Fahamu ni kwa nini umbeya wa kazini ni bora kwako

Muhtasari

•Huku baadhi ya usengenyaji unaweza kuwa wa kipuuzi na kutokuwa wa kitaaluma, aina nyingine ya usengenyaji unaweza kufurahisha, wa kawaida, na hata wa kutusaidia kiafya na katika uzalishaji.

Image: GETTY IMAGES

Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kuyakosa kuhusu kuhusu kufanya kazi ofisini: Kahawa ya bure, kiyoyozi cha bure, sababu ya kuvaa nguo nyingine nzuri badala ya kuvaa nguo za kawaida tunazovaa nyumbani.

Lakini kitu ambacho tutakikosa zaidi ni watu wengine-na mazungumzo nao.

Hususan, mazungumzo kama vile -jinsi mwenza wa Mike alivyopata mtoto mchanga mwingine tu hivi karibuni , Jinsi friji ilivyojaa vyakula vya milo ya mchana vya Jane vilivyokaa kwa muda mrefu, kwamba dawati la teknolojia ya IT linavyozorota kutoa huduma na jinsi bosi alivyomuongezea mshahara Mark na sio Jean.

Kwa maneno mengine tutakosa : Umbeya

Huku baadhi ya usengenyaji unaweza kuwa wa kipuuzi na kutokuwa wa kitaaluma, aina nyingine ya usengenyaji unaweza kufurahisha, wa kawaida, na hata wa kutusaidia kiafya na katika uzalishaji.

Wataalamu wanasema kwamba kuwateta watu bila wao kukusikia haipaswi kuwa jambo la kupoteza muda ofisini- inaweza kuwa njia ya maana inayoweza kumsaidia mfanyakazi kuelewa mazingira ya kazi na kufahamu taarifa muhimu.

"Ninadhani kwa ujumla, umbeya ni kitu kizuri," anasema Elena Martinescu, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Vrije cha Amsterdam, ambaye alichunguza kwa kina saikolojia ya masengenyo.

"Kulingana na nadharia ya mageuzi, binadamu waliendeleza taarifa za masengenyo ili kuwezesha ushirikiano katika kikundi."

Kupitia mazungumzo kuwahusu watu wengine, tunaweza kujifunza, ni nani wa kushirikiana naye, na ni nani wa kumuepuka.

kitu ambacho husaidia kikundi cha watu kufanya kazi vyema zaidi kwa pamoja. Tabia hii ya mtu hufasili kwenye kazi za kisasa, anasema , "ambapo ni muhimu kumfahamu ni mfanyakazi gani mwenzako unayeweza kumuamini na ni yupi unayefaa kuwa mwangalifu kwake.

Baadhi ya masengenyo yanaweza kuwa ya kufurahisha, ya kawaida, na ya faida kiafya...na hata kutusaidia kiutendaji
Baadhi ya masengenyo yanaweza kuwa ya kufurahisha, ya kawaida, na ya faida kiafya...na hata kutusaidia kiutendaji
Image: GETTY IMAGES

Profesa wa masuala ya utawala Matthew Feinberg, katika Chuo Kikuu cha Toronto, ambaye pia alifanya utafiti kuhusu masengenyo, anasema kwamba kuna aina tofauti za masengenyo.

"Wakati masengenyo yanapokuwa tu ni 'mazungumzo machafu'- kuzungumza kuhusu muonekano wa mtu fulani kwa mfaho hilo halina lengo chanya, kwahiyo hilo ni hasi, inaharibu na linakuwa tatizo."

Lakini utafiti unaonesha kuwa masengenyo kwa kiasi kikubwa huwa sio ya kusababisha madhara.

Utafiti wa mwaka 2019 , kwa mfano , ulionesha kuwa wakati watafiti waliporekodi mazungumzo ya washiriki wapatao 500 , wengi wao - zaidi ya robo tatu ya mazungumzo hayakuwa chanya au hasi, bali yalikuwa ya kawaida.

Inaweza kuwa mazungumzo yanayosafiri kupitia masengenyo, lakini 'Nilisikia binti yake Mary anafanya vizuri katika masoko' au 'Pete yuko mapumzikoni katika Cornwall'.

Kwahiyo hata kama uchunguzi huo ulionyesha kwamba tuna uvumi sana - kwa wastani wa dakika 52 kwa siku, na ukweli ni kwamba - maudhui kwa kiasi kikubwa hayakuwa mabaya kama tulivyotarajiwa.

Tunaongea masengenyo mengi-kwa wastani wa dakika 52 kwa siku-lakini maudhui kwa kiasi kikubwa sio mbaya kama tulivyotarajiwa

"Kwa kumuuliza mfanyakazi mwingine, 'Unaweza kuamini Mfanyakazi X amechukua siku nyingi za mapumziko ya ugonjwa?', mfanyakazi msengenyaji anajaribu kuhukumu au kutathmini ibu kutoka kwa yule anayemwambia iwapo tabia ya Xinakubalika au la ," anasema Taylor.

Mabadiliko ya tabia

Umbeya sio tu kwa ajili ya kukusanya taarifa, hatahivyo. Kusikiliza masengenyo kuwahusu wafanyakazi wenzetu kunaweza kutufanya tujichunguze zaidi, wakati tunapohusishwa na masengenyo na inaweza kuwafanya watu wabadili tabia.

Katika utafiti wa mwaka 2014 , Martinescu na wenzake waliwataka washiriki kujibu maswali kuhusu matukio ambayo yalihusisha kusikia masengenyo hasi hasi na ya mzaha kwa pamoja kuwahusu watu wengine.

Watafiti walibaini kwamba huku masenegnyo hasi yaliwafanya wasikilizaji wajihisi bora zaidi ya mtu aliyekuwa akisengenywa, na hivyo kujithamini, uvumi huu ulimfanya msikilizaji kujihisi zaidi kuwa anaweza kuwa katika hali sawa na yule aliyesengenywa.

Wakati huo huo kusikiliza masengenyo ya kusifiwa kwa mtu kuliwapa wasilikizaji mawazo kuhusu jinsi ya kujiboresha, ili waweze kuwa sawa na mtu aliyekuwa akisengenywa.

"Ninadhani dhana kubwa zaidi potofu ni kwamba usengenyaji kila mara huwa kila mara unakuwa ni hasi-kuzungumza vibaya kumuhusu mtu fulani wakati hayupo.

Lakini tafiti zinaonyesha kuwa sababu ya msingi inayowafanya watu kumzungumzia mtu mwingine huwa ni kwasababu wanataka tu kuyaelewa mazingira yao ," anasema Shannon Taylor, profesa wa utawala katika Chuo Kikuu cha Kati cha Florida, Marekani, ambaye anasomea mienendo ya mazingira ya kazi.

Masengenyo yanaweza "kuthibitisha hisia zetu" na kutusaidia kutambua msimamo wa watu wengine kuhusu mambo, anasema , na kwamba usengenyaji hutusaidia kuhakikisha iwapo "mtazamo wetu wa kidunia ni sawa na wa wenzetu pamoja na wafanyakazi wenzetu.

Kusema ukweli ni kuhusu ukusanyaji wa taarifa." Kwahiyo, kama mtu fulani kazini anasema kitu fulani kama "Ralph amekuwa akichukua mapumziko ya ugonjwa hivi karibuni," inaweza kufungua njia kwa wengine kushirikishana mitazamo yao na tatmini- kwamba labda mapumziko ya mara kwa mara ya ugonjwa anayoyaomba Ralph yanaweza kuchangia utendaji duni wa kazi yake, kwa mfano.

Inaweza pia kusaidia kuangalia ni kwa kiasi gani mapumziko ya kazi yanaonekanakama "yanayofaa" miongoni mwa wafanyakazi (bila kujali sera rasmi) pamoja na kufahamu ni nanimweye huruma au asiyemuhurumia Ralph.

Bila mazungumzo karibu na chupa za maji baridi , tumepata njia za kuhamisha masengenyo yetu kwenye mitandao kwani tumekuwa hatuzungumzi ana kwa ana
Bila mazungumzo karibu na chupa za maji baridi , tumepata njia za kuhamisha masengenyo yetu kwenye mitandao kwani tumekuwa hatuzungumzi ana kwa ana
Image: GETTY IMAGES

Huchochewa na kutokuwa na uhakika

Masengenyo- Makala ya 2017 yanayoitwa "an essential part of any working process" (sehemu muhimu ya mchakato wowote wa kazi) - huenda ikafaa zaidi sasa kama njia ya kujitetea ambayo tumekuwa tukiitumia sasan katika kukabiliana na wasiwasi wakati wa janga la corona.

Ingawa hatukusanyiki kimwili karibu ya chupa za maji maofisini kusengenya kuhusu kashfa tulizozisikia baina yetu, jumbe za moja kwa moja hutumiwa kama njia mbadala ya kuwasiliana kikazi.

"Masengenyo husababishwa na kutokuwa na uhakika wa mambo," anasema Taylor.

"Sitashangaa kabisa kama tunashuhudia viwango vya juu vya usengenyaji katika maneo ya kazi zaidi ya ilivyokuwa kabla ya Covid. Kwa hali hii yote ya watu kutokuwa na uhakika wa mambo, tunajaribu kufahamu ni nini watu wengine wanafikiria na ni nini watu wengine wanachokifanya ."

Hiyo inamaanisha kwamba sasa hivi, usengenyaji unaweza kuwa ni kuhusu kutaka kujua iwapo wenzako wanatafuta kazi nyingine ambayo itawawezesha kupata muda zaidi wa kufanyia kazi nyumbani, au kutaka ku linganisha hali yako na wazazi wenzako wakati huu wa janga -na enzi ya mzozo wa malezi ya watoto.

Kwa kufanya hivi, unajaribu kuelewa, ni taarifa gani zilizopo katika hali zinzaobadilika kwa haraka na pia ni nani ana hali kama yako.

Wakati mwingine, masengenyo huwa ni kuhusu mambo yasiyofaa kuwahusu watu ay mifumo usiyoipenda .

Labda ni kuhusu mkubwa wa kazi jeuri anayeongoza kwa mkono wa chuma , au wafanyakazi wanaofanya kazi kwa uzembe . Bado uvumi huu unaweza kusaidia kutoa mtandao wa uchunguzi na maonyo njia isiyo rasmi ya hutoa usaidizi nje ya mifumo ya kawaida ya kazi kama vile idara za huduma kwa wafanyakazi (HR)

"Usengenyaji unaweza kuwaonya watu kuhusu watu wengine hatari, na pia husaidia kujenga uhusiano wa kijamii baina ya watu wanaoongeza uvumi ," anasema Martinescu. " Baada ya muda, uvumi unaweza kuwasaidia watu kutambua kuwa wanashirikishana maadili na uzoefu, jambo linaloweza kuwaleta karibu zaidi ."

Ikizingatiwa kwamba usengenyaji umekuwepo kwa muda mrefu kabla ya janga, uliendelea wakati wa janga na utaendelea kuwepo baada ya janga , hatupaswi kujihisi vibaya sana juu ya haja yetu ya kujadili kuhusu maisha ya watu wengine. Kufanya hivyo kunaweza kunusuru malengo hasi ili mradi masengenyo sio ya nia mbaya.