Mafunzo muhimu kila polisi anapaswa kujifunza kutoka kwa habari ya askari Kangogo

Muhtasari
  • Mafunzo muhimu kila polisi anapaswa kujifunza kutoka kwa habari ya askari Kangogo
Mshukiwa wa mauji ya watu wawili Caroline Kangogo
Mshukiwa wa mauji ya watu wawili Caroline Kangogo
Image: HISANI

Polisi wa kike aliyetajwa kama Koplo Caroline Kangogo, aligonga vichwa vya habari kwa kumuua polisi mwenzake  John Ogweno, katika mji wa Nakuru.

Kilomita 200 kutoka eneo la tukio la kwanza polisi huyo alimuua kwa kumpiga risasi mwanaume mwingine Peter Njiru mwenye umri wa miaka 32 .

Hali inayozingira mauaji ya wawili hao ni ya kutatanisha kwani hakuna aliye na uhakika kabisa wa kiini cha mauaji yao.

Huku wazazi wake wakizungumza kwa mara ya kwanza tangu visa hivyo kutendeka walimtaka Caroline ajisalimishe kwani anafahamu sheria vyema.

Lakini ni mafunzo yapi kila polisi au kila mkenya anapaswa kujifunza kutokana na habari hiyo?

1. Mapenzi

Kama wafahamu vyema wataka kuachana na mpenzi wako, haya basi msiachane kwa roho mbaya mnapaswa kusikilizana na kuachana kwa uzuri ili kila mmoja anapoendelea na maisha yake asiweze kuumiza maisha ya mwenzi wake.

2.Msongo wa mawazo au tatizo

Tunafahamu vyema kwamba kazi ya kitengo cha polisi na sio kazi rahisi, kama unatatizo na mpenzi wake na mmeachana nenda ukamtafute mtalaamu akupe ushauri ili usije ukafikiria mambo na mauaji.

3.Mpango wa kando

Ni tabia ambayo wanaume na wanawake wameamini lazima wawe na mpango wa kando ili maisha yao yaendelee, kama unajua kwamba unampango wa kando na mambo yenu hayaendi vyema,zungumzeni na mtatue shida zenu kwani mauaji au ugomvi hautatatua jambo lolote.

Yote tisa kumi ni kuwa kumbuka kazi yako na familia yako ni muhimu, na endapo utafikiria kutoa uhai wa mwenzako fahamu hautamrudisha duniani, na kwamba akifariki kuna wale wataachwa mayatima.