Maajabu!Mpenzi wangu anataka kunirudia baada ya kuambukizwa virusi vya ukimwi-Mwanamume asema

Muhtasari
  • Jamaa asimulia jinsi mpenzi wake alipata virusi vya ukimwi
sad man
sad man

Ni kawaida watu waiwa kwenye uhusiano wawe na ugomvi huku wengi wakiamua kuachana na jambo moja au lingine.

Kuna wale hujaribu kila wawezalo ili watatue shida zao na kuendelea na maisha yao.

Pia kuna wale huwa hawatosheki na wapenzi wao, huku wakitoka nje ya ndoa au uhusiano wao,lakini wakikaa bila wapenzi wao wanaanza kujuta na kuwapenzi waliokuwa wapenzi wao na kutaka warudiane tena.

Ziara

Nikiwa katika ziara yangu, katika makala haya tutazingatia mwanamume ambaye alinisimulia hadithi yake na aliyekuwa mpenzi wake.

Kulingana na John alipatana na mpenzi wake akiwa shule ya upili, na walibarikiwa na mtoto mmoja.Huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa kidato cha tatu nilipopatana na mpenzi wangu ambaye alikuwa ametoka kidato cha nne, tulianzisha uhusiano wa kimapenzai na nilimpenda sana

Baada ya kumaliza shule tulibarikiwa na mtoto mmoja, tulikuwa tumeoanga kuona, mtoto alipofikisha mwaka mmoja na nusu aliniambia kuwa anaenda Nairobi kutafuta kazi

Nilimruhusu, lakini alipofika miezi michache baadaye alibadilisha tabia, alikuwa ananitumia pocha akiwa uhi na wanaume kitandanai, na ahta video wakifanya tendo la ndoa

Nilikanya lakini hakunisikia,  sasa amerudi na anataka turudiane licha ya mambo yoe alinifanyia baada yake kufika Nairobi

Pia aliniambaia kwamba amepatwa na virusi vya ukimwi baada ya kuwa na wanaume tofauti, sijui nimrudie ama nimuache nataka ushauri," John alieleza.

Je utampa ushauri upi John arudiane na mpenzi wake au aendelee na maisha yake.