Tamaa au laana? Mume wangu hajui kwamba mpango wangu wa kando ni ndugu yake-Mwanamke akiri

Muhtasari
  • Ni kweli siku za mwisho zimewadia au tu ni porojo ya wanadamu,lakini kulingana na maoni yangu siku hizo zimewadia kwa sababu ya tabia za watu wengi duniani
  • Baadhi ya watu wengi hawaheshimu ndoa zao, kwa njia moja au nyingine
  • Nani wa kulaumiwa wakati mwanamume au mwanamke ameanza tabia kama hizo?
Side view of young woman with eyes closed
Side view of young woman with eyes closed

Ni kweli siku za mwisho zimewadia au tu ni porojo ya wanadamu,lakini kulingana na maoni yangu siku hizo zimewadia kwa sababu ya tabia za watu wengi duniani.

Baadhi ya watu wengi hawaheshimu ndoa zao, kwa njia moja au nyingine.

Nani wa kulaumiwa wakati mwanamume au mwanamke ameanza tabia kama hizo?

Kuna wale wanawatafuta mipango wa kando, na hata wengine kuwadhulumu wake zao na kuwaacha na shida.

Ziara

Nikiwa kwenye ziara zangu nilipatana na mwanamke mmoja ambaye hakutaka kujilikana kwa jina, na kunisimulia jinsi amekuwa akienda nje ya ndoa.

Licha ya hayo mumewe anafahamu kwamba ana mpango wa kando lakini hajui ni nani.

"Nimekuwa katika ndoa yangu kwa miaka 6 na nusu, nilianza kuenda nje ya ndoa mume wangu alifahamu na kisha nikamwambia kinagaubaga kwamba hanitoshelezi kitandani

Ndio anafahamu kwamba nina mpango wa kando lakini hajui kwamba mpango wangu wa kando ni ndugu yake

Nimekuwa naye sasa kwa mwaka mmoja, na ambaye nimekuwa nikifanya naye tendo la ndoa, naskia kumuacha mume wangu niolewe na ndugu yake lakini nitaleta vurugu nyumbani nikifuata maamuzi hayo

Sijui nifanye nini kwa maana kwa sasa sina hisia zozote za mume wangu," Alieleza mwanamke huyo.

Kwa maoni yangu anapaswa kutosheka na mume wake,na kumpenda mumewe kama awali, je ushauri wako ni upi?