Kupanda kwa viwango vya riba: Jinsi mfumuko wa bei duniani unavyokuathiri, ni nani anayefaidi?

Muhtasari

• Kati ya athari zote ambazo zimechangiwa na kupanda kwa viwango vya riba, lililo dhahiri zaidi ni changamoto ya kudhibiti ongezeko la gharama ya maisha.

Image: GETTY IMAGES

Mfumuko wa bei unaokumba ulimwengu umechangia kupanda kwa viwango vya riba ambavyo vimekuwa vikiongezeka kwa kasi.

Katika juhudi ya kudhibiti ongezeko hilo la mfumko wa bei za bidhaa, nchi katika maeneo tofauti duniani zimeongeza gharama ya pesa, hii ikimaanisha ongezeko la gharama ya mkopo.

Hali hiyo imechangia viwango vya juu sana vya riba, hivyo basi hakuna faida ya mtu yeyote kukopa.

Hali hii imeathiri zaidi makampuni zinazotaka kukopa fedha za kuwekeza, serikali zinazotaka kufadhili matumizi ya umma, na pia huathiri watu wanaohitaji mikopo ya kununua nyumba, gari au kufadhili gharama zisizotarajiwa.

Ni nani anayefanya maamuzi ya kupanda au kushuka kwa viwango vya riba? Benki kuu ya kila nchi inafanya kazi bila kutegemea serikali iliyopo madarakani.

Tangu mfumko wa bei ulipoanza kupanda kwa kasi, kwanza kufuatia athari za janga la covid-19 na kisha kufuatia vita vya Ukraine, mjadala umejikita katika kasi na ukubwa wa mfumuko wa bei.

Hatua zinazochukuliwa na nchi kudhibiti hali hii

Nchini Marekani kwa mfano,Mfumo wa Hifadhi ya Kitaifa (unaojulikana kwa njia isiyo rasmi kama Fed), sawa na benki kuu, umekosolewa vikali kwa "kuchukua muda" kuanza kuongeza viwango.

Mambo yalitulia mwezi Machi wakati ilipoongeza viwango vya riba kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa janga, na kutoa ishara ya kwanza kwamba "zama za mkopo rahisi", kwa viwango vya riba vya chini zaidi, inaelekea kuisha.

Siku ya Jumatano, Fed iliongeza viwango vya riba kwa nusu alama, na kuziacha kwa kati ya 0.75% na 1%, huku nchi ikitumbukia katika lindi la mfumuko wa bei ambayo ilifikia 8.5%, kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 40.

Nchini Marekani, "zama za mkopo wa gharama nafuu" imeisha.

"Mfumko wa bei uko juu sana na tunafahamu fika athari inayotokana na hali hiyo," alisema Mwenyekiti wa Fed Jerome Powell. "Na tunafanya kila juhudi kupunguza."

Kati ya athari zote ambazo zimechangiwa na kupanda kwa viwango vya riba, lililo dhahiri zaidi ni changamoto ya kudhibiti ongezeko la gharama ya maisha.

Benki za Marekani ambazo hazitaki tena pesa za wateja wao.

"Wakati kiwango kinapopanda, kinadharia, mahitaji yanapaswa kuwa ya wastani na hiyo itasababisha shinikizo kidogo kwa mfumuko wa bei," Elijah Oliveros-Rosen, mwanauchumi mkuu katika kitengo cha Uchumi na Utafiti cha Global S&P Global Ratings nchini Marekani, aliiambia BBC Mundo.

"Kupanda kwa viwango vya riba ni mwelekeo wa kimataifa," anaongeza, lakini anaonya kuwa hilo limefanyika kwa kasi tofauti katika sehemu mbalimbali za dunia.

Image: GETT IMAGEES

"Ilianza mwaka jana huko Amerika Kusini. Kisha ikaja Marekani, kisha Uingereza, na hatimaye Asia. Sasa ni zamu ya Benki Kuu ya Ulaya," alisema mwanauchumi huyo.

Haya ni baadhi ya matokeo muhimu zaidi ya kupanda kwa viwango vya riba.

1. Ni ghali zaidi kukopa pesa

Benki za biashara zitakutoza kiwango cha juu cha riba ili kukukopesha pesa.

Hata kama hutakopa moja kwa moja, lakini tumia kadi ya mkopo, inafanya kazi kwa kiwango cha kutofautiana.

Ikiwa hutalipa kwa wakati, "adhabu" itakuja kwa njia ya malipo ya juu zaidi ya riba.

 

2. Himiza uwekaji akiba

Kwa upande mwingine, makampuni hutumia mikopo mingi kuwekeza, hivyo viwango vya juu havihimiza uwekezaji.

Na hii inafanya gharama ya ufadhili wa bajeti kuwa ghali zaidi kwa nchi.

Kwa hivyo wanapotoa dhamana, wanapaswa kutoa kiwango cha juu cha riba ili kuwashawishi wakopeshaji kwamba wanapata mpango mzuri kwa kutoa rasilimali.

Muungano wa Benki Kuu za Afrika katika mkutano wa Dakar.

Kimsingi, serikali inapaswa kuwalipa wawekezaji zaidi.

"Ndiyo maana mtaji unahamia nchi zinazotoa viwango vya juu vya riba ili kutafuta faida bora," Pablo Gutierrez, mtafiti katika Chuo Kikuu cha British Columbia, aliiambia BBC Mundo.

"Kuongeza kiwango cha riba ni kama njia ya kuweka breki kwenye uchumi," Gutiérrez anasema.

Hatimaye, anasema, "kuna ugavi mdogo wa fedha katika uchumi na hivyo shinikizo la chini la mfumuko wa bei."

Lakini kupandisha viwango si kiashiria cha fedha, ndiyo maana kunafanya kazi vyema katika baadhi ya nchi kuliko nyingine.

3. Huendakukaathiri ukuaji wa uchumi

Wimbi la kimataifa la kupanda kwa viwango vya riba "huchangia athari katika ukuaji wa uchumi", anaelezea José Luis de la Cruz, mkurugenzi wa Taasisi ya Mexico ya Maendeleo ya Viwanda na Ukuaji wa Uchumi (IDIC).

Kupanda kwa viwango vya riba huathiri uwezo wa uwekezaji wa makampuni na mahitaji ya mikopo ya watumiaji katika mazingira magumu ya kimataifa.

"Kuongeza kiwango cha riba ni kama njia ya kuweka breki kwenye uchumi," Gutiérrez anasema.

Hatimaye, anasema, "kuna ugavi mdogo wa fedha katika uchumi na hivyo shinikizo la chini la mfumuko wa bei."

Lakini kupandisha viwango si kiashiria cha fedha, ndiyo maana kunafanya kazi vyema katika baadhi ya nchi kuliko nyingine.

3. Huendakukaathiri ukuaji wa uchumi

Wimbi la kimataifa la kupanda kwa viwango vya riba "huchangia athari katika ukuaji wa uchumi", anaelezea José Luis de la Cruz, mkurugenzi wa Taasisi ya Mexico ya Maendeleo ya Viwanda na Ukuaji wa Uchumi (IDIC).

Kupanda kwa viwango vya riba huathiri uwezo wa uwekezaji wa makampuni na mahitaji ya mikopo ya watumiaji katika mazingira magumu ya kimataifa.

Muktadha ambao unaweza kuchangia kufufuka kwa uchumi wa Ulaya, kudorora kidogo kwa baadhi ya maeneo ya Marekani na matatizo yanayotoka China, kwa sababu ya kudorora kwa ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo kubwa ya Asia na matatizo yanayosababishwa na Covid-19, anasema mchumi huyo.

"Ulimwengu unaelekea kwenye mabadiliko kutoka uchumi wa ukuaji wa chini, mfumuko wa bei hadi uchumi ambao utaweza kudhibiti shinikizo la mfumuko wa bei katika miaka miwili au mitatu ijayo, lakini kwa mipaka fulani ya ukuaji," alisema Bw. de la. Cruz katika BBC Mundo.

Uchina: mtoaji mkubwa au mkopeshaji?

Kwa maana hii, "hii ni habari mbaya kwa ulimwengu unaoibuka kutoka katika moja ya mdororo mbaya zaidi wa uchumi katika miaka 90 na kwa mara nyingine tena inakabiliwa na hali ya kiuchumi yenye vikwazo kutokana na shinikizo la mfumuko wa bei, kupanda kwa viwango vya riba na ukuaji dhaifu".

Lakini, ikiwa viwango vya juu vya riba vinaweza kupunguza ukuaji, vinaweza pia kupunguza mfumuko wa bei.

Kilicho wazi ni kwamba kutafuta uwiano sahihi katika maamuzi ya sera ya fedha kulingana na mahitaji ya kila nchi si kazi rahisi.