Je ni nadharia tu au ni kweli wapenzi wanaweza kunata wakati wa tendo la ndoa?

Muhtasari

•Tukio la Kenya la mwaka 2012 ilitokea baada ya madai kwamba mume wa mwanamke huyo kwenda kwa mganga na iliripotiwa kuwa watu hao waliweza kutengana baada ya kufanyika kwa maombi - na baada ya mtu aliyefumaniwa kuiba mke wa mwenzie kuahidi kumlipa mume shilingi za Kenya 20,000 sawa na dola $200.

•Uume wa mbwa una sehemu maalumu ambayo hujaa damu mara tu anapoanza kujamiiana, na hilo huufanya kung'ang'ania ukeni

Picha ya watu wanaoshiriki katika tedno la ndoa
Picha ya watu wanaoshiriki katika tedno la ndoa
Image: MALAYALAMEMAGAZINE.COM

Inaonekana ni kipande kisichofaa cha filamu ya mapenzi . Lakini taarifa kuhusu 'kunatana' wakati wa tendo la ndoa ni jambo lililopo kwa karne na karne - huenda zingine kukawa na ukweli.

Safari ya kukimbizwa hospitali kwa dharura kamwe halijawahi kuwa jambo zuri, lakini pia siku kitu ambacho ungetamani kitokee hasa baada ya kushiriki mapenzi.

"Sio mwisho mzuri wa kuburudisha kwa wapenzi," anasema daktari Aristomenis Exadaktylos, kutoka hospitali ya Bern, Switzerland.

Ni mmoja wa waandishi wa andiko la utafiti linaloitwa '11 years of admissions' katika hospitali hiyo. Yeye na waandishi wenzie wamekutana na wagonjwa wengi ambao wamepitia matatizo mbalimbali baada ya kutoka kushiriki mapenzi ama tendo la ndoa. Mfano matatizo yanayofahamika kitaalamu kama 'migraines', amnesia' na matatizo ya moyo.

Lakini alipoulizwa na kipindi cha Radio cha masuala ya afya cha BBC kama amewahi kukutana na kesi ya uke na umme kung'ang'aniana, alisema '"Hapana" -na kuongeza pengine hiyo ni dhana potofutu.

Hata hivyo wasikilizaji wawili walitoa maoni yao kumpinga.

"Lazima nikuambie, hiyo sio dhana potofu," aliandika mwanamke mmoja ambaye aliomba kutotajwa jina. "Iliwahi siku moja kutukuta mie na marehemu mume wangu. Hakuweza kuutoa uume wake kwangu, tulikuwa tumeng'ang'aniana. Nalihusisha hilo na namna misuli ya uke inavyokuwa wakati wa kufikia kilele."

Nchini Kenya watu walikongamana katika eneo moja baada ya habari kwamba wapenzi walikuwa wamekwama wakati wa tendo la ndoa
Nchini Kenya watu walikongamana katika eneo moja baada ya habari kwamba wapenzi walikuwa wamekwama wakati wa tendo la ndoa
Image: HISANI

Msikilizaji mwingine ambaye alitaka aitwe John ingawa si jina lake halisi, alikua karibu na uwanja wa ndege kusini mwa England. "Nakumbuka kusikia taarifa za aina hii nikiwa na miaka 14 au 15 kuhusu rubani mmoja Mmarekani ambaye alinata kwa mwanamke na kukimbizwa Hospitali kwa gari ya wagonjwa wa dharura ili kuwatenganisha," Anasema John, anakumbuka yaliyomtokea akiwa na mpenzi wake Mjapan.

Anasema wakati wakishiriki mapenzi ghafla akajikuta hawezi kuutoa uume wake. Anakumbukuka ilichukua dakika mbili au tatu katika hali hiyo huku wakicheka kwa utani na mpenzie - anasema zoezi hilo halikua la maumivu kwake wala kwa mwenzake.

John, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 75, hakuwahi kuzungumza jambo hili popote na anasema halikuwahi kujirudia.

Daktari John Dean, wa Uingereza anasema matukio yote haya yanaonyesha kwamba ni jambo la nadra sana linaloitwa na madaktari kitaalamu kama "penis captivus".

"Wakati uume uko ndani ya uke, unazidi kutanuka," anasema akieleza mtazamo wake kuhusu chanzo cha tatizo hilo.

"Misuli ya uke wa mwanamke nayo hufuata mirindimo hiyo wakati wa kufikia kileleni ama mshindo. Misuli hii inapokutana na uume inag'andana na kuendelea kutanua."

Mwishowe misuli ya uke inaporudi kawaida , damu inatembea kawaida na ni wakati huo ambapo mwanaume anaweza kuutoa uume wake.

Wamiliki wengi wa mbwa wamewahi kuona mbwa wakigandana wakati wa kujamiina. Hata hivyo, kuna utofauti wa hali hiyo kwa binadamu kwa mujbiu wa Peggy Root, mtaalam wa wanyama kutoka chuo kikuu cha Minnesota.

Uume wa mbwa una sehemu maalumu ambayo hujaa damu mara tu anapoanza kujamiiana, na hilo huufanya kung'ang'ania ukeni

Dakatari Dean anasema kwa miaka mingi baadhi ya wagonjwa wake wamekuwa wakijadiliana naye kuhusu uzoefu wake wa mwanaume na mwanamke kugandana ama kung'ang'anianana wakati wa kufanya mapenzi, wengi wanadadisi kwa kuwa lilikuwa tatizo kubwa.

Kumekuwa na matukio ya kudhalilisha yakiendelea kuhusu haya. Vyombo vya habari vimeripoti kuhusu hali hii 'penis captivus' katika nchi za Kenya, Malawi, Zimbabwe na Philippines - vyote vikihusisha uzinzi wa watu wazima.

Mchoro wa watu waliokwama wakati wa tendo la ndoa
Mchoro wa watu waliokwama wakati wa tendo la ndoa
Image: HISANI

Kipande cha Video cha YouTube kikionyesha umati wa watu ukikusanyija katika jiji la Nairobi, ambapo wapenzi wakiripotiwa kung'ang'aniana au kunatana.

Tukio la Kenya la mwaka 2012 ilitokea baada ya madai kwamba mume wa mwanamke huyo kwenda kwa mganga. Iliripotiwa kuwa watu hao waliweza kutengana baada ya kufanyika kwa maombi - na baada ya mtu aliyefumaniwa kuiba mke wa mwenzie kuahidi kumlipa mume shilingi za Kenya 20,000 sawa na dola $200.

Mtu huyo alipigwa picha akionekana kwenda kutoa fedha kwenye mashine ya fedha ya ATM.

Vyombo vya habari vya Zimbabwe viliripoti kwamba mwanamke mmoja alipeleka kesi mahakamani dhidi ya mpenzi wake wa zamani kwa kumuwekea alichokiita "runyoka" - na kumsababishia kung'ang'ania au kunatana na mpenzie wa sasa.

Alitaka mpenzi wake huyo wa zamani amlipe fidia kutokana na "kumdhalilisha na kujaribu kuingilia na kumdhibiti jinsi anavyopaswa kutumia sehemu zake za siri."

Zipo taarifa zingine kwamba 'penis captivus' ama kunatana kwa wapenzi kunaweza kutokea kwa hata wale walio katika ndoa ikiwemo matukio yaliyowahi kuripotiwa huko nyuma kwenye karne ya 19 na wataalamu wa uzazi kwa wanawake.

Daktari John Dean anasema hawezi kufafanua zaidi kuhusu "jambo hili lisilo kawaida", tangu watu wakutane na tatizo hili kwa ujumla wamekuwa wakipata shida ya sekunde chache tu ya kutengana kutoka kwenye kung'ang'aniana.

Lakini akaongeza: "Kama uko kwenye hali hiyo, unaweza kuhisi kwamba ni jambo la milele."