Fahamu kwanini watu katika nchi hizi 5 huishi miaka mingi zaidi kuliko nchi zingine duniani

Muhtasari

•Hadithi za kwa kwamba maji ya chemichemi huchelewesha kifo hazijawahi kuthibitishwa, lakini kuna nchi katika sayari yetu ambapo watu wake wanaonekana kuishi miaka mingi kuliko maeneo mengine ya dunia

ISTOK

Tangu nyakati za Herodotus, na labda hata mapema zaidi, binadamu hakupenda uzee na kutokana na hilo binadamu amekuwa akitafuta mbinu mbalimbali za kumfanya aendelee kuwa kijana daima.

Hadithi za kwa kwamba maji ya chemichemi huchelewesha kifo hazijawahi kuthibitishwa, lakini kuna nchi katika sayari yetu ambapo watu wake wanaonekana kuishi miaka mingi kuliko maeneo mengine ya dunia.

Hizi ni nchi ambako, watu wake huishi kwa zaidi ya wastani miaka 71.

Tulijaribu kubaini siri ya maisha marefu katika nchi tano ambazo ziliwekwa katika nafasi za kwanza mwaka 2017 katika ripoti ya Siku ya dunia ya furaha iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa , na kuzungumza na wakazi wa nchi hizo.

Kwa wastani, mtu wa Japan huishi miaka 83- hivi ni viwango vya wastani wa juu zaidi duniani
Kwa wastani, mtu wa Japan huishi miaka 83- hivi ni viwango vya wastani wa juu zaidi duniani
Image: WIBOWO RUSLI/GETTY IMAGES

JAPAN

Kwa wastani, Wajapan huishi miaka 83- Japan imekuwa miongoni mwa nchi zenye matarajio ya juu zaidi ya maisha marefu ya watu.

Katika kisiwa cha Okinawa, ambacho mara nyingi huitwa kisiwa cha wasiokufa, tafiti za kimataifa hali hiyo zinaendelea - zaidi ya watu 400 huishi hapo, ambao umri wao umepita miaka mia moja.

Wanasayansi huwa wnaeleza kwamba hii inatokana na jinsi wenyeji wanavyokula : Wanakula tofu kwa wingi (bidhaa yenye protini nyingi itokanayo na soya ) pamoja na viazi vitamu, na samaki wachache. Zaidi ya hayo mazungumzo baina wazee na maisha ya kuishi pamoja huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuishi maisha ya raha yasiyo na msongo wa mawazo.

Ili kuishi vyema maisha ya aina hiyo, unahitaji kujifunza Kijapan, anasema Daniele Gatti, ambaye ameishi katika ardhi ya Jua linalochomoza.

"Ubora wa maisha nchini Japan ni wa hali ya juu kwa kiwango kisicho cha kawaida, lakini kama utaweza kukabili pingamizi la lugha- vinginevyo hautaweza kufahamu mawazo ya wenyeji, ambayo yanatofautiana na yale ya kimagharibi na maeneo mengine ya dunia kuliko unavyoweza kufikiria ," aliongeza.

"Wale wanaoamua kuhamia hapa wanapaswa kufikiria sana iwapo wanaweza kupata muda wa kutosha na juhudi za kujifunza lugha. Hii ni muhimu sana kwa ajili ya maingiliano ya kina na jamii za wenyeji, ili kuishi maisha kamili ya watu wa hapa."

Wazee katika jamii ya Wajapan huishi maisha ya kufanya kazi na hula mlo wa afya
Wazee katika jamii ya Wajapan huishi maisha ya kufanya kazi na hula mlo wa afya
Image: ISTOK

UHISPANIA

Mlo wa Mediterranean uliojaa Mafuta yanayoboresha afya ya moyo ya mizeituni, mboga na mvinyo ni mojawapo ya sababu za kuishikwa umri mrefu miongoni mwa Wahispania, ambao wastani wa matarajio yao ya kuishi ni miaka 82.8. Hatahivyo, kuna siri zaidi - siesta( kujilaza mchana)

"Watu hudhani kuwa Wahispania wanakwenda katika la siesta , kwasababu maduka yote hufungwa kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na moja jioni. Lakini ukweli ni kwamba kila kitu kimepangwa hapa ," anasema Mikel ngel Diez na Besora kutoka Barcelona.

"Wakati unapokuwa na nusu dakika tu kula chakula, huwa unakula mkate wa haraka haraka wa kununua. Lakini iwapo unajua kuwa una saa mbili au tatu za kupumzika, unaweza kwenda nyumbani ay kwenye mgahawa- ambako utaketi chini na kutulia na kuwa na mlo kamili. Halafu unakuwa na muda wa chakula chako kumeng'enywa mwilini vyema- jambo ambalo ni la kiafya zaidi kuliko kula kitafunio na kwenda tena kazini. "

Miji ya Uhispania imeundwa kwa kuzingatia kutembea kwa miguu zaidi ya kuendesha magari, kwahiyo watu hutembea kwenda madukani na kwenye migahawa.

"Nilipohama kutoka Moscow kuja Barcelona, niligundua mara moja kuwa watu hapa wanapenda kutembea au kuendesha baiskeli-au kutembea umbali fulani kwanza ndio watumie usafiri wa umma , lakini sio kutumia gari," anasema Marina Manasyan. "Matokeo yake, unapata hapa kuna hewa safi ya oksijeni na na hewa chafu inakuwa kidogo. "

Image: CHANZO CHA PICHA,JEREMY HORNER/GETTY IMAGES

SINGAPORE

Mfumo wa afya wa Singapore, unamuwezesha kila mkazi kupata huduma za afya. Sio jambo la kushangaza kwamba wastani wa matarajio ya muda kuishi wa watu wa nchi hii ni - miaka 83.1.

Nchi hiyo ina viwango vya chini vya vifo vya wanawake wakati wa kujifungua kuliko nchi nyingine yoyote ile duniani , na imejikita katika hatua za kuzuwia badala ya kutibu magonjwa.

Utamaduni wan chi hiyo na mazingira yake pia vinachangia maisha marefu. "Utaona jinsi watu wengi wanavyokwenda katika klabu za kujenga mwili na kufanya mazoezi katika bustani, ambapo kuna watu wanaofanya mazoezi," anasema Bino Chua, mwanablogi mwenye makao yake nchini Singapore.

Bustani ya mazoezi ya wakongwe zaidi wa Singapore inayoitwa 'first seniors' therapy park hivi karibuni ili kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha afya ya akili kwa wazee.

Pia ni muhimu kusema kuwa katika Singapore ni vigumu sana kuzowea tabia mbaya.

" Wale wanaotaka kuhamia hapa wanapaswa kujua kuwa ushuru wa sigara na vileo ni wa juu sana, kwahiyo bidhaa hizi ni ghali zaidi kuliko nchi nyingine," alionya Bino Chua.

Image: GETTY IMAGES

USWISS

Katika nchi ya Uswiss, wanaume huishi miaka mingi kuliko nchi nyingine yoyote duniani, ikiwa na wastani wa miaka 81 ya kuishi.Ikiwa ni moja ya nchi tajiri zaidi dunaini barani Ulaya hutoa hakikisho kwa wakazi wake la huduma za hali ya juu za afya, kiwango ch ajuu cha usalama wa mtu binafsi na maisha bora.

Baadhi ya tafiti hata zimeonyesha kuwa maisha marefu nchini Uswiss yanaweza kuhusishwa na ulaji mkubwa wa jibini na bidhaa nyingine zitokanazo na maziwa.

Ingawa Waswiss ni wachapakazi sana na kazi ni muhimu sana, kila upande wan chi unazingatia haki ya watu ya kupata kufanya kazi na kucheza.

Katika siku za wikendi, ni kawaida kwa wakazi wa nchi hiyo kwenda kutembea katika maeneo mengine ya bara la Ulaya kwa muda mfupi katika maeneo yenye hali ya hewa safi, kwasababu mabonde ya Alps yapo karibu ," anakumbuka Daniele Gatti, aliyeishi Uswis kabla ya Japan

Shule za kibinafsi pale ni "bora duniani ," aliongeza.

Waswiss hufanya kazi sana, lakini kwasababu wako karibu na milima ya Alps ni rahisi kutembea huko kwa muda katika maeneo asilia
Waswiss hufanya kazi sana, lakini kwasababu wako karibu na milima ya Alps ni rahisi kutembea huko kwa muda katika maeneo asilia
Image: FRANK BIENEWALD/GETTY IMAGES

KOREA KUSINI

Korea Kusini inaweza kuwa nchi ya kwanza duniani kufikia wastani wa miaka 90 wa matarajio ya kuishi ya watu wake , kulingana na utafiti wa hivi karibuni. Sababu ni ipi? Uchumi imara na unaokua, upatikanaji wa huduma za afya kwa raia wake wengi na ... viwango vya chini vya shinikizo la damu ikilinganishwa na nchi nyingine duniani

Mlo wa Wakorea huwa umejaa vyakula vilivyochachishwa ambavyo vinaaminiwa kushusha viwango vya Mafuta mwilini, na kuongeza kinga ya mwili, na kuzuwia saratani mbali mbali.

"Kwa ujumla, chakula cha Wakorea kina wanga mwingi utokanao na mime ana chenye virutubisho vya hali ya juu ,"anasema Camilla Hoheb, muasisi na mwenyekiti wa taasisi ya utalii wa maisha bora duniani.

Heshima kwa wazee, kipaumbele kwa umma badala ya mtu binafsi na mahusiano imara ya kijamii huwawezesha Wakorea kuimarisha viwango vya juu vya maisha bora.

"Mtindo wa kitamaduni wa kuoga pamoja hadharani ni eneo la kuchangamana na kuongoa msongo wa mawazo, na kupona ," anasema Hoheb