Covid-19: Maambukizi yaongezeka Kenya

Jumla ya wagonjwa 340 wamepona, 272 kutoka mpango wa Kutengwa na kutibiwa nyumbani huku 68 wakiwa kutoka vituo hospitalini

Muhtasari

• Kenya imesajili visa vipya 837 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,545 chini ya saa 24 zilizopita.

• Wagonjwa wengine 1,058 wamelazwa katika hospitali mbali mbali, huku 4,407 wakiwa chini ya mpango wa Kutengwa Nyumbani.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya imesajili visa vipya 837 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,545 chini ya saa 24 zilizopita.

Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 191,020 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 11.1.

Watu tisa walifariki kufikisha Jumla ya watu 3,746 walioangamia kutokana na virusi vya Covid-19 baada ya vifo vipya kuripotiwa kutoka kwa ukaguzi wa rekodi za hospitali miezi ya Aprili, Mei, Juni na Julai, 2021.

Jumla ya wagonjwa 340 wamepona, 272 kutoka mpango wa Kutengwa na kutibiwa nyumbani huku 68 wakiwa kutoka vituo hospitalini.

Idadi ya waliopona sasa ni 180,420.

Kulingana na takwimu zilizotolewa siku ya Alhamisi wagonjwa wengine 1,058 wamelazwa katika hospitali mbali mbali, huku 4,407 wakiwa chini ya mpango wa Kutengwa Nyumbani.

Wagonjwa wengine 129 wako katika Kitengo cha Huduma ya wagonjwa mahututi (ICU), 38 kati yao wanapokea msaada wa upumuaji na 65 wakiwa kwenye oksijeni ya ziada, wagonjwa 26 wako chini ya uangalizi.

Sajili za maambukizi ni kama ifuatavyo, Nairobi 376, Mombasa 87, Nyeri 45, Kiambu 34, Kilifi 33, Uasin Gishu 32, Nakuru 26, Siaya 23, Kajiado 21, Kericho 15, Bungoma 13, wakati Busia, Nyamira, Kisumu, Makueni na Laikipia zikirekodi visa 11 kila mmoja.

Kitui ilirekodi visa 10, Embu na Turkana 7 kila moja, Machakos, Nyandarua na Homa Bay 6 kila moja, Elgeyo Marakwet, Garissa na Migori 5 kila moja, Baringo, Bomet na Kakamega 4 kila moja, wakati Kwale, Lamu, Marsabit, Meru, Narok, Isiolo, Taita Taveta na Tharaka Nithi zikirekodi kisa kimoja kimoja.