Baadhi ya watu mashuhuri nchini waliotajwa kwa sakata za kusakata ngoma ugenini

Mwaka wa 2017, mwanamke mmoja alifichua kuwa alikuwa na mtoto wa miaka 11 (kwa wakati huo) na naibu rais wa taifa la Kenya.

Muhtasari

• Siku ya Jumatatu hatua ya mwanamke mmoja aliwa silisha kesi mahakamani akitaka mahakama imshurutishe spika wa seneti Kenneth Lusaka kuwajibikia ujauzito ambao alidai ni wake.

• Mwaka wa 2017, mwanamke mmoja alifichua kupata mtoto na naibu rais wa taifa la Kenya.

Kenneth Lusaka, Dp Ruto, Okoth Obado, Mutula Kilonzo Jr
Kenneth Lusaka, Dp Ruto, Okoth Obado, Mutula Kilonzo Jr

Wa jadi walisema kutenda kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa na hakuna binadamu mkamilifu ila Mwenyezi Mungu pekee. 

Siku ya Jumatatu hatua ya mwanamke mmoja aliwashangaza wakenya wengi baada ya kuwasilisha kesi mahakamani akitaka mahakama imshurutishe spika wa seneti Kenneth Lusaka kuwajibikia ujauzito ambao alidai ni wake.

Mwanamke huyo alitaka mahakama kuagiza Lusaka kugharamia ujauzito wake  kwa kumlipa Shilingi lakini mbili kila mwezi kama pesa za kugharamia mahitaji ya mtoto ambaye hajazaliwa.

Mwanamke huyo alidai kuwa na uhusiano na spika tangu mwaka wa 2018 na wamekuwa.

Hata hivyo huyu sio mtu mashuhuri wa kwanza nchini kujipata katika kizungu mkuti cha kudaiwa kulamba asali nje ya mzinga wa nyumbani . Wafahamu wanasiasa wengine ambao wamewahi kudaiwa kujikwaa nje ya ndoa;

Naibu Rais William Ruto

Naibu rais William Ruto
Image: Maktaba

Mwaka wa 2017, mwanamke mmoja alifichua kupata mtoto wa miaka 11 (kwa wakati huo) na naibu rais wa taifa la Kenya.

Mwanamke huyo kupitia wakili Gitobu Imanyara alimshtaki Ruto kwamba alikuwa ametelekeza majukumu yake kama mzazi na alimtaka kuanza kugharamia mahitaji ya binti huyo.

Naibu rais kwa ujasiri alikiri kuwa babake mtoto huyo lakini alikanusha madai kwamba alikuwa hawajibiki katika malezi ya  binti huyo na kusema kuwa alikuwa akigharamikia mahitaji yake yote.

"Binti yangu wa miaka 11, Abby anagharamiwa vizuri ikiwemo kulipiwa masomo katika shule ya kibinafsi . Wanasiasa na wadaku wanafaa kukaa mbali"  Ruto alisema kupitia mtandao wake wa Twitter.

Ruto alifunga pingu za maisha na mama Rachel Ruto mwaka wa 1991.

Gavana Okoth Obado

Okoth obado
Gavana wa Migori Okoth Obado Okoth obado

Mwaka wa 2018, gavana wa Migori Okoth Obado alifikishwa mahakamani kwa madai ya mauaji ya mwanafunzi  aliyeaminika kuwa mpango wake wa kando.

Sharon Otieno ambaye alipatikana msituni akiwa ameuliwa alidaiwa kwamba alikuwa na ujauzito wa gavana Obado wakati wa kifo chake. Upasuaji wa mwili wake ulithibitisha kweli mwanadada huyo alikuwa mjamzito.

Wakili wa Obado, Cliff Ombeta alithibitisha kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi ila gavana huyo hakujua kuwa Sharon alikuwa na mimba .

Mutula Kilonzo Jr

mutula-696x464
mutula-696x464

Mwaka wa 2016, seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Jr alifikishwa mahakamani na mwanamke aliyemtaka kumlipa shilingi 259,000 kila mwezi ili kugharamia bintiye wa miaka tatu ambaye alidai kuwa babake.

Mwanamke huyo alidai Mutula alikuwa ametelekeza bintiye  na alitaka mahakama kumshurutisha seneta kugharamia malezi yake hadi afikishe umri wa miaka 18.

Alidai kuwa walikuwa na uhusiano na seneta kati ya mwaka wa 2012 na 2013 ila wakatengana 

Hata hivyo, seneta Mutula alikanusha madai hayo na kusema kuwa mwanadada huyo alikuwa anataka pesa zake tu.

Profesa Hamo

Mcheshi Profesa Hamo
Mcheshi Profesa Hamo
Image: Facebook

Mcheshi Herman Kago alifanywa mada ya kuongelewa na Wakenya wengi mapema mwezi wa Mei baada ya mcheshi mwenzake kwa jina Jemutai kuweka wazi kuwa alikuwa ametelekeza wanawe wawili ambao walikuwa wamepata pamoja.

Jambo hilo liliibua gumzo sana mitandao na wengi yakaendelea kufichuliwa kuhusiana na uhusiano wa wawili hao.

Ingawa Hamo alikuwa ametilia shaka watoto wale, vipimo vya kubaini uzazi zilithibitisha kuwa ndiyr baba rasmi ya watoto hao.

Kufuatila hayoaliomba msamaha hadharani kwa wanawe, familia yake, marafiki na Jemutai mwenyewe. Aliendelea kuahidi kuwa atamuao rasmi kama bibi wa piili.

“Watu huomba msamaha wakigundua wamekosea. Ilibidi nirudi kwa familia na kutafuta amani nao kwani mambo yangeharibika. Tunasuluhisha maneno. Ingawa hatujafika bado, tunaendelea vyema.” Hamo aliandika.

Hamo kwa sasa amefunga ndoa na ana watoto wawili na mkewe rasmi.

Samidoh

Samidoh
Samidoh
Image: Maktaba

Ilikuja kuwekwa wazi kuwa mwanamuziki wa nyimbo za mugithi, Samuel Muchoki almaarufu kama Samidoh ndiye baba mzazi wa mwanawe mwanasiasa Karen Nyamu mnamo mwezi wa Februari.

Fununu zilizokuwa zinaenea kuhusu uhisiano wa wawili hao zilithibitishwa wakati Samidoh alikubali kukiri kuwa alikuwa na uhusiano na mwanasiasa huyo ambao ulipelekea wawili hao kupata mtoto wa kiume.

Samidoh aliendelea kuomba msamaha kutoka kwa familia yake na mashabiki.

“Nimekosea! Nimeweka familia na nikajieka katika hali mbaya. Ni kweli nilikuwa na urafiki na Bi. Nyamu ambao ulisababisha kuzaliwa kwa mtoto ambaye hana hati.Nimekuwa nikiwajibika na nitaendelea kuwajibika kihisia na kifedha. Mimi ni baba anayefurahia wanawe” Samidoh alisema

(Mhariri: Davis Ojiambo)