Hizi hapa sababu kwa nini msanii Diamond Platnumz ni mfano mwema kwa vijana

Muhtasari
  • Msanii na staa wa bongo kutoka Tanzania Diamod Platnumz amekuwa akivuma tangu kutoa kibao chake cha kwanza
  • Safari ya msanii huyo inafahamika sana na mashabiki wake, kwani hakuanza tu juzi bali miaka michache iliyopita
Diamond Platnumz

Msanii na staa wa bongo kutoka Tanzania Diamod Platnumz amekuwa akivuma tangu kutoa kibao chake cha kwanza.

Safari ya msanii huyo inafahamika sana na mashabiki wake, kwani hakuanza tu juzi bali miaka michache iliyopita.

Licha ya changamoto ambazo msanii huyo huopatana nazo, kwenye tasnia amekuwa akitia bidii na hata kutoa vibao akiwashirikisha wasanii tofauti.

Msnii huyo hajakuwa akiwatenga wasanii chipukizi bali amekuwa akikuza talanta zao na hata kuwasajili baadhi ya kwenye lebo yake ya WCB.

Lakini swali kuu ni je msanii huyo ni mfano mwema kwa vijana wa wakati wa sasa?

Kulingana na mao no yangu Diamond ni mfano mwema kwa vijana wengi hasa wenye wana ndoto ya kuwa wasanii.

Hizi hapa sababu kwa nini msanii Dimond ni mfano mwema kwa vijana;

 

1.Familia

Licha ya Dimaond kuwa na watoto na wanawake ofauti amekuwa akiwasaidia, na hata kupenda familia yake hasa mama yake mzazi

2.Kazi

Msanii huyo amekuwa akitia bidii katika kazi yake, miezi mieili iliyopita amekuwa Marekani, na kushirikiana na wasanii wa nchi hiyo, ambapo mashabiki wanaamini walikuwa wanajitayarisha kwa ajili ya kibao katika albamu yake

3.Bidii

Wakati huu wa sasa vijana wengi hawataki kutia bidii, lakini msanii huyo amewaonyesha ukitaka kuishi maisha mazuri unapaswa kuwa na bidii katika kazi yako yote.

4.Pesa

Diamond hajakuwa akiharibu pesa zake oovyo ovyo bali amekuwa akiwekeza katika kazi yake jambo ambalo vijana wengi wanapaswa kujifunza kutoka kwake.