Mafunzo muhimu kila mkenya anapaswa kujifunzwa kutokana na drama ya Omosh

Muhtasari
  • Mafunzo muhimu kila mkenya anapaswa kujifunzwa kutokana na drama ya Omosh

Kipindi cha Tahidi High kilitumbuiza Wakenya sana miaka kwa zaidi ya mwongo mmoja, huku nyota Omosh akifahamika sana kupitia kwenye kiindi hicho.

Kipindi hicho kilishirikisha baadhi ya waigizaji na watangazaji bora nchini wakiwemo Ken Wakuraya,Abel Mutua , Sarah Hassan miongoni mwa wengine.

Wengi wa waliokuwa waigizaji kwenye kipindi hicho waliendelea kubombea kwenye vitengo mbalimbali vya usanii.

Hata hivyo, kunao baadhi yao ambao hawakuweza kustawi baada ya kuondoka Tahidi High. Mmoja wao ambaye ameibuaa gumzo mitandaoni ni Joseph Kinuthia almaarufu kama Omosh.

Kwa muda sasa Omosh amekuwa akivuma baada ya kujitokeza wazi wazi mnamo FEbruari na kusema ya kwamba na hitaji msaada kutoka kwa wakenya na wasamaria wema.

Alipata msaada, na hata kujengewa nyumba.

Mnamo Juni25 Ijumaa akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba anahitaji msaada tena mabapo wakenya walimkejeli na kumshambulia.

Je ni mafunzo yapi muhimu wakenya wanapaswa kujifunza kutoka kwa muigizaji huyo?

1.Mtegemea cha nduguye hufa maskini

Kama kenya unapaswa kujua na kufahamu kwamba lazima utie bidii katika kazi yako ili upate mkate wa kila siku na wala sio kutegemea jasho la mwenzio.

2.Akiba

Endapo unafanya kazi unapaswa kuwekeza akiba kwa ajili ya maisha yako ya usoni, na wala sio kula pesa zako zote.

3.Shukrani

Baada ya kusaidiwa na wakenya Omosh angetoa shukrani kwao badala ya kuwakejeli na kusema kwamba hakuwalazimisha mtu yeyote amsaidie.

4.Bidii

Baada ya Omosh kusaidiwa angefanya juu chini na ata kutafuta kazi yeyote na kutia bidii ili hasirudi mahali alikuwa pa kuomba omba.