Fahamu baadhi ya marais wa bara Afrika waliowahi kuuliwa wakiwa madarakani

Habyarimana alikuwa katika hali tatanishi wakati ndege aliyokuwa anasafiri nayo pamoja na rais wa Burundi kwa wakati huo, Cyprian Ntaryamira kulipuliwa ikiwa angani.

Muhtasari

•Lumumba aliuliwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa kikoloni mnamo Januari 17, 1961.

•Mwili wa Doe ambao ulikuwa umenyolewa na ulikuwa na ishara za kuchomwa na sigara ulionyeshwa hadharani ukiwa uchi jijini Monrovia.

MARAIS WALIOULIWA AFRIKA
MARAIS WALIOULIWA AFRIKA

Kifo cha rais wa HaitiJovenel Moïse ambaye aliuliwa kwenye mashambulizi ya risasi katika makazi yake jijini kuu la Port-au-Prince siku ya Jumatano kilishangaza wengi kote duniani.

Ikawaje kiongozi wa taifa, kamanda mkuu wa jeshi akashambuliwa na kuulia kwa namna hiyo?

Hata hivyo, Moise si rais wa kwanza kuuliwa akiwa madarakani. Zaidi ya viongozi wa nchi zaidi ya 100 kote  duniani wameuliwa ndani ya kipindi cha karne moja iliyopita.

Hawa baadhi ya viongozi wa taifa waliouawa barani Afrika wakiwa madarakani;

Patrice Lumumba  (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, 1961)

Lumumba aliuliwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa kikoloni mnamo Januari 17, 1961.

Iliripotiwa kuwa mwili wake ulichomwa na  asidi ya sulfuriki ili usiwahi patikana.

Alikuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kihalali nchini Congo.

PATRICE LUMUMBA
PATRICE LUMUMBA

Abeid Karume (Zanzibar/Tanzania, 1972) 

Karume alikuwa rais wa kwanza wa Zanzibar na naibu rais wa kwanza wa muungano wa Jamhuri ya Umoja ya Tanzania.

Alikuwa madarakani kati ya mwaka wa 1964 na 1972.

Karume aliuliwa kwa kupigwa risasi na watu wanne alipoikuwa anacheza 'bao' katika makao makuu ya chama cha Afro-Shirazi, mjini Zanzibar mnamo Aprili 7, 1972.

Marien Ngouabi (Jamhuri ya Congo, 1977)

Ngouabi alikuwa rais wa tatu wa Jamhuri ya Congo kati ya mwaka wa 1969 na 1977.

Aliuliwa kwa kupigwa risasi  akiwa nyumbani kwake  jijini Brazaville.

Ilisemekana kuwa rais wa awali, Alphonse Masssamba Debat alikuwa nyuma ya mauaji hayo.

Thomas Sankara (Burkina Faso, 1987)

Sankara ambaye alikuwa mwanajeshi alihudumu kama kiongozi wa Burkina Faso kati ya mwaka wa 1983 na 1987 baada ya kubandua serikali iliyokuwa inatawala.

Uongozi wake wa mapinduzi ulisifiwa sana kote Afrika.

Aliuliwa mnamo Oktoba 15, 1987 na kikosi kilichoongozwa na Blaise Compaore ambaye alichukua uongozi.

THOMAS SANKARA
THOMAS SANKARA

Samuel Doe (Liberia, 1990)

Doe aliongoza nchi ya Liberia kati ya mwaka wa 1980 na 1990 baada ya kubandua serikali iliyokuwa inatawala.

Aliteswa na kuuliwa mnamo Septemba 9, 1990.

Mwili wa Doe ambao ulikuwa umenyolewa na ulikuwa na ishara za kuchomwa na sigara ulionyeshwa hadharani ukiwa uchi jijini Monrovia

Melchior Ndadaye (Burundi, 1993)

Ndadaye alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Burundi kwenye uchaguzi  wa 1993.

Uongozi wake haukufurahisha wanajeshi amabo wengi walikuwa wa jamii pinzani ya  Tutsi.

Aliuliwa katika jaribio lankijeshi kupindua serikali miezi mitatu baada ya kukalia kiti cha urais.

Juvenal Habyarimana(Rwanda, 1994)

Habyarimana alijulikana kama 'Kinani' nchini Rwanda kumaanisha 'ambaye haonekani'.

Alihudumu kama rais wa pili wa Rwanda kati ya mwaka wa 1973 na 1994.

Habyarimana alikuwa katika hali tatanishi wakati ndege aliyokuwa anasafiri nayo pamoja na rais wa Burundi kwa wakati huo, Cyprian Ntaryamira kulipuliwa ikiwa angani.

Kuuliwa kwake kulisababisha mizozo ya kikabili na kuchangia mauji mabaya ya 1994.

Cyprian Ntaryamira (Burundi, 1994)

Ntaryamira alihudumu kama rais wa Burundi kwa kipindi cha miezi miwili tu kati ya Februari 5, 1994 na Aprili 6, 1994.

Alikufa pamoja na rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda mnamo Februari 5, 1994 baada ya ndege waliyokuwa wanasafiri nayo kulipuliwa kwa bomu ikiwa hewani.`

Laurent-Desire Kabila (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, 2001)

LAURENT DESIRE KABILA
LAURENT DESIRE KABILA

Kabila alikuwa rais wa tatu wa Congo  ambaye alihudumu kati ya mwaka wa 1997 na 2001 baada ya kupindua serikali ya Mobutu Sese Seko.

Alipigwa risasi akiwa ofisini mwake  jijini Kinsasha mnamo Januari 16, 2001 na kupelekwa Zimbambwe kupata matibabu. Kufariki kwake kulitangazwa siku mbili baadae.

Mwanawe Joseph Kabila alichukua uongozi wa taifa hilo siku nane baadae.

Joao Bernardo Viera (Guinea Bissau, 2009)

Viera alihudumu kama rais wa Guinea Bissau kwa mihula mitatu.

Aliondolewa mamlakani kufuatia vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka wa 1999 na kuenda mafichoni ila akarejea tena mwaka wa 2005 na kushinda kiti cha urais.

Aliuliwa na wanajeshi mnamo Machi 2, 2009.`

Idriss Deby (Chad,  2021)

IDRIS DEBY
IDRIS DEBY
Image: HISANI

Deby aliongoz nchi ya Chad kwa miaka 30 kuanzia Desemba 2, 1990 hadi Aprili 20, 2021 alipokumbana na kifo chake.

Aliuliwa mnamo Aprili 2021 wakati alikuwa anaongoza wanajeshi waliokuwa wanakabiliana na waasi wa Front for Change and Concord in Chad(FACT).

Ilisemekana kuwa aliaga kutokana na majeraha mwilini aliyopata kwenye vita hiyo