'Nabii' wa Bungoma mwenye wake 42 asimulia jinsi anavyowaponya wagonjwa

Muhtasari

•  “Huduma zangu zote zinahusiana na Biblia. Mimi ndiye mtu pekee wa Mungu ambaye nitabadilisha injili ya ulimwengu huu," alisema. 

• Nabii aliongeza kuwa Mungu alimpa uwezo wa kutabiri, kuombea wagonjwa na kutibu wagonjwa kwa dawa za mitishamba. 

• Nabii ana maboma matano: matatu Bungoma (Nandolia, Matulo na Webuye), Kitale na Lugari kaunti ya Kakamega. 

Yohana Tano Nabii katika mahojiano katika boma lake la Nandolia Jumatano, Mei 11, 2022. Picha: TONY WAFULA
Yohana Tano Nabii katika mahojiano katika boma lake la Nandolia Jumatano, Mei 11, 2022. Picha: TONY WAFULA

Yohana Tano Nabii, mwenye umri wa miaka 82, kutoka kijiji cha Nandolia kaunti ya Bungoma, ambaye anajiita nabii anadai kuwa amewaponya watu wanaougua UKIMWI, saratani, ukoma na majeraha. 

Nabii huyo ambaye ana wake 42, alizungumza na gazeti la Star katika mahojiano ya kipekee akieleza jinsi ambavyo amewaponya wateja wake wengi kwa kutumia dawa za mitishamba. Alisema anahudumia angalau watu 70,000 kwa mwaka. 

Baba wa watoto 289 alisema anasaidia kuwaunganisha wanaume na wanawake ambao wametaliki. 

Nabii alisema ana Biblia yake, ambayo ina vitabu 69 ambavyo anatumia kufundisha waumini wake katika Kanisa la Muungano.

 “Huduma zangu zote zinahusiana na Biblia. Mimi ndiye mtu pekee wa Mungu ambaye nitabadilisha injili ya ulimwengu huu," alisema. 

Katika mahojiano katika makazi yake ya Nzoia, Nabii alisema alizaliwa mwaka wa 1940 katika eneo ambalo sasa ni eneo bunge la Saboti katika kaunti ya Trans- Nzoia. Babake baadaye alihamia Kanduyi katika kaunti ya Bungoma alipokuwa na umri wa miaka minane kabla ya (Nabii) kuachana na familia yake ili kumtumikia Mungu.

 “Kumtumikia Bwana ni jambo ambalo nilianza muda mrefu uliopita na sijawahi kukata tamaa,” alisema na kuongeza kwamba amekuwa katika utumishi kwa miaka 62. 

Nabii aliongeza kuwa Mungu alimpa uwezo wa kutabiri, kuombea wagonjwa na kutibu wagonjwa kwa dawa za mitishamba. 

Catherine Nalonja mke wa 10 wa Yohana Nabii Picha: TONY WAFULA
Catherine Nalonja mke wa 10 wa Yohana Nabii Picha: TONY WAFULA

Alisema amewaombea mamilioni ya watu kutoka pande zote za dunia. Nabii pia alisema huwa anahudumia wateja bila malipo bila kuomba pesa taslimu, akisema kuwa ni zawadi aliyopewa na Mungu na hataruhusu wateja kumlipa. 

Nabii ana maboma matano: matatu Bungoma (Nandolia, Matulo na Webuye), Kitale na Lugari kaunti ya Kakamega. 

Alisema mke wake mdogo ana umri wa miaka 24, na ujauzito wa miezi sita. Nabii alisema bado ni mchanga na bado ataoa wake zaidi siku zijazo. 

Nabii ana kanisa lake katika boma lake lenye wodi za kulaza wagonjwa walio katika hali mbaya.

"Dawa hizi wakati mwingine zina madhara kwa mwili kwa hiyo katika boma langu nimetenga baadhi ya vyumba ambavyo wagonjwa wanaweza kupumzika na kufanyiwa maombi," alisema. 

Baada ya kuwaombea wagonjwa, anahamia Mto Chwele na kuwabatiza kwa maji, akisema ni njia ya kuosha dhambi zao. 

Bendera ya kanisa la Muungano. Picha: TONY WAFULA
Bendera ya kanisa la Muungano. Picha: TONY WAFULA

"Ninalo shamba kubwa na rasilimali za kutosha kufadhili familia yangu,” alisema. 

Mke wa 10 wa Nabii, Catherine Nalonja, ambaye ni mama wa watoto watano, alisema aliolewa mwaka wa 2002.

Wake wote 42 wanakaa na wana uhusiano mzuri na nabii. Aliongeza kuwa Nabii hana tatizo la kuhudumia familia.

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO.