Umepatana na wao?Tabia za ajabu vijakazi wa nyumbani hufanya

Muhtasari
  • Tabia za ajabu vijakazi wa nyumbani hufanya
  • Wanawake wengi hufanya kazi kama wajakazi au wasaidizi wa nyumba  nchini Kenya lakini duniani kote pia
  • Katika Kenya, kazi hiyo inaongozwa sana na wanawake lakini kuna wanaume pia
mBOCH
mBOCH

Wanawake wengi hufanya kazi kama wajakazi au wasaidizi wa nyumba  nchini Kenya lakini duniani kote pia.

Katika Kenya, kazi hiyo inaongozwa sana na wanawake lakini kuna wanaume pia.

Kuna tabia nyingi za ajabu zilizoonyeshwa na wasichana ambao Wakenya wengi wanaweza kuthibitisha kuwa wamepatana nazo au wajakai wao wamekuwa wakifanya.

Tabia hizo nikama;

1.Kuchukua wanaume wa nyumba

Sio hadithi mpya wakati unasikia mume wa nyumba alikimbia na mjakazi Wakati mwinginena pia ukifuata kwa karibu mlinzi wa nyumba alikuwa nafahamu hayo yote.

2.Kula chakula cha watoto

Kuna baadhi pia wajakazi abao wanatabia ya kula chakula cha watoto baada ya kuachwa na mwajiri wao pekeyao, kisha wanasema kwamba ni watoto walikula chakula.

3.Kuiba

Pia una wale wna mkono mrefu wa kuiba vitu vya dhamana katika nyumba na kupeleka kwao wakati wanaenda kutembelea jamaa zao.

4.Masengenyo na wafanyakazi wenzao

Mwajiri anaweza pata hadithi yake inafahamika sana na wajakazi wa nyumba zingine kuliko vile familia yake inamfahamu.

wajakazi wengi wana tabia ya kutoa siri za mwajii wake kwa wajakazi wenake kila mara.

5.KUwanyanyasa watoto na kuwaiba

Kuna baadhi ya wafanyakazi nyumbani wanatabia ya kuwacharaza watoto wa wajiri wao vibaya sana, pi tumeina katika video mitandaoni wengi wakitekeleza kitendo hicho.

KUna wale pia watawaiba watoto wa wajiri wao na kutoroka nao bila ya kujua wala kufahamu sababu ya kitendo hicho.

Kama unamtafuta kijakazi wa nyumbani kwako haya basi kuwa makini yule unamleta nyumbani kwako.