Fahamu dawa ya PrEP ni nini na inatumika vipi kuepuka maambukizi ya VVU

Muhtasari

•Pre-exposure prophylaxis au PrEP ni matumizi ya dawa za kupunguza makali ya VVU na watu wasio na VVU ili kuzuia upatikanaji wa maambukizi ya VVU.

Image: NIPHON SUBSRI / EYEEM

Katika vita dhidi ya janga la VVU njia kadhaa za kuzuia hutumiwa. Moja ni utumiaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU kama pre-exposure prophylaxis (PrEP).

PrEP ni nini?

Pre-exposure prophylaxis au PrEP ni matumizi ya dawa za kupunguza makali ya VVU na watu wasio na VVU ili kuzuia upatikanaji wa maambukizi ya VVU.

Tangu Septemba 2015, WHO imependekeza kwamba watu walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa VVU, wanaojulikana kama watu walio katika hatari, wapewe PrEP kama chaguo la ziada la kuzuia, kama sehemu ya kuzuia kwa ujumla.

PrEP inapatikana kama tembe na inapaswa kunywe kabla ya kujamiiana kuepuka maambukizi.

Image: CHANZO CHA PICHA,MARC BRUXELLE

Ufanisi wa PrEP ya kumeza umeoneshwa katika majaribio ya kudhibiti na ufanisi huwa juu wakati dawa inatumiwa kama ilivyoelekezwa na CDC, Kituo cha Marekani cha Kudhibiti Magonjwa.

Je, inamlinda mwenzangu?

Inapunguza hatari ya kupata VVU kutokana na ngono kwa takriban 99% inapotumiwa kama ilivyoagizwa.

Ingawa kuna taarifa ndogo kuhusu jinsi PrEP inavyofanya kazi vizuri kwa watu wanaojidunga dawa, CDC inasema inapunguza hatari ya kuambukizwa VVU kwa angalau 74% inapotumiwa kama ilivyoelekezwa.

Hatahivyo, huwa haina ufanisi kama haitatumika inavyopaswa.

Post-exposure prophylaxis, au PEP, ni njia ya kuzuia maambukizi ya VVU kwa mtu asiye na VVU ambaye anaweza kuwa ameambukizwa virusi hivi karibuni.

Inahusisha kuchukua dawa za kuzuia VVU haraka iwezekanavyo baada ya uwezekano wa kuambukizwa na virusi.

PrEP pia inafaa kwa watu wanaojidunga dawa na kuwa na mwenzi aliye na VVU, ambaye wanashiriki naye sindano, au vifaa vingine.

Image: CHANZO CHA PICHA,YAKUBOVALIM

PrEP inamezwa wakati gani?

Sharti la kwanza la kuipata ni kuwasilisha kipimo cha VVU kinachoonesha kutokuwa na maambukizi.

Inaweza kuwa chaguo zuri kwa wale ambao hawatumii kondomu kila wakati, na wale ambao wamegunduliwa na mgonjwa ya zinaa ndani ya miezi 6 iliyopita.

'Nilidhani VVU ni ugonjwa wa vijana' Post-exposure prophylaxis, au PEP, ni njia ya kuzuia maambukizi ya VVU kwa mtu asiye na VVU ambaye anaweza kuwa ameambukizwa virusi hivi karibuni.

Inahusisha kumeza dawa za kuzuia VVU haraka iwezekanavyo baada ya kuwepo uwezekano wa kuambukizwa virusi.

PrEP pia inafaa kwa watu wanaojidunga dawa na kuwa na mwenzi aliye na VVU, ambaye wanashiriki naye sindano, sindano, au vifaa vingine.

Image: CHANZO CHA PICHA,MARTIN HARVEY

Je, tunaweza kupata PrEP barani Afrika?

Kutumwa katika Afrika kunakuja kukiwa na vikwazo mbalimbali kama vile gharama, upatikanaji wa huduma za afya, unyanyapaa… Lakini maendeleo yanazingatiwa hapa na pale.

Dawa ya kuzuia kabla ya kuambukizwa ilipunguza maambukizi mapya ya VVU katika utafiti wa kikundi uliofanywa nchini Burkina Faso, Ivory Coast, Mali na Togo kwa miaka miwili na nusu kwa takribani wanaume 600 wanaofanya ngono.

Dk Safiatou Thiam aliyekuwa Waziri wa Afya na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mapambano dhidi ya Ukimwi nchini Senegal anaeleza kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2021, PrEP imekuwa sehemu ya silaha za kuzuia wataalam wa afya wanaohusika katika mapambano dhidi ya VVU nchini Senegal kupata maambukizi.

Kwa kuongezea, matokeo ya utafiti, uliofanywa Afrika Magharibi na watafiti kutoka Inserm na IRD, na kuchapishwa katika jarida la The Lancet HIV mnamo Mei 25, 2021, yanatia matumaini.

Kulingana na Dk Thiam, nchini Senegal kuna miongozo ya matumizi ya PrEP, ambayo inalenga watu walio katika hatari lakini pia wanandoa ambao mwenzi mmoja ana VVU na mwingine hana.

Watu wengine walio katika hatari ambao hawawezi kutumia kondomu wanaweza pia kutafuta PrEP.

Na ikiwa wanakidhi vigezo, kwa sababu kuna vigezo vinavyohusiana na hatari lakini pia kuna vigezo vya matibabu, hivyo ikiwa watu hawa wanakidhi vigezo, wanaweza kuagiza PrEP, ambayo hutolewa kwao bila malipo.