Baba auawa kwa kupigwa risasi kwa kumbaka bintiye - Somalia

Mahakama katika mji wa Dhobley umemkuta Hussein Adan Ali mwenye umri wa miaka 28

Muhtasari

• Viongozi wa jadi na maofisa wa mahakama walipitia ushahidi kabla ya kutekeleza hukumu hiyo.

• Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa chini ya sheria za kiislamu, mahakama ilisema.

Mwanaume mmoja nchini Somalia auawa kwa kupigwa risasi mpaka kufa huko kusini mwa Somalia na serikali ya Jimbo la Jubaland baada ya kumbaka binti yake wa kambo mwenye umri wa miaka mitatu ambaye alifariki kutokana na majeraha ya kubakwa.

Mahakama katika mji wa Dhobley umemhukumu Hussein Adan Ali mwenye umri wa miaka 28, amekutwa na hatia siku ya Jumatano, na ilitangazwa Jumatano katika kituo cha Televisheni cha eneo hilo.

Viongozi wa jadi na maofisa wa mahakama walipitia ushahidi kabla ya kutekeleza hukumu hiyo.

Kwa mujibu wa ushaidi, Ali alikuwa amekula mirungi wakati alipomfanyia unyanyasaji huyo mtoto.

Haijaweka wazi tukio hilo lilitokea wapi lakini mahakimu wamesema mtoto amefariki Jumatano.

Matangazo ya Televisheni hayakuonesha kama mawakili walihudhuria mahakamani au mshutumiwa kama alipata fursa ya kukata rufaa.

Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa chini ya sheria za kiislamu, mahakama ilisema.

Televisheni ya taifa ya Somalia iliweka picha ya Ali katika kurasa yake ya twitter: