Baada ya raha, Karaha! Kwa nini wanaume wa Kenya wanaogopa kuwapa wanawake wao ujauzito

Muhtasari
  • Kwa nini wanaume wa Kenya wanaogopa kuwapa wanamke wao ujauzito
pregnancy.and.coffee
pregnancy.and.coffee

Wanaume wengi wanaogopa kuchukua jukumu la udhaifu wao hasa wakati wanapompa mwanamke ujauzito, na bila kujua kwamba wanaharibu uhusiano huo.

Kama mwanamume, unapaswa kujifunza kuchukua jukumu kamili kwa tabia yako mwenyewe.

Acha kumkelelesha kwa nini alipata mimba badala ya kumshtaki na kila mtu mwingine, simama na udhibiti.

Jifunze kuwa mtu na kuchukua jukumu. Usimshtaki kwa kupata ujauzito, huyo ni mtoto na sio mtu.

Haupaswi kufanya ngono ikiwa unafikiri huyko tayari kuwa baba. Unahitaji kuchukua umiliki wa matendo yako.

Nikiwa kwenye ziara yangu, nilipatana na wanaume kadhaa, na kuwauliza swali muhimu kwa nini wanaogopa kuwapa wake au wapenza wao mimba.

Na haya hapa baadhi ya majibu yao;

Dennis:Kwanaza safari ya mimba ni ndefu sana mke wako akiwa na ujauzito ni kama wewe pia una ujauzito, mimi kwanza naohopa bei ghali ya vitu, kama Pampers we hapo siwezani," Alijibu Dennis.

Onesmus: Bei ya mafuta ikipanda lazima kila kitu kipande, na mimi siko tayari kuwa na majuku mengine kama yangu mwenyewe yamenishinda, sitaki mtoto wangu aje duniani na aanze kuteseka.

Kevolution: One of the things that would give me HBP at this stage in life after loss of income is getting someone pregnant, like dude, sasa ni kuhama to a bigger house, relatives waanze trips sijui kwa kina nani, hiring househelp, korogoco nyingi mani ata huwezi pumua.

Emmanuel:Mimi ni baba wa mtoto mmoja, na sijuti mtoto wangu kuja duniani kwa sababu nimezoea majukumu, katika maisha ya hivi sasa huwezi subiri maisha yawe rahisi,lazima uzoee.

Je kulingana na maoni yako kwa nini wanaume wengi wanaogopa kuwapa wake na wapenzi wao ujauzito?