Jinsi wanawake wa Kenya wanavyoteseka mikononi mwa 'sponsors'

Muhtasari
  • wachanga waliofadhiliwa hulazimisha kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume wazee

Hali ya kutatanisha inaibuka  na imezidi kuibuka kwa muda ambapo vijana wa kike walio na umri wa chini ya miaka thelathini wanapoteza maisha yao ya thamani inayodaiwa kuwa mikononi mwa 'sponsor' wao wanaowadhulumu.

Baadhi ya 'sponsors' wamedai wazi kuwa wamedanganywa katika uhusiano wa kimapenzi kinyume na matakwa yao.

Wanawake wachanga waliofadhiliwa hulazimisha kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume wazee walioolewa kwa miaka kadhaa ambao ni wazee wao wakitafuta maisha ya kifahari,  na ya kuridhisha.

Nikiwa katika ziara yangu nilipatana na wanawake wa chuo kikuu ambao wameponea mikononi mwa 'sponsors', huku baadhi yao wakisiulia changamoto amazo wamepitia wakiwa mikononi mwa 'wababa' hao, kama wanavyojulikana kwa lugha ya mtaa.

Badala yake wanawake hawa wanakabiliwa na changamoto ambazo huishia kuwateketeza kwa njia ya aibu, hata vile ndoto ya maisha ya kifahari inakuwa miraa kwao.

Swali kubwa ambalo tunatafuta kupata majibu ni jinsi wanawake hawa wanavyojikuta wakitangulia ghadhabu za 'sponsors' ambao wanapaswa kuwafurahisha kama malkia wa hadithi.

Lakini ni mambo au changamoto zipi wanapitia mikononi mwa sponsors hawa?

1.Uavyaji mimba

Nilipopatana na Salome alinisimulia jinsi ameavya mimba mara kwa mara ili awe mrembi mbele ya sponsor wake.

Licha ya kutaka kuwa mgonjwa sponsor wake hana haja na mtoto anataka tu kijivinjari, kwa hivyo kulingana na Salome njia bora yao ni kuavya mimba ili waweze kuwekwa maisha ya kifahari.

2.Vitisho

Sio wote ambao watakupenda, bali ukiwatishia kutoa siri zao kwa umma haya basi utapewa vitisho maishani na kuishi na uoga.

Grace alinisimulia hadithi jinsi alitishiwa na sponsor wake baada yake kutaka kumwambia bibi yake kuhusu uhusiano wao, huku akitoroka maeneo hayo na kuanzisha maisha yake upya.

3.Kuuwawa

Tumeona na kushuhudia vifo vya wasichana wadogo wa vyuo vikuu, huku wakiuawa bila sababu, na bila hatia yeyote, kwa sababu tu ya tamaa na sponsor.

Je tabia hii itakoma lini na kweli itakoma kwani karne hii wasichana wengi hawaambiliki bila ya kujua kesho yao.