Fahamu sababu tano zinazosababisha ugumba kwa mwanaume na tiba yake

Muhtasari

•Wanaume wengi hunyamaza wakati wanapoanza kuathiriwa na tatizo la kushindwa kutekeleza wajibu wao katika ndoa ikiwemo tatizo la kushindwa kushiriki tendo la ndoa.

Fahamu sababu tano zinazosababisha ugumba miongoni mwa wanaume
Fahamu sababu tano zinazosababisha ugumba miongoni mwa wanaume
Image: REBECCA HENDIN / BBC THREE

Wanaume wengi hunyamaza wakati wanapoanza kuathiriwa na tatizo la kushindwa kutekeleza wajibu wao katika ndoa ikiwemo tatizo la kushindwa kushiriki tendo la ndoa.

Hivyobasi mara nyingi hulazimika kujiondolea lawama hiyo na badala yake kusema kwamba kizazi cha wake zao ndicho chenye tatizo.

Utafiti umeonesha kwamba wanaume wenye kati ya umri wa miaka 18 hadi 35 ni asilimia 15 ya idadi ya watu.

Vilevile wanaume wenye zaidi ya umri wa miaka 40 ni asilimia 40 ya wale wasioweza kuwatosheleza wake zao kindoa kutokana na tatizo linaloathiri sehemu zao za siri. (uume kushindwa).

Hali hiyo humfanya mwanaume kuhisi kukejeliwa na jamii ambayo hubeza hali hiyo.

Mwanaume au mwanamke aliye katika hali hiyo pia anaweza kukejeliwa au kupokea shutuma chungu nzima kutoka kwa jamii iwapo siri yake itajulikana nyumbani ama mahala popote pale.

Kutokana na hilo wanaume ambao hujipata katika hali hiyo ya kiafya hupendelea sana kutoshiriki katika mjadala kuhusu suala hilo kwasababu hujihisi kukatishwa tamaa.

Kunapotokea hali kama hiyo , magonjwa mengine pia huanza kumwathiri mwanaume kama huyo na mara nyingi huogopa kushiriki na wake zao katika tendo la ndoa.

Na iwapo mwanaume anashindwa kutekeleza wajibu wake nyumbani, humfanya mke wake kuanza kumshuku na hivyobasi kusababisha kuzuka kwa ugomvi wa mara kwa mara bila sababu.

Daktari Rasheed Adedapo Abassi, kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani ana uzoefu wa miaka 19 katika afya ya wanaume.

Anaelezea kile kinachosababisha mwanamke kushindwa kushika ujauzito ,tiba yake na jinsi ya kujilinda na hali hiyo.

Je ina maana gani mwanamume kushindwa kushiriki tendo la ndoa na mke wake?

Hali ya maumbile nyeti kushindwa kuwa tayari, kwa kitaalamu Erectile dysfunction (ED) ni wakati ambapo mwanamume hawezi kushiriki katika tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo.

Utafiti umeonesha kwamba iwapo mwanaume ana uwezo wa kushiriki katika tendo la ndoa, sehemu yake ya siri huonesha mihemko nyakati za alfajiri anapoamka.

Lakini daktari Abass anasema kwamba iwapo sehemu ya siri ya mwanaume haina mihemko, au iwapo hawezi kushiriki katika tendo la ndoa basi huenda yeye ana tatizo la ugumba.

Kuna sababu kadhaa kwanini hali hii huwakumba waathiriwa.

1.Ukosefu wa homoni za kiume za kutosha mwilini:

Testosterone ni homoni za kiume zinazowafanya wanaume kuhisi kuwa wanaume huku estrogen zikiwa homoni za kike ambazo humsaidia mwanamke kupata ujauzito .

Kama wanaume, viwango vya homoni za oestrogen katika mwili wa mwanamke hupungua wakati mwanamke anapofikisha umri wa miaka 50.

Wanaume wengi hunyamaza wakati wanapoanza kuathiriwa na tatizo la kushindwa kutekeleza wajibu wao katika ndoa ikiwemo tatizo la kushiriki katika tendo la ndoa
Wanaume wengi hunyamaza wakati wanapoanza kuathiriwa na tatizo la kushindwa kutekeleza wajibu wao katika ndoa ikiwemo tatizo la kushiriki katika tendo la ndoa
Image: BBC

Wanaume wengi hunyamaza wakati wanapoanza kuathiriwa na tatizo la kushindwa kutekeleza wajibu wao katika ndoa ikiwemo tatizo la kushiriki katika tendo la ndoa.

Kwa upande wa wanaume viwango vya homoni za kiume havipungui , lakini hukabiliwa na changamoto ambazo mara nyingi hupuuzwa.

2.Msongo wa mawazo:

Shinikizo la kiakili ni miongoni mwa sababu kuu zinazosababisha ugumba miongoni kwa wanaume. Msongo wa mawazo unaweza kutokea iwapo mwanaume hana kazi, iwapo mwanaume hana fedha ama iwapo kuna changamoto katika ndoa yake ama kutoka kokote kule.

Dalili hizi ni tofauti na zile za kufanya mazoezi , kwasababu mazoezi husaidia moyo kusukuma damu vyema katika misuli muhimu. Sonona husababishwa na mgando wa damu kila mahali mwilini.

3.Kushiriki mazoezi mbali na tendo la ndoa mara kwa mara:

Hili ni suala linalohitaji msisitizo ili kuzuia ugumba. Mtu anapaswa kujifunza kufanya mazoezi kwa muda mfupi kila siku.

''Je Unajua mazoezi ambayo huwashauri wagonjwa wangu kufanya? Ni kushiriki katika tendo la ndoa mara kwa mara.

Na kuna utafiti unaothibitisha hili, ambao naweza kusema kwamba ni ushahidi ulio sawa'', alisema Dkt Abbas.

4.Unyanyasaji wa kingono:

Dkt. Abass anawashauri wanaume kushiriki katika tendo la ndoa mara 21 kwa mwezi . Inadaiwa kwamba kushiriki katika tendo la ndoa mara kwa mara kunasaidia kuzuia saratani ya tezi dume.

5.Ukosefu wa maji safi

Suala hili linaonekana kama la kushangaza kwa watu wengi, kulingana na Dkt Abbas.

Hatahivyo , anaelezea kwamba ukosefu wa maji safi , ambayo hayana virutubisho , huathiri afya ya uzazi ya wanaume. Aliongezea kwamba serikali imelazimika kuhakikisha uwepo wa maji safi ya kunywa kwa kuweka dawa kama vile Fluoride, Calcium na Selenite.

Inahakikisha kwamba maji yana virutubisho vyote ili afya ya wanaume iwe bora