Kwa nini vijana wengi wanapatwa na kiharusi na shinikizo la damu katika nyakati hizi?

Muhtasari
  • Kwa nini vijana wengi wanapatwa na kiharusi na shinikizo la damu katika nyakati hizi?

Ilikuwa mwaka jana wakati kijana Zakaria (sio jina ake halisi) mwenye umri wa miaka 29 alikuwa amelala kitandani mwake usiku majira ya saa kumi usiku.

Mara alianza kuhisi maumivu ya kifua. Mwili wake mzima ulianza kutokwa jasho. Hapakuwa na mtu mwingine nyumbani wa kumpeleka hospitalini wakati ule.

Maumivu yaliendeelea kumzonga lakini baadaye muda yakakoma na akasinzia.

Hatahivyo hakwenda kumuona daktarin asubuhi yake kwani maumivu aliyokuwa mayo yalikuwa yameisha.

Lakini siku iliyofuata Zakaria ahisi tena maumivu yale ya kifua na kuamua kwenda kumona daktari.

Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa vipimo mbali mbali Zakaria anasema daktari alimshauri akafanyiwe uchunguzi wa kipimo cha echo-cardiogram- kinachochunguza mapigo ya moyo. Kipimo hicho kilifichua kuwa Zakaria alikuwa na mshituko wa moyo, siku iliyotangulia.

Zakaria alishangaa sana wakati aliposikia kile daktari alichokisema. Hakuelewa kuwa mshituko wa moyo unaweza kumptata kijana mwenye umri sawa na yeye./

Maradhi ya moyo husababisha vifo kote duniani vinavyokadiriwa kuwa milioni 17.9 kila mwaka kulingana na ripoti ya Shirika la Afya duniani ya mwaka 2021.

Miongoni mwa waathiriwa wa maradhi haya ni vijana, huku idadi yao ikitajwa kuendelea kuongezeka.

Zaidi ya vifo vinne kati ya vitano vinavyotokea hutokana na mshituko wa moyo au shinikizo la damu, na theluthi moja ya visa hivi hutokea miongoni mwa watu wenye chini ya umri wa miaka 70, kulingana na WHO.

Sababu za kushindwa kufanya kazi kwa moyo

Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo Padma Shri awardee pamoja na Dkt Manchanda wanasema mioyo ya vijana katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikidhoofika

Daktari Manchanda, ambaye kwa sasa anafanya kazi katika hospitali Sir Gangaram Hospital mjini Delhi, anaamini kuwamtindo wa maisha ya kisasa ndio sababu kuu inayodhoofisha mioyo ya vijana.

Kuna sababu tano kuu za 'mtindo wa usio na mpangilio ' miongoni mwa watu hususan vijana . Amezitaja sababu hizo kuwa ni :

  • Msongo wa mawazo katika maisha
  • Tabia ya kula vibaya
  • Matumizi ya muda mrefu ya Kompyuta na vifaa vingine vya kielekroniki
  • Matumizi ya sigara, tumbaku, tabia ya kunywa pombe mara kwamara
  • Uvutaji wa hewa chafu

Inaweza kutokea kwa kijana mwenye umri wa miaka 29 au kwa mwenye umri wa chini ya miaka 21 Dokta Manchanda anamini kuwa mambo haya matano ndio sababu ya kuu zinazosababisha mshituko wa moyo.

Zakaria aliiambia BBC kuwa amekuwa akivuta sigara tangu alipokuwa na umri wa miaka 22. Lakini aliacha kuvuta miaka miwili iliyopita baada ya kupatw ana shikikizo la moyo.

Ingawa sababu ya shinikizo la moyo miongoni mwa vijana huwa mara nyingi haifahamiki, ni ukweli kwamba elimu ni moja ya mambo yanayowapa vijana wengi msongo wa mawazo. Zaidi ya hayo vijana wengi hawala chakula kwa wakati unaofaa na hutumia muda wao mwing katika utumiaji wa vifaa vya kielekroniki.

Madaktari wanaamini kwamba maumivu ya kifua ni dalili muhimu ya shinikizo la moyo. Wakati shinikizo la moyo linapotokea unahisi kana kwamba mtu fulani anakusukuma kwa nguvu kifuani. Hatahivyo dalili inaweza kutokuwa dalili ya shinikizo la moy wakati wote.

Shinikizo la moyo kusababishwa na ukosefu kabisa wa damu inayokwenda kwenye moyo. Mara nyingi hutokea kutokana na kuziba kwa mishipa ya moyo (ateri) , na hivyo kusababisha damu kutofika kwenye moyo. Hali hii husababisha maumivu ya kifua. Lakini wakati mwingine shinikizo la moyo hutokea pasi na maumivu yoyote. Shinikizo hili huitwa 'shinikizo tulivu la moyo '.

Kwa mujibu wa wavuti wa healthdata.org, shinikizo la moyo ni moyawapo ya sababu zinazoongoza za vifo duniani.

Ukitazama maelezo kuhusu sababu mbali mbali za vifo katika mwaka 2016, asilimia 53 kati yao walikufa kutokana na shinikizo la moyo.

Dalili za shinikizo la moyo

Madaktari wanaamini kwamba maumivu ya kifua ni dalili muhimu ya shinikizo la moyo. Wakati shinikizo la moyo linapotokea unahisi kana kwamba mtu fulani anakusukuma kwa nguvu kifuani. Hatahivyo dalili inaweza kutokuwa dalili ya shinikizo la moy wakati wote.

Shinikizo la moyo kusababishwa na ukosefu kabisa wa damu inayokwenda kwenye moyo. Mara nyingi hutokea kutikana na kuziba kwa mishipa ya moyo (ateri) , na hivyo kusababisha damu kutofika kwenye moyo. Hali hii husababisha maumivu ya kifua. Lakini wakati mwingine shinikizo la moyo hutokea pasi na maumivu yoyote. Shinikizo hili huitwa 'shinikizo tulivu la moyo.

Kwa mujibu wa wavuti wa healthdata.org , shinikizo la moyo ni mojawapo ya sababu zinazoongoza za vifo duniani.

Ukitazama maelezo kuhusu sababu mbali mbali za vifo katika mwaka 2016, asilimia 53 kati yao walikufa kutokana na shinikizo la moyo.

Jinsi ya kujikinga na shinikizo la moyo

Daktari Manchanda anasema kwamba ili kuepuka hatari za shinikizo la moyo, vijana wanahitaji kubadili mtindo wao wa maisha.

Anasema kwamba mazoezi mbali mbali kama vile yoga husaidia katika kuzuwia shinikizo la moyo.

"Serikali zinapaswa kuweka kodi za zaidi kwa vyakula visivyo na virutubisho vya mwili vya kutosha, pamoja na bidhaa za sigara. Zaidi ya hayo hatari ya kula vyakula vya haraka haraka( kama chips na vinginevyo) visivyo na virutubisho zinapzswa kuandikwa kwa herufi kubwa , "aliongeza.

Hii haiwezi kutatua tatizo kabisa, lakini inaweza kuongeza uelewa miongoni mwa watu.

Badhiya watu wanasema kuwa magonjwa ya moyo hutegemea kiwango cha Mafuta mtu alichonacho mwilini, kwahiyo ni muhimu kupunguza vyakula vyenye Mafuta mengi kwenye mlo wako wa kila siku. Lakini je ni lipi la kweli kati ya haya?

Kulingana na Dokta Manchanda , mafuta yanaweza kuwa sababu ya shinikizo la moyo lakini Mafuta yaliyotengenezwa na kuwa magumu kabla ya kuyeyushwa yanaweza kuwa sababu ya shinikizo la moyo . Mafuta ya aina hii hupunguza kiwango cha Mafuta mazuri mwilini na kupngeza kiwango cha Mafuta mabaya mwilini. Daktari anasema Mafuta kama

Margarine sio mazuri na anashauri watu wasiyatumie.