Masomo muhimu kila mwanasiasa anapaswa kujifunza kutoka kwa uongozi wa hayati Mwai Kibaki

Muhtasari
  • Masomo muhimu kila mwanasiasa anapaswa kujifunza kutoka kwa uongozi wa hayati Mwai Kibaki

Siku ya Ijumaa, Aprili 22, 2022 itaishia kuwa moja ya siku za giza, huzuni kubwa maishani mwetu kama Wakenya.

Kifo cha Rais wa awamu ya 3 Jamhuri ya Kenya, Mhe. Emilio Mwai Kibaki kilishangaza taifa ilipotangazwa na rais wa 4 wa jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta katika ikulu ya Nairobi. Kibaki aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 90.

Kazi ya kisiasa ya Kibaki ilianza mwaka wa 1963 kama Mbunge wa Donholm wakati huo (sasa Makadara jijini Nairobi) kabla ya kuhama katika uchaguzi uliofuata hadi eneo bunge la sasa la Othaya, ambako alihudumu kama Mbunge hadi 2001.

Wakati wa baraza la mawaziri la kwanza baada ya uhuru chini ya uongozi wa Rais Jomo Kenyatta, Kibaki aliwahi kuwa Waziri Msaidizi kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha kuanzia 1969 hadi 1982.

Ni katika kipindi chake kama Waziri wa Fedha, ambapo gazeti la Times lilimtaja kuwa miongoni mwa watu 100 wakuu duniani waliokuwa na uwezo wa kuongoza.

Huku Hayati Mwai KIbaki akizikwa nyumbani mwake Othaya siku ya JUmamosi, wanasiasa wanapaswa kujifunza mabo kadha wa kadha, kutokana na uongozi wake wa miaka 10.

Lakini wanasiasa wanapaswa kujifunza nini huku, uchagui wa Agosti ukiwadia?

Haya hapa baadhi ya masomo muhimu wanapaswa kujifunza;

1.Leta mabadiliko

Kama wngi wanavyomkumbuka Mwai Kibaki, wanamkumbuka kwa kuleta mabadiliko katika sekta nyingi nchini kenya.

Kama mwanasiasa unapaswa kuleta mabadiliko katika maisha ya wanachi wako ambao walikuchagua.

2.Kuleta athari

Kama mwanasiasa unapaswa kukumbukwa kwa kuleta atahari katika maisha ya mwananchi wako.

3.Kuleta maendeleo

Je kama mwananchi unaweza sema maendelea mabayo mwanasiasa wako amabaye anawania kiti tofauti katika kaunti yako maendelea ambayo ameweza kuleta alipokuwa kwenye iti chake?

Wananchi wanapaswa kujifuna kuwachagua wanasiasa ambao wataleta maendelea katika wadi yako, wanasiasa wanapaswa kujifunza pia kuleta maendela kwa wananchi na wala sio kutoa ahadi za bure

4.Uongozi ni utumishi

Kama mwanasiasa ambaye amejitolea kuwatumikia wananchi wake, wanapaswa kujifunza kwamba Kibaki aliwatumikia wananchi wake na kwamba wanapaswa kufahamu uongozi ni utumishi, na wala sio kutimizza mahitaji yao wenyewe.