Mambo unayostahili kufanya baada ya kuachana na mpenzi wako

Muhtasari
  • Mambo unayostahili kufanya baada ya kuachana na mpenzi wako
  • Moja ya jambo ngumu zaidi ni kuwa na uhusiano na mtu ambaye anajipenda sana kuliko vile anakupenda
  • Hata hivyo, wakati umeamua huwezi kuishi na mateso ya akili ya kuwa katika uhusiano na mtu anajipenda

Moja ya jambo ngumu zaidi ni kuwa na uhusiano na mtu ambaye anajipenda sana kuliko vile anakupenda.

Hata hivyo, wakati umeamua huwezi kuishi na mateso ya akili ya kuwa katika uhusiano na mtu anajipenda, na kumuacha ni moja ya mambo magumu ambayo utawahi kufanya.

Hapa ni baadhi ya mambo unayohitaji kufanya baada ya kumtupa mpenzi wako.

1.Mpe block, usiwe rafikiye

Ukitaka kumsahau mpenzi wako, na kusahau mateso ambayo ulipiia ukiwa nawe, kwa maana ni kawaida kupitia mateso, ukiwa atika uhusiano na mtu ambaye anajipenda mpe block na wala usiwe rafiki yake hasa kwenye mitandao ya kijamii.

2.Jiwezeshe mwenyewe kupitia elimu yako mwenyewe.

Moja ya sababu wengi waathirika wa unyanyasaji wa mtu anayejipenda  hawatambui kuwa ni waathirika mpaka baadaye au hata baada yamwisho wa uhusiano ni kutokana na ukosefu wa ujuzi wa kile kinachofanya unyanyasaji.

3.Wachana na watu ambao hawayuko upande wako kwa asilimia 100

Kuna baahi ya marafiki ambao mkiachana na mpenzi wako watakuwa upande wa mpenzi wako lakini hawatakuonyesha

Kama rafiki au marafiki zako hawayuko upande wako kwa asilimia 100 haya basi wateme ili uweze kuendelea na maisha yako.

4. Usifungie ya kale

Ndio yakumbuke mamb ambayo uliyapitia na funzo ambalo ulipata kutoka kwa uhusiano wako wa awali.

Unapoyazungumzia haya basi utajipata umesahau mateso hayo na kuendelea na maisha yako ya sasa.