Kwa nini inashauriwa kutomeza Paracetamol kuondoa uchovu wa pombe

Muhtasari
  • Hali ya uchovu wa baada ya kunywa pombe( hangover) kwa wengi wenu, huenda ukawa ni ugonjwa wa kawaida baada ya sherehe za usiku
Image: BBC

Hali ya uchovu wa baada ya kunywa pombe( hangover) kwa wengi wenu, huenda ukawa ni ugonjwa wa kawaida baada ya sherehe za usiku.

Hatahivyo, si kila mtu hupata uchovu asubuhi baada ya unywaji wa pombe. Jibu linategemea na mtu binafsi , mazingira au mambo ya muda.

Yote kwa pamoja yanaweza kukuathiri wakati mtu anapopata hisia za udhaifu (na wakati mwingine kujuta kwa kutoepuka kunywa pombe) au iwapo ni ya kiwango kikubwa au cha chini.

Sababu ya udhaifu baada ya kunywa pombe iko wapi ?

Kama tukifanya utafiti wa kisayansi, dalili za uchovu wa baada ya kunywa pombe zimekuwa zikijaribu kupewa sababu za kuuhalalisha. Sababu ya kwanza ni upungufu wa maji mwilini.

Lakini pia husababishwa na kuondolewa kwa endogenous (yaani vitu vinavyotengenezwa katika seli za mwili) kama vile aina ya sukari ya glucose na baadhi ya homoni. Hii inaweza kutokea kutokana na kutomeng'enywa kwa kiasi kikubwa cha vilevi, jambo ambalo linasababisha mikusanyiko ethanoli na kuyeyuka kwa bidhaa zake katika damu .

Hatahivyo, haikuwa wazi kwamba usumbufu unaoambatana na hali anayoipata mtu baada ya kunywa kilevi kupindukia hutokana na hali hii na asili yake bado inachunguzwa.

Hivi ndivyo vileo vinavyoteremka katika mwili wako

Wakati tunapokunywa kinyaji cha kilevi, ethanol unayokuwa nayo huingia haraka sana katika mfumo wa utumbo na baadaye kufikia ini. Kiungo hiki kinahusika katika mchakato huo kupitia kimeng'enyo dehydrogenase (ADH).

Zaidi ya hayo mmeng'enyo unaweza kusababisha majeraha na hivyo kusababisha maini kuwa na mafuta, ambayo ni hatua ya kwanza ya kuugua kwa ugonjwa wa ini unaosababishwa na matumizi makubwa ya vilevi.

Baada ya kufahamu madhara ya matumizi makubwa ya vilevi, ngoja tuone matibabu yanayotumiwa zaidi kukabiliana na unywaji mbaya wa vilevi na jinsi unavyosababisha madhara zaidi kuliko kuwa na faida.

Kama tayari umeishawahi kupitia hatua hizi uliishia kunywa paracetamol au ibuprofen ukitumaini kupata matokeo ya ajabu ya kuzuia maumivu . Lakini je unafahamu jinsi dawa hizi zinavyofanya kazi?

Kwanza kabisa, paracetamol ni dawa inayosaidia kupunguza maumivu, ina ufansi sana katika kudhibiti homa au kuponya maumivu. Ni mojawapo ya dawa ambazo huchaguliwa na wengi kuondokana na maumivu.

Hatahivyo, dawa hizi hazina uwezo wa kuponya majeraha, kwahiyo kama maumivu yanasababishwa na majeraha huwa ufanisi wake unakuwa wa kiwango cha chini.

Dawa, kwa kiwango chake cha dozi, ni salama na haina athari za sumu. Inapoingia mwilini na katika mfumo wa damu, huingia katika ini utendaji wake ini mara nyingi kuiondoa nje kupitia kwenye figo.

Kwa upande wake, dawa ya ibuprofen huwa katika kundi la dawa zenye kuponya majeraha ya mwilini zisizokuwa na homoni za steroide husaidia kupunguza maumivu.

Mara nyingi hutolewa kwa mtu mwenye maumivu yaliyosababishwa na majeraha kama vile maradhi ya mishipa - arthritis, meno au misuli na maumivu yanayosababishwa na hedhi.

Kinyume na paracetamol, ibuprofen haiharibu ini, ingawa kutokana na tiba yake ya kuzuia maumivu yatokanayo na majeraha ya mwilini inaweza kuathiri ute wa utumbo na kuharibu ukuta huu unaolinda tumbo. Lakini itafanya hivyo kwa kiwango kidogo kuliko kundi jingine la dawa za kuponya majeraha ya mwilini.

Paracetamol itayafanya maini yetu kufanya kazi zaidi iwapo tumetumia vilevi.

Tatizo la kumeza paracetamol baada ya kutumia vilevi kwa muda mrefu inahusiana na utendaji mzima wa mwili.

Kwa upande wake, paracetamol pia huingia katika mfumo wa ini kupitia michakato: 80% kwa kupitia mchakato wa asidi na 20% kwa kupitia vimeng'enyo aina ya CYP2E1.

Kama unavyoweza kuona, vimeng'enyo hivi hushiriki katika mchakato wa mfumo wa vilevi na paracetamol. Hapa ndipo tatizo linapotokea.

Kwa hali yoyote ile, tahadhari inapaswa kuchukuliwa ibuprofen inaweza kuzuia usumbufu wa vilevi katika tumbo, kwa kuharibu ukuta wa tumbo.

Lakini hii mara nyingi huwa haitokei baada ya kunywa dozi moja ipasavyo ya dawa hii inayozuia maumivu yatokanayo ya majeraha ya ndani ya mwili ,athari hutokea baada ya kumeza dawa hii mara kwa mara na pale dozi ya juu inapotumiwa.

Hatahivyo, tukumbuke kuwa dawa bora ya uchovu na maumivu ya baada ya kutumia vilevi kwa muda mrefu sio kutumia vilevi. Au, walau sio kutumia kwa kiasi kikubwa.