MAAJABU HAYA!

Kulala ukitembea:Mmoja alijipata akiendesha pikipiki ,mwingine alishtakiwa kwa ubakaji-wakiwa wamelala!

Kutembea ukiwa umelala ama Sleepwalking ni hali ambayo mtu anaendelea kufanya shughuli kama anazofanya akiwa macho lakini akiwa usingizini

Muhtasari

•Wakati mwingi tatizo hili hutokea kwa watoto hadi umri wa miaka 18 hivi lakini kwa kawaida kufikia wakati huo ,basi unafaa usiweze kujipata unatembea au kufanya shughuli za kawaida ukiwa usingizini 

•Mnamo agosti mwaka wa 2019 mwanamme mmoja ambaye alikuwa na historia ya kutembea akiwa amelala alifutia makosa ya ubakaji baada ya siku moja kupatikana katika chumba cha mpenzi wa rafiki yake .

Mwanamke aliyelala
Mwanamke aliyelala
Image: Hisani

Kutembea ukiwa umelala ama Sleepwalking ni hali ambayo mtu anaendelea kufanya shughuli kama anazofanya akiwa macho lakini akiwa usingizini .

Hali hii pia huitwa somnambulism kwa lugha ya kitaalam . Kuna watu ambao wamefanya vitu vya kushangaza wakiwa wamelala na mara nyingi inakuwa vigumu hata kuaminika kwamba waliyafanya mambo hayo wakiwa wamelala .

Wakati mwingi tatizo hili hutokea kwa watoto hadi umri wa miaka 18 hivi lakini kwa kawaida kufikia wakati huo ,basi unafaa usiweze kujipata unatembea au kufanya shughuli za kawaida ukiwa usingizini .Cha kushangaza ni kwamba kuna watu wanaoweza kuamka na kufanya vitu vingi kama hata kupika na kula na warejee kitandani kuendelea na usingizi wao .

Umewahi kuamka ukiwa mchovu na hujui umefanya nini usiku?Chunga usije ukawa basi una hali hii ya kufanya shughuli zako ukiwa usingizini .

Hapa angalia mifano ya kweli ya watu waliofanya mambo haya wakiwa usingizini.Mmoja hata alipatikana na tuhuma za ubakaji ,mwingine alijipata anaendesha pikipiki na wa tatu aliamka na kwenda kutumia pesa kununua vitu mtandaoni -wakiwa wamelala! Hali hii wakati mwingine huweza kuwa mbaya na kumlazimu mtu kutafuta usaidizi wa matibabu ya kitaalam.

Mwanamke wa Basildon atumia pauni 3000 akiwa usingizini

Mwanamke akiwa amelala
Mwanamke akiwa amelala
Image: Hisani

Mwanake mmoja kutoka eneo la Basildon aliyekuwa usingizini alijipata ameamka na kutumia pauni 3000 kununua vitu mtandaoni .

Madaktari waligundua Kelly Knipes, kutoka Basildon huko Essex, angeacha tena kupumua usiku kucha, akilazimisha ubongo wake kuamka kidogo na kumsababisha atembee.

Aligunduliwa na hali ya kulala iitwayo parasomnia na sasa anavaa kifaa maalum cha hewa usiku ili kuhakikisha anapumua kwa usahihi.

Alisema: "Nilikuwa nimechoka sana kila wakati lakini sasa sina. Ninajisikia kama mtu mwingine kabisa."

Niliendesha pikipiki nikiwa nimelala

Kutembea usingizini kunaweza kuwa hatari wakati kuna kitu kama maji, barabara zenye shughuli nyingi au maeneo yenye miinuko anapoweza kuanguka mtu. Lakini kuendesha gari usingizini huongeza hatari kwa kiwango kipya kabisa.

Daktari mshauri wa neva Guy Leschziner anaelezea kisa cha mmoja wa wagonjwa wake, Jackie, ambaye amekuwa akiendesha pikipiki au hata gari akiwa usingizini.

Muda mfupi baada ya kuhamia Uingereza kutoka Canada, Jackie alikuwa akikaa na mwanamke mmoja wa umri wa juu .

"Asubuhi moja aliuliza," Ulienda wapi jana usiku? "Jackie anasema.

Jackie alisema hakuwa ameenda popote.

"Sawa, umetoka na pikipiki yako," mama mwenye nyumba akajibu.

Jackie alishtuka. Yeye aliuliza mara moja ikiwa alikuwa amevaa kofia yake ya kujikinga .

"Ndio, ulishuka kutoka chumbani mwako ulikuwa na kofia yako na ukatoka," mama mwenye nyumba alisema, akiongeza kuwa alikuwa amekwenda kwa muda wa dakika 20.

Jackie hakuwa na kumbukumbu ya safari yake ya usiku kwa sababu alikuwa amelala wakati huo. Na hakukuwa na dalili zingine kuashiria alikuwa ametoka nje, kwani alikuwa amerudisha pikipiki mahali ilipokuwa .

Wakati akiwa mdogo wakati walipkuwa wamekwenda kupiga kambi huko Vichakani ansema alikuwa akifanya vitu nyakati za usiku kisha baadaye anashangaa alikuwa wapi .

"Ningeamka katikati ya usiku na ningeshuka kwenda mtoni. Ningeingia msituni na unajua hawangeweza kunivumilia, kwa hivyo ilibidi nichukuliwe na kurudishwa nyumbani tena. "

Jackie alikuwa mtu anayetembea usingizini .

Mwanamume aliyetembea akilala afutiwa makosa ya ubakaji

sad man
sad man

Mnamo agosti mwaka wa 2019 mwanamme mmoja ambaye alikuwa na historia ya kutembea akiwa amelala alifutia makosa ya ubakaji baada ya siku moja kupatikana katika chumba cha mpenzi wa rafiki yake .

Dale Kelly, 21, aliingia kwenye chumba cha kulala cha wenzi hao, akaingia kitandani mwao na kumgusa mwanamke huyo kwa karibu.

Wakili wake aliyemtetea kortini aliwaambia majaji kwamba Kelly hakuweza kusema ni nini kilitokea kwani alikuwa amelala wakati huo.

Jaji Simon Hickey alisema Kelly kutoka Dalton-le-Dale katika Kaunti ya Durham, alikuwa akifikiria kutoa agizo la kumzuilia mtuhumiwa hospitalini.

Majaji waliotoa uamuzi wilichukua zaidi ya masaa mawili kuamua kwamba Kelly alikuwa ametenda kosa hilo lakini alikuwa akisumbuliwa na parasomnia wakati huo - ikimaanisha hakuwajibikia vitendo vyake.

Jaji Hickey aliielezea kama kesi "isiyo ya kawaida" na akasema chaguzi za hukumu zilipunguzwa kwa agizo la hospitali, agizo la usimamizi au kutolewa kabisa

Alipatikana kitandani

Mahakama ilisikia kwamba Kelly alikuwa kwenye kilabu cha usiku na rafiki yake na mwanamke huyo kabla ya kurudi nyumbani huko North Yorkshire kwenye teksi asubuhi ya 17 Aprili.

Kelly alilala ndani ya teksi na kwenda moja kwa moja kitandani walipofika lakini karibu saa moja baadaye yule mwanamke aliamka na kumkuta kwenye kitanda alichokuwa akilala na mwenzake.

Alisema aliamini Kelly alikuwa amemnyanyasa kingono na kuwaita polisi.

Eleanor Fry, akimtetea, alisema Kelly hakuweza kusema ni nini kilitokea asubuhi hiyo kwa kuwa alikuwa amelala wakati huo.

Korti ilisikia kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa parasomnia tangu utotoni na wataalam walisema alikuwa "labda" au "ana uwezekano wa kuwa" aliugua shida ya kulala wakati wa shambulio hilo linalodaiwa lakini hawakuweza kusema kwa hakika.

Jaji Hickey alisema madaktari katika kesi hiyo waliamini "ugonjwa wa akili" wa Kelly unatibika na unahitaji kutibiwa.

"Kwa sasa ninaegemea agizo la hospitali lakini nitasubiri kusikia wataalam wanasema nini," jaji huyo akaongeza.