , magari 60,000 ya kimkakati wa kivita, ndege 1092 za kijeshi na visima vingi vya mafuta .

Hatahivyo kitu kinacholifanya jeshi hilo kuwa la aian ya kipekee Afrika ni uwezo wake katika jeshi la wanamaji ambalo lina meli za kijeshi na manuwari zenye uwezo wa kinyuklia.

Jeshi hilo limekuwa madarakani tangu mapinduzi ya kijeshi yaliomuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi na kumuweka al. Sisi madarakani . katika kura ya maoni iliofanyika mwaka huu, mapendekezo ya mabadiliko yaliowasilishwa yalilipatia jeshi uwezo mkubwa , suala ambalo wanaharakati wanasema ilipelekea jeshi kuingilia masuala ya raia.

2. Algeria

Sawa na mataifa mengine ya Afrika Magharibi, Algeria imefanikiwa katika mpaka wake mkubwa wa maji unaoipatia fursa kubwa. Taifa hilo limefanukiwa kuweka uwezo wa kijeshi ardhini, angani pamoja na majini. Hatahivyo taifa hilo linaorodheshwa la 27 kote duniani. Algeria ina takriban wanajeshi 130,000 wanaohudumu katika jeshi lake na ina magari 2000 ya kivita

Taifa hilo hatahivyo linakumbwa na mzozo baada ya rais wake wa miaka mingi kujiuzulu, lakini jeshi limepata sauti huku ukosefu wa uthabiti na ghasia za wenyewe kwa wenyewe zikiendelea.

Mkuu wa jeshi ameonesha wasiwasi wake kuhusu mapendekezo ya kucheleweshwa kwa uchaguzi ambayo yanaweza kusababisha ghasia nchini humo.

Jeshi nchini Algeria ndilo linaloweza kukabiliana na nguvu ya kiislamu iliochukua uongozi wa taifa hilo tangu uhuru wake.

3. Afrika Kusini

Wanajehi wa Afrika Kusini
Wanajehi wa Afrika Kusini
Image: Hisani

Kwa kuwa taifa hilo halijakumbwa na mzozo wa kivita kwa muda mrefu sasa, Afrika kusini inatumia jeshi lake lililopiga hatua kiteknolojia kuweka amani na ushirikiano wa kimataifa. Ukosefu wa mizozo haujalizuia taifa hilo kulitengea jeshi lake $4.6b.

Ndege zake na vifaa vya majini zinamiliki teknolojia ya kisasa na ijapokuwa lina wanajeshi 100,000, lina uwezo mkubwa.

Mbali na kumiliki teknolojia ya hali ya angani na ardhini , jeshi la Afrika Kusini lina sifa kubwa.

4. Nigeria

Taifa hilo la Afrika magharibi limekuwa likikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram siku nenda siku rudi kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

Licha ya ufanisi mkubwa kupatikana katika awamu ya kwanza ya rais Buhari, Jeshi limepata mapigo katika kipindi cha mwaka mmoja kwasababu limefunzwa kukabiliana na jeshi jingine badala ya vita vya gorilla vinavyotumiwa na adui.

Kama Algeria na Misri, Jeshi la taifa hilo lina uwezo wa kuendelea na vita kutokana na raslimali ya mafuta linayomiliki.

Nigeria ina zaidi ya magari 1800 ya kivita , vifaru 250 , magari mengine 6000 ya kimkakati wa kivita mbali na ndege 300 za kijeshi na meli 25 za jeshi la wanamaji.

Hatahivyo uwezo wa wanamaji wake upo chini ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika yalio na mpaka wa majini.

5. Ethiopia

LOCK HEAD
LOCK HEAD
Image: Hisani

Ndilo taifa la pakee lisilo na mpaka wa majini kati ya mataifa matano bora yenye uwezo mkubwa wa kijeshi.

Taifa hilo limeelekeza raslimali yake kuu kujenga jeshi lake .

Mtandao wa GFP haufutilii mbali mataifa yasio na mpaka wa majini kwa kutokuwa na jeshi la wanamaji.

Waziri mkuu Abiy Ahmed amekuwa na uhusiano mzuri na jeshi lake tangu alipochukua madaraka huku wanajeshi wakionekana wakitembelea baadhi ya miradi ya waziri huyo na akiwaelezea maono yake kuhusu taifa hilo.

Taifa hilo kwa miaka kadhaa sasa limekumbwa na mzozo wa wenyewe kwa wenyewe , uwezo wa kuwa na jeshi thabiti umetajwa kuwa muhimu kutokana na tisho la wapiganaji wa Al-Shabab.

Taifa hilo kwa sasa lina wanajeshi 140,000 huku watu milioni 2 kila mwaka wakiafikia umri wa kujiunga na jeshi.

6. Angola

Jeshi la Angola lina vitengo vitatu: Jeshi la angani, ardhini na lile la wanamaji.

Mapema mwaka huu ajenda ya mabadiliko ya rais Lourenco ilipitishwa jeshini ambapo majenarali 88 wa jeshi waliwachishwa kazi.

Hatua hiyo inajiri baada ya kamanda wa jeshi kupoteza kazi yake alipotajwa na mwanasheria mkuu kuwa katika uchunguzi wa ufisadi.

Hifadhi ya mafuta ya taifa hilo imelifanya kuwa na uwezo wa kusimamia bajeti kubwa ya jeshi lake.

Taifa hilo lina wanajeshi 100,000 wanaosaidiwa na magari 585 ya kijeshi, vifaru 300 ,ndege za kijeshi 285 na meli 57 za wanamaji.

7. Morocco

Mapema mwaka huu, Mfalme Mohammed VI alitoa wito kwa serikali kusajili raia 10,000 wa Morocco kuhudumia jeshini kwa lazima kwa mwaka mmoja na idadi hiyo ilitarajiwa kuongezeka hadi 15,000 kufikia mwaka 2020.

Jeshi la Kifalme lina wafanyakazi 196,000.

Pia lina ndege 291, magari 2,720 ya kivita, vifaru 1,109 na manowari 121.

Jeshi hilo pia lilianza mazoezi ya kijeshi ambayo yalipewa jina na Marekani la "African Lion 2019" mnamo mwezi Machi ambayo ililenga kuifunza dhidi ya ugaidi na ghasia za itikadi kali.

Hatahivyo, licha ya bajeti yake kubwa, washirika wake wanaowafadhili kama vile Marekani wameripoti uwepo wa "ufisadi, urasimu usiofaa na kiwango duni cha elimu katika upandishaji wa vyeo jeshini."

Upelekaji wa vikosi vyake Magharibi mwa Sahara bado ndio changamoto yake kubwa hadi hivi sasa.

8. Sudan

Wanajeshi
Wanajeshi
Image: Hisani

Pengine ni nchi iliyoleta utata katika kuingizwa kwake kwenye orodha hii mwaka huu, mashujaa waliogeuka na kuwa mabaradhuli. Baada ya maandamano ya muda mrefu na waandamanaji kuamua kukita kambi katika makao yake makuu, jeshi lilimuondoa kiongozi Omar al-Bashir aliyekuwa amehudumu kwa kipindi kirefu.

Hata hivyo, wiki chache zilizopita kumekuwa na ripoti za kutokea kwa ukatili wa kijeshi huko Sudan wakati ambapo mazungumzo kati ya wawakilishi wa raia na wanajeshi yalipogonga mwamba.

Uimara wa jeshi uliendelea kukua kwa miongo ya utawala wa Bashir na pia limekuwa likipokea ufadhili kutoka kwa Saudi Arabia kwa kipindi cha miezi michache iliyopita baada ya kunyakua madaraka.

Jeshi hilo lina wanajeshi 104,000, ndege 191 za kijeshi, vifaru 410, magari ya kijeshi 403 na jumla ya manowari 18. Idadi kubwa ya vifaa hivi vinatoka Urusi na China kwasababu nchi hiyo imewekewa vikwazo na nchi za Magharibi.

9. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC)

amhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni ya pili kwa idadi kubwa ya watu Afrika ambayo ni milioni 86 Umoja wa Mataifa bado una majeshi yake nchini humo kwasababu vikosi vyake haviwezi kukabiliana na operesheni za kuleta amani kikamilifu.

Mabadiliko ya kiusalama nchini humo yalianza 2003 baada ya kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe na bado inakabiliana na juhudi za washirika wake wa kijeshi wa nchi za nje katika taasisi ya taifa ya usalama.

Nchi hiyo ina wanajeshi 134, 000 ingawa licha ya idadi hiyo bado iko nyuma kwa misingi ya mafunzo ikilinganishwa na wanajeshi wa nchi zingine.

10. Libya

Wanajehi wa Libya
Wanajehi wa Libya
Image: Hisani

Hakujakuwa na amani wala uthabiti katika eneo la Afrika Kaskazini tangu kung'olewa madarakani kwa Muammar Gaddafi.

Jeshi hilo lina vifaa imara na bila shaka ni kutokana na pesa ambazo chanzo chao ni uuzaji wa mafuta.

Nchi hiyo sasa hivi imegawanyika kati ya Tripoli na jenerali aliyeasi, Jenerali Haftar, amabye anaungwa mkono na nchi za magharibi zenye nguvu kama vile Marekani.

Serikali huko Tripoli inakabiliana na kuondoa wanajeshi waliovamia mji huo kwasababu haina kikosi thabiti.

Lakini licha ya hayo, nchi hiyo bado ina magari 2,500 ya kivita, vifaru 500, zana 600 za kivita na magari 6,500 ya usafirishaji wanajeshi

Wakati huohuo Global Firepower imeorodhesha Kenya katika nafasi 12 , Uganda katika nafasi 14 huku Tanzania ikiwa katika nafasi 23 barani Afrika