Aina 5 ya mazoezi hatari yanayoweza kusababisha majeraha au kifo

Muhtasari

•Mapema mwezi oktoba madaktari walionywa kuhusu mtindo hatari wa kabla ya mazoezi unaoitwa "dry scooping" ambao baadhi ya washiriki wa mazoezi wanafanya.

Image: GETTY IMAGES

Mapema mwezi oktoba madaktari walionywa kuhusu mtindo hatari wa kabla ya mazoezi unaoitwa "dry scooping" ambao baadhi ya washiriki wa mazoezi wanafanya.

Uliohusisha kula virutubisho vya poda badala ya kuichanganya kwenye maji, kama inavyopendekezwa na watengenezaji, kutengeneza kinywaji.

Watafiti, waliohutubia mkutano wa matibabu wa Marekani, walionyesha wasiwasi kwamba vijana wadogo wangeweza kujaribu, wakichochewa na video nyingi za mtandaoni za mtindo huo.

Walichanganua TikTok, wakihesabu mamilioni ya watu waliozipenda video hizo .

Poda za kabla ya mazoezi kwa kawaida huwa na asidi nyingi za amino, vitamini na viambato vingine, kama vile kafeini.

Wazo ni kuupa mwili nguvu kabla ya mazoezi ili kusaidia stamina, ingawa sayansi inayohusishwa na hilo ni dhaifu.

Image: SCHOLAR KASINGA

Hata hivyo jambo ambalo wataalam hawakulizungumzia pia wakati wa kutoa tahadhari hiyo ni kuhusu aina mbali mbali za mazoezi ambazo ni hatari na zinazoweza kusababisha majeraha mabaya au hata vifo.

Unashangaa ni aina gani za mazoezi zinaweza kukufanya uwe hatarini zaidi?

Ingawa zoezi lolote linalofanywa kwa mbinu mbovu linaweza kukuweka katika hatari, baadhi huwa na matatizo zaidi kuliko nyingine.

1.Bicycle crunches

Ni mazoezi yanayoonekana rahisi ukimuona mtu akiyafanya kwani ni kama kuendesha baiskeli .lakini matatizo mengi hutokea wakati unapoibana vibaya misuli yako ya miguu unapotumia kasi kupindukia .

Image: WOMEN'S BUILD

Pana hata uwezekano wa kukatika kwa baadhi ya misuli ya sehemu ya chini ya miguu na uchungu magotini .Endapo hujakuwa ukifanya mazoezi ya kujipasha misuli moto au umesusa mazoezi kwa muda mrefu ,mazoezi aina hii si ya kurukia siku ya kwanza kabla ya mwili kuwa na uwezo wa kuyastahimili .

Wataalam wanashauri uyaanze pole pole na kuzidisha kasi yako pindi mwili wako unapoyazoea .

2. Lat pull-downs (nyuma ya kichwa )

Ikiwa hutambui nafasi hatarishi unazoweka mwili wako, hutaweza kuzuia majeraha.

Image: BODYBUILD.COM

"mazoezi haya yanaweka mkazo mwingi kwenye kapsuli ya pamoja ya bega na hatimaye inaweza kusababisha msukumo au hata kuraruka kwa baadhi ya sehemu za ndani za misuli ya bega " anasema Jessica Malpelli, DPT. Yeye ni tabibu katika Taasisi ya Mifupa ya Florida.

3. The kettlebell swing

Umeziona kengele hizo kubwa zikibebwa na kurushwa na watu kwa uarahisi katika video.Kisha ukajishauri kwamba ni mazoezi unayoweza kuyafanya.umekosea kwa sababu hii ni mojawapo ya aina hatari Zaidi ya mazoezi .

Ingawaje yakifanywa vizuri na ifaavyo ni mazoezi bora ya kujipa nguvu,yanahitaji ufahamu wa mtindo unaotumia .

Wengi hufikiri kwamba mazoezi haya hutumia nguvu nyingi za mkononi lakioni ukweli ni kwamba nguvu za kuzungusha kifaa hiki zinatoka katika sehemu ya chini ya tumbo . ni vyema kujifunza njia bora ya kufanya aina hii ya mazoezi bila kujiumiza .

4. Bent over rows

Mazoezi haya huhusisha kujipinda kwa kila sehemu ya mwili na wakati mwingine usipokuwa mwangalifu unaweza kujiumiza bila kufahamu hadi baadaye wakati uchungu unapozidi .

Wataalam wanashauri kufanya mazoezi haya wakati unapojipinda kuanzia kiunoni na wala sio upande sehemu ya upande mmoja hasa kama hujayazoea .

Wanaofanya vibaya mazoezi haya hujipata na majeraha mabaya ya uti wa mgongo au hata kukatika kwa mifupa inayounganisha misulu ya mgongoni na sehemu nyingine za mwili .

Unaweza kujaribu kuyafanya kwa kutumia mpira maalum unaokuruhusu kujipinda bila kuwa katika hatari ya kuanguka .

5. The Romanian dead lift

Ikiwa imefanywa kwa usahihi, ni mazoezi mazuri kwa mgongo na nyonga. Hata hivyo, ni mojawapo ya njia rahisi zaidi za kuumiza mgongo wako ikiwa hujui unachofanya. Kwa nini?

Wanyanyuaji wengi huzungusha migongo yao wakati wa kuinua au kuweka chini chumba kinachobeba uzani - na mara nyingi wanaweza hata wasitambue kwamba wanachofanya ni hatari .