Fahamu mambo usiyoyajua kuhusu Sadio Mane wa Senegal na Liverpool

Muhtasari
  • Sadio Mane anayevalia jezi nambari 10 , alitimiza ndoto yake ya kihistoria ya kuisaidia timu yake ya taifa Senegal kushinda kwa mara ya kwanza taji la Afrika
Sadio Mane
Image: Hisani

Sadio Mane anayevalia jezi nambari 10 , alitimiza ndoto yake ya kihistoria ya kuisaidia timu yake ya taifa Senegal kushinda kwa mara ya kwanza taji la Afrika.

Mshambuliaji huyo wa Liverpool pia ni maarufu na mzungumzaji. Yeye ni tofauti na wachezaji wengine kama yeye ambao hununua vitu ghali kama vile simu za bei ghali na vitu vinginevyo.

Ni mchezaji anayetoka katika familia masikini ambayo ilikabiliwa na changamoto chungu nzima maishani akiwa mtoto mdogo.

Katika taarifa hii tunakuelezea kuhusu mambo sita kuhusu mchezaji huyu ambaye amepokea uungwaji mkono wa kiwango cha juu mbali na mchezo wake .

1.Alitoroka nyumbani kwao ili kucheza soka

Huenda una ufahamu kuhusu habari hii . Akiwa mtoto mdogo , Mane alikulia katika kijiji kwa jina Bambali nchini Senegal. Wakati huo familia yake haikumruhusu kucheza mpira.

Babake alifariki akiwa na umri wa miaka saba , na alilelewa na wajomba zake. Anatoka katika familia ya Maimamu wa kiislamu. Hivyobasi kitu cha kwanza ambacho mtoto anatarajiwa kupatia kipau mbele ni elimu.

''Baba yangu hakutaka nicheze mpira kwasababu aliamini kwamba elimu ni muhimu kushinda mpira. Ilikuwa vigumu kucheza soka kwasababu yeye hakutaka hivyo'', alisema Mane kwa makala ya BBC.

Mane alielezea kwamba alifurahia sana kucheza soka na hata akalazimika kutumia matunda na mawe akiwa mtoto kwasababu hakuwa na uwezo kupata mpira wakati huo.

2. Kazi ya jamii ya kiislamu

Mane anasemekana kutumia fedha nyingi kuwasaidia masikini katika maeneo mengi ya taifa la Senegal. Alitumia fedha zake kusaidia Watoto wadogo mbali na kuwajengea nyumba na vyoo watu masikini. Mapema kanda ya video ilizua hisia huku wengi wakimsifu.

3.Mzozo wa hali ya tabia nchi Ulaya

Mnamo 2011, Mane aliondoka Senegal na kujiunga na klabu ya Ufaransa ya FC Metz. Kitu cha kwanza alichogundua alipokwenda Ulaya ni baridi.

Mane anazungumzia kilichompata yeye na wachezaji wenzake alipotoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwa amevalia shati pekee. Alijua hali ya hewa ya Afrika mara nyingi ilikuwa ya joto.

"Wote walianza kunicheka na sikuelewa," alisema. "Waliniuliza, 'Unathubutuje kuvaa nguo hizo?'

4.Shinikizo kutoka kwa mashabiki wa timu ya taifa

Kwa muda mrefu, Mane amekuwa akionesha kiwango kizuri katika soka na klabu alizochezea zimenufaika na kazi yake, lakini amefanya machache kwa nchi yake.

Kwa hiyo, licha ya kupendwa na mashabiki wa nchi yake, walikuwa wakimshinikiza kuikuza Senegal.

Mnamo 2017, hakufanya vyema kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika alipokuwa akiichezea nchi yake. Alishindwa kufunga penalti ili kufuzu katika robo fainali.

Mnamo 2019, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya Senegal kupoteza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Algeria 1-0.

Lakini ni wazi, Mane sasa amepunguza shinikizo kwa timu ya taifa, na katika maeneo mengi ya Senegal ushindi wa timu ya taifa uliadhimishwa kila mahali jana usiku. Mane alifunga bao la mwisho la ushindi dhidi ya Misri.

5.Mzozo wa hali ya tabia nchi Ulaya

Mnamo 2011, Mane aliondoka Senegal na kujiunga na klabu ya Ufaransa ya FC Metz. Kitu cha kwanza alichogundua alipokwenda Ulaya ni baridi.

Mane anazungumzia kilichompata yeye na wachezaji wenzake alipotoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo akiwa amevalia shati pekee. Alijua hali ya hewa ya Afrika mara nyingi ilikuwa ya joto.

"Wote walianza kunicheka na sikuelewa," alisema. "Waliniuliza, 'Unathubutuje kuvaa nguo hizo?'