Hizi hapa sababu kwa nini wanaume wa Kenya hawaoi siku hizi

Muhtasari
  • Idadi ya wanaume wanaofunga ndoa nchini Kenya imepungua na hii pia inasababisha kupungua kwa idadi ya wanawake wanaoolewa
Image: GETTY IMAGES

Idadi ya wanaume wanaofunga ndoa nchini Kenya imepungua na hii pia inasababisha kupungua kwa idadi ya wanawake wanaoolewa.

Huku wanaume zaidi na zaidi wakikosa kazi na kukosa matarajio siku hizi, wanawake wengi sasa wanapendelea kuwa peke yao na kufanikiwa kuliko kuolewa na mwanamume ambaye haoni maisha yake ya kesho.

Kuna maandalizi mengi ya kiakili na kihemko ambayo huenda na ndoa. Usipowapata sawa, kuna uwezekano wa kupata ndoa yako sawa.

Kwa hivyo, ni vizuri kukumbuka kuwa ni muhimu, na ingeonekana kama jambo kubwa, sio jambo kuu au mafanikio makubwa.

Kwa hivyo hakuna maana kukimbilia ndoa; chukua muda wako, tathmini maisha yako, na hakikisha uko tayari kuingia ndani.

Kwa nini kuna vijana wengi hawatamani ndoa?

Labda wengine wangesema wanawake wanaahirisha au hata wanakataa ndoa siku hizi kwa kupendelea kazi yao. Lakini hiyo inaweza kuwa kweli jinsi gani?

Lakini sababu ni ipi ya wanaume ya kutooa siku hizi?

1.Talaka

Nikiwa kwenye zaiara yangu, nilipatana na kundi la wanaume ambao walikiri kwamba sababu yao kubwa ya kutooa ni kuoeana talaka na mkewe au kuachwa licha ya kuamua kuendelea na maisha yao.

Ndio watafunga ndoa lakinibaada ya muda mfupi wtapeana talaka na kuleta aibu kwa jamii.

2.Uzinzi

Baadhi ya wanandoa wamekuwa wakitoka nje ya ndo na kutafuta mipango ya kando sbaabu kuu ya kufanya hivyo ni kwa ajili ya tamaa.

3.Kuogopa majukumu

Kwa maana wamezoea tu kufanya kazi na kupata riziki yake peke yake, wanaume wengi wanaogopa kuoa kwa sababu hawataki kuongezewa majukumu.

Lakini kile hawajui ni kwamba wakati unayoyoma na hamna mtu ambaye atakungoja.

Katika sekta ya maoni ni sababu ipi nyingine wanaume hawataki kuoa siku hizi?