Fahamu siri za kuishi miaka mingi duniani

Ulaji wako kabla ya muda wa kulala, ndiyo tiketi yako ya safari ya umri, kituo gani na cha umbali gani utashukia pale utakapomaliza safari yako duniani.

Muhtasari

•Kipimo cha sukari ya nyongeza inayokubalika ni vijiko vidogo vya chai visivyozidi 6 kwa mwanamke na visivyozidi 9 kwa mwanaume.

•Mikate ya nafaka tupu inakuwa na virutubisho na madini aina ya tryptophan na magnesium; yanayotajwa kusaidia kiwango cha serotonin mwilini ambacho ni silaha ya uzalishwaji wa melatonin ambacho hukusaidia kutokuwa na mihangaiko na kulala vyema.

Jeanne Calment kutoka Ufaransa, ndiye binadamu aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi duniani, alifikisha umri wa miaka 122 na siku 164 kwa mujibu wa rekodi za Guinness.
Jeanne Calment kutoka Ufaransa, ndiye binadamu aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi duniani, alifikisha umri wa miaka 122 na siku 164 kwa mujibu wa rekodi za Guinness.
Image: GETTY IMAGES

Jeanne Calment kutoka Ufaransa, ndiye binadamu aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi duniani, alifikisha umri wa miaka 122 na siku 164 kwa mujibu wa rekodi za Guinness.

Katika imani tofauti, kuishi muda mrefu una kudra zake, lakini kisayansi, zipo sababu za wazi kabisa ambazo wanasayansi wamezitafiti na kuzithibitisha kwamba zina uwezo kutafsiri na kuamua kiwango gani cha umri binadamu anaweza kuishi.

Inawezekana ingawa ngumu kuamua kwa fikra za kawaida na ni rahisi kufikiria kwamba liko nje ya uwezo wako. Lakini watafiti wanaeleza kwamba pamoja na sababu nyingine, lakini nini unachokula ama kunywa wakati wa kulala kina mchango mkubwa sana wa kuamua uishi kwa muda gani.

Kwa sasa Shirika la Afya duniani (WHO) linasema wastani wa umri wa kuishi binadamu duniani ni miaka 72, ambapo mwanaume ni miaka 69 na miezi 8 na mwanamke ni 74 na miezi miwili.

Ulaji wako kabla ya muda wa kulala, ndiyo tiketi yako ya safari ya umri, kituo gani na cha umbali gani utashukia pale utakapomaliza safari yako duniani.

Hakuna siri kubwa ya kukuwezesha kuishi umri mrefu zaidi, na siri hizo tano zinabainishwa na wanasayansi.

1. Acha kula vyakula vyenye sukari ya nyongeza kabla ya kulala

Image: GETTY IMAGES

Ni rahisi tu kusema, sukari ni mbaya, na ubaya wake unazidiana na aina ya sukari. Ziko aina nyingi za sukari karibu 17, lakini sukari mbaya zaidi ni ile unayoiongeza wakati wa ulaji wako. Pamoja na umuhimu wake kwenye mwili, sukari inayoshauriwa zaidi ni ile inayopatikana kwenye vyakula tunavyokula bila kuiongoza.

Kipimo cha sukari ya nyongeza inayokubalika ni vijiko vidogo vya chai visivyozidi 6 kwa mwanamke na visivyozidi 9 kwa mwanaume.

Ni kama wastani wa gramu zisizozidi 30 kwa siku. Lakini Shirika la afya duniani (WHO) linashauri kwa siku mtu kutumia angalau vijiko viwili vya chai ama gramu zisizozidi 10.

Ukitumia hivi utakuwa sawa, lakini ukiacha kabisa sukari ya nyongeza inayotumika sana kwa mfano kwenye vitu kama chai, vinywaji kama soda, 'Ice cream', keki na vingine, utajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuepuka maradhi, kulala vizuri na tatizo la kuchelewa kulala.

Utafiti unaonyesha kuwa karibu nusu ya watu walioishi umri mrefu zaidi wa miaka 80 walikuwa hawatumii sukari kabisa katika muda mrefu wa maisha yao, au wengine walikuwa wameacha kutumia sukari ya nyongeza, na wachache kabisa walikuwa wanatumia kwa uchache.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba unapokula sukari wakati wa chakula cha usiku ama jioni ama muda mfupi kabla ya kwenda kulala ama muda unajiweka katika hatari zaidi ya kupata vitambi, unene, magonjwa kama saratani, moyo, pata chunusi na mengine.

2. Unywaji wa green tea 'chai ya kijani'

Image: HEALTHYWOMEN

Ni kawaida hasa nyakati za asubuhi kukuta watu wakinywa chai. Chai ni kitu kinachotumiwa sana karibu na jamii nyingi duniani, licha ya uwepo wa vinywaji vingie. Katika maeeo ambayo watu wake wanaishi umri mrefu wanatumia green tea' pamoja na vinywaji vingine kama maji, kahawa, na wine nyekundu.

Moja ya faida ya green tea ni kwamba inakitu kinaitwa antioxidants, ambacho ni muhimu sana katika kulinda seli za mwili dhidi ya magonjwa ya moyo, saratani na magonjwa mengine.

Watafiti wanasema ukiinywa bila kuweka sukari, itafanya kazi vizuri zaidi katika mwili kuliko chai ya kawaida ama kahawa. Maeneo mengi watu wake wanaoshi kwa muda mrefu ikiwepo Japan wanatumia zaidi 'green tea'.

3. Unywaji wa divai nyekundi baada ya saa 11

Image: GETTY IMAGES

Unaweza kushangazwa na hili, ukajiuliza inawezekana vipi Divai nyekundu ikawa ni kitu kinachoweza kumsaidia mtu kuishi miaka mingi. Mwandishi na mtafiti Dan Buettner anakiri unywaji huu wa divai na matokeo yake unaleta sintofahamu kwa sababu inaonekana kana kwamba utafiti unapigia chapuo unywaji wa pombe kama kitu kizuri kwa afya.

"Naelewa tafiti za hivi karibuni zikionesha vileo vinaongeza uwezekano wa kupata saratani hasa ya matiti kwa wanawake na magojwa mengine. Lakini naweza kukueleza katika maeneo matano wanakoishi watu wenye mri mrefu zaidia, wanatumia kiasi kinywaji hiki kwa siku," .

Kuhusu jambo hili, mwanasayasi Dokta Kristen Willeumier, anaeleza tofauti kupitia machapisho ya Well+Good kwmaba "Pombe mwanzoni inaonekana kama inaweza kutuliza, lakini ikikolea, inaweza kukuvuruga na kukufanya usilale usingizi mzuri."

4. Usile halafu ukaenda kulala

Image: GETTY IMAGES

Hii ni siri inayoelezeka lakini isiyokubalika zaidi na jamii ile inayoamini kwamba ni bora kushinda njaa kuliko kulala bila kula. Katika eneo la Okinawa, Japan, watu wake wanatajwa kutokula vyakula usiku na wale wanaokula wanakula mapema zaidi mpaka masaa 3 kabla ya kwenda kulala.

Na wanaokula chakula hicho cha jioni hula chakula kiduchu sana ambacho hakifikii ama kiasi cha robo ya chakula kinacholiwa mchana. "Chakula kinachocheza mwili kuruhusu insulin, ambazo zinafanya kazi kinzani na homoni ziazousaidia mwili kulala, melatonin.

Sasa kula sana ama kula wakati unakaribia kwenda kulala itaharibu mfumo wa uzalishaji wa melatonin mwilini na kufanya upate wakati mgumu wa kulala, ama usipate usingizi ama upate usingizi wa mang'amng'am," anaeleza mtaalama mwingine, Whitney English Tabaie, RDN.

5. Kula mkate uliotengenezwa na nafaka tupu

Image: GETTY IMAGES

Mikate ya nafaka tupu inakuwa na virutubisho na madini aina ya tryptophan na magnesium; yanayotajwa kusaidia kiwango cha serotonin mwilini ambacho ni silaha ya uzalishwaji wa melatonin ambacho hukusaidia kutokuwa na mihangaiko na kulala vyema.

Ingawa wapo watafiti wanaotazama tofauti, ila tafiti nyingine zinakubaliana wazi kwamba kula mapema, kidogo ama kutokula kabisa usiku wakati wa kulala kunasaidia ujenzi wa afya yako , unasaidia kuutuliza mwili wako na upumzike kwa viwango vinavyokubalika.

Dokta Kristen Willeumier anasema, inawezekana kuwa na umri mrefu, ukiwa na mwili usio na maradhi, usio na matatizo, unaopata muda mrefu wa kupumzika na haya yanawezekana kwa kupunguza sukari ya ziada, kunywa 'chai ya kijani', diai nyekundu, kula mkate wa nafaka tupu na usile halafu ukaenda kulala.