Mcheza kikapu: Unyanyasaji wa kingono umekuwepo kwa miaka mingi Kenya

Muhtasari
  • Mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu nchini Kenya anasema unyanyasaji wa kingono umekuwa 'ukiutesa mchezo wa kwa miaka mingi', lakini hofu inawazuia kujitokeza na kusema wazi
Image: BBC

Mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu nchini Kenya anasema unyanyasaji wa kingono umekuwa 'ukiutesa mchezo wa kwa miaka mingi', lakini hofu inawazuia kujitokeza na kusema wazi.

Akiwa na umri wa miaka 30 sasa, anasema amenyanyasanywa kingono na mmoja wa makocha wake wakati alipokuwa anaanza kucheza mchezo huo. Maelezo yake ameyatoa wakati huu ambao mchezo huo wa kikapu kwa wanawake ukimulikwa kufuatia taarifa iliyoripotiwa wiki iliyopita kuhusu masuala hayo ya unyanyasanyi wa kingono" uliokuweko kwa miongo kadhaa nchini Mali.

"Kila mahali Kenya wachezaji wa kikapu wanafahamu mambo haya, lakini watu wako kimya," anasema muathirika huyo, ambaye tumempa jina la Rachel kulinda utambulisho wake. Rachel ameiambia BBC kuwa "Wasichana wengi wamekuwa wakitumika lakini hawataki kusema." "Nimewaona wasichana wengi tu, hata kwenye timu kubwa hapa, lakini wote wako kimya. Nafikiri watu wanaogopa. Hapa Kenya watu wamekuwa wakitumika (kingono)."

Akizungumza bila kutaka kutambulishwa, Rachel alisema unyanyasajii huo mara nyingi hufanyika wakati mabinti hao wakipewa ahadi ya kusaidiwa kuendelezwa kwenye mchezo huo. Rachel alikuwa akizungumza kuhusu uelewa wake kwenye uchunguzi unaofanywa na Shirika la kimatafa la haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) juu ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono wanaofanyiwa wasichana kwenye mchezo wa kikapu Kenya.

Shirika hilo limesaidia pia wasichana wanaofanyiwa hivyo nchini Mali, ikionekana kwenye ripoti maalumu iliyowasilishwa na Fiba, wasichana hao wakieleza masaibu yanayowakuta. HRW sasa wamegeukiwa nchini Kenya.

"Human Rights Watch imeguswa na taarifa za kunyanyaswa kingono kwa wasichana wacheza kikapu chini ya Shirikisho la mchezo huo Kenya (KBF), " anasema Minky Worden kutoka HRW.

"Maafisa wanaosimamia mchezo wa mpira wa kikapu wana jukumu la kuwalinda wachezaji wanaochupukia, na kuhakikisha usalama wao. Shirikisho la kikapu ulimwenguni, Fiba, lina sera ya kutokomeza unyanyasaji wa kingono kwenye mchezo huo. "Ni wajibu wa Fiba na mashirikisho mengine kuhakikisha kuna mazingira salama kwa vijana kushiriki mchezo huo, kuhakikisha pia haki inatendeka kunapotokea vitendo hivyo na unyanyasaji mwingine wa kijinsia.

'Nahitaji kujiokoa mwenyewe'

Taarifa ya HRW inakuja mwezi mmoja baada ya hivi karibuni mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji ya KBF kusafishwa kutokana na makosa ya kujaribu kumnyanyasa kingono binti mchjeza kikapu mwenye umri wa miaka 22 jijini Nairobi.

Mwezi Julai, Philip Onyango - anatajwa kama mmoja wa makocha wenye mafanikio makubwa kwenye mchezo huo ambaye awali aliwahi kufundisha timu ya watoto ya Kenya - aliamu kuachia ngazi kwenye nafasi hiyo ili kupisha uchunguzi wa Polisi kuhusu tuhuma zilizotolewa na wanawake waliodai kunyanyaswa kingono.

Siku iliyofuata, KBF "ikamsimamisha [Onyango] kushiriki kwenye shughuli zote za mchezo huo" mara moja kutokana na uchunguzi wao wa awali walioufanya. Onyango, ambaye amekuwa akifnya kazi [pia kama muandishi wa habari wa taarifa za mchezo huo, amekana tuhuma hizo. Baadae Polisi walieleza kutohusika kwake kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha. Hata hivyo bado KBF haijamrejesha kwenye nafasi zake za awali.

Alipotafutwa na BBC, binti mwenye umri wa miaka 22 kueleza kuhusu uamuzi huo wa Polisi., alisema "Kesi imeisha kwa sababu hakuna ushahidi," alisema binti huyo. "Nimesikitishwa sana". Kesi hiyo iliwasilishwa baada ya rafiki wa karibu wa binti huyo kurekodi kwa siri mazungumzo yaliyomuhusisha kocha huyo ambayo baadae yaliibua tuhuma hizo. Sauti hiyo iliyorekodiwa sio tu ilitumwa KBF lakini pia ilitumwa kwa watu wengi wa mchezo huo.

Rachel anasema amesukumwa kujitokeza na kusema kutokana na matukio ya hivi karibuni, yanayorudisha kumbukumbu ya wakati unyanyasaji aliofanyiwa wakati akianza mchezo huo. "Kama kusema kutasaidia kuondoa haya kwenye mchezo huu, kwa nini nisiseme?" alifafanua. "Nahitaji kuokoa wengine, nahitaji kujiokoa na mie pia. Kwa kufanya hivi ni kama sehemu ya kushusha mzigo na kupumua."

Anasema hakuripoti wakati huo kwa sababu alifikiri wasingemuamini, akieleza pia wengine walishindwa kwa sababu walikuwa wanahofia kupoteza nafasi kwenye timu zao.

BBC imepokea ushahidi kutoka kwa wanawake wengine watatu ambao wanasema wamekuwa wakinyanyaswa kingono ama walipitia majaribu ya kunyanyaswa kingono wakati wakiwa mabinti wadogo. "Tulikuwa mabinti wadogo kiasi hata kujieleza ilikuwa shida - hakuna ambaye angetusikiliza wakati huo. wangefikiri tu tunadanganya," alisema mmoja.

'Acha unyanyasaji wa kingono'

Wakati huo huo Polisi walikuwa wanaendelea na uchunguzi wao kuhusu kampeni iliyoitwa "Acha unyanyasaji wa kingono" nchini Kenya uliosambaa sana mitandaoni huku KBF ikitupiwa lawama kwa 'kuifumbia macho'. Zaidi ya saini 2,000 zilikusanywa kuhusu kampeni hiyo.

Mwezi Julai, serikali ya Kenya iliunda kamati maalumu kuhusu masualawalioathirika kutoa kuripoti matukio ya unyanyasaji kwa kamati hiyo" ambayo ripoti yake haijawekwa wazi mpaka sasa.

Waliothirika wapewe msaada

Nahodha wa timu ya taifa ya kikapu ya Kenya anasema anaunga mkono hatua zote hizo.

"Ni suala nyeti sana, ni wakati sasa wa kufanyiwa kazi," anasema Rose Ouma, ambaye anaiambia BBC kwa upande wake hajaathirika na matukio hayo.

Kwa kuwa sasa jambo hili limewekwa wazi, inamaanisha mabinti na sie wanawake, tutaanza kuangaliwa. "Isiwe tu kwenye michezo, iwe kwenye jamii nzima, kwa hivyo ni wakati sasa wa kulishughulikia. Mabinti walioathirika wanahitaji msaada wa kisaikolojia, kimwili na kihisia." "Kwa wote ambao wameathirika, tunahitaji wajitokeze ili tujue ni eneo gani sio salama, ili tujihadhari."

Jumatano hii, Kenya iliondolewa kwenye mashindano yanayoendelea ya mchezo wa kikapu kwa wanawake Afrika huko Cameroon.

Nchini Mali, maafisa saba wa shirikisho la mchezo wa kikapu nchini humo wametimuliwa na shirikisho la mchezo huo Ulimwenguni Fiba kufuatia ripoti ya unyanyasaji wa kingono wiki iliyopita.

Ripoti ya uchunguzi huo ilibaini kwamba, Shirikisho hilo limekuwa likificha vitendo vya unyanyasaji wa kingono vinavyofanywa na maafisa wake, huku kocha wa zamani wa timu ya taifa ya vijana wa kike, Amadou Bamba, akiwa jela sasa akisuburi kushitakiwa , tuhuma ambazo amezikana.

Ripoti hiyo iliyojumuisha mashahidi 31, huku wengine 22, wakigoma kuzungumza, imemsafisha rais wa Fiba, Hamane Niang aliyekuwa akipuuza unyanyasaji huo wakati alipokuwa kiongozi wa Shirikisho la kikapu Mali kutoka 1999 hadi 2007.